Ukweli Kuhusu CHADEMA na Harakati Zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli Kuhusu CHADEMA na Harakati Zake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngoromiko, Jun 17, 2012.

 1. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Wana-JF, napenda kuwashirikisha alichosema Mzee Peter Kisumo kuhusu CHADEMA:

  ‘Tatizo kubwa kwenye Chadema kuna wanaharakati na si wanasiasa, na haiwezekani kuongoza serikali kwa kuwa na viongozi wanaharakati’.

  “Hawa Chadema wanachokifanya ni kuvizia makosa madogo madogo ya serikali na kisha kuwashawishi wananchi wawe upande wao,”.

  “Wapo viongozi wa Chadema na waasisi, kama Mzee Edwin Mtei na watu wengine makini ninaowafahamu ndani ya chama hicho, sijawahi kuwasikia wakiropoka hovyo kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa chama hicho.”

  'Ikiwa hulka hiyo itandelea, kuna hatari ya kukosa sifa ya kushika dola vinginevyo watapata shida, kwani hakuna serikali inayoweza kwenda kwa kuendeshwa na wanaharakati'.

  'Inatakiwa chama ambacho kitashinda kiwe na uwezo wa kuongoza katika hali ya amani na utulivu na si kuingia kwenye machafuko mara baada ya uchaguzi'.

  'Ili Chadema ishike dola, ni lazima wajitahidi kujenga safu ya uongozi wa kutawala na si kuwa na viongozi ambao kila wakati wanahamasisha watu kuandamana, kugoma na kuvizia makosa ya serikali iliyopo madarakani'.

  'Wanachokifanya Chadema ni sawa na wawindaji wanaokoka moto kwa ajili ya kuchoma nyama ili hali nyama yenyewe hawajaipata, ..... kazi ya kuing’oa CCM si rahisi kama inavyofikirika'.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani CCM mmejaa watu wapuuzi sijawahi kuona mzee mtei ndiyo msemaji wa chama, hivi chama gani kati ya CCM na chadema kina cho ropoka hovyo, hivi wewe maswala kama ya richmond ni madogo kwako..ina ele kea hajuai kazi ya chama cha siasa kuwa ni kuikosoa lakini namsikitikia kwa kuwa anaita ni maswala madogo madogo wakati sisi wananchi tunayaona ni matatizo makubwa mfano mfumuko wa bei, serikali imeshindwa kuuzuia waziri mkuu anatangaza bei ya sukali isiuzwe zaidi ya 1700 wafanya biashara wana uza zaidi ya 2200 harafu unaita matatizo madomado... hebu tuwekee matati makubwa kwako wewe...........
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni mtanzania yupi mwenye akili timamu anayeweza kushawishika na maneno ya kipuuzi ya hawa Mafisadi wa CCM?
   
 4. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Itafika mahali hata wapumbavu watanena pamoja na uhuni wao wote.
   
 6. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ninaamini tunaweza kujadili bila ya kuitana wapumbavu.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mweleze mpumbavu kwamba yeye ni mpumbavu ili aache upumbavu wake.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Wazee wengi wa CCM kwao uzee ni ugonjwa na si dawa. Matamshi kama haya yametolewa na Wasira nk. Ukweli ni kuwa uwezi kutenganisha siasa na harakati. Na mwanasiasa bora ni lazima awe mwanaharakati, awe na uwezo wa kupambana kwa mbinu za aina zote.
   
 9. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Siku zote ukweli unauma, ccm hawataki kuambiwa ukweli
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Mkuu hakuna jina lingine la mpumbavu. Ubaya zaidi upumbavu uwa ni ngumu kutoka akilini mwa mtu.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mawazo mgando
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ni bora wanaharakati wa chadema kuliko MAJIZI,MAUZA MADAWA YA KULEVYA,MAFISADI,WACHAWI NA WAPUMBAVU waliojaa CCM.na harakati ndio tunazotaka sio porojoporojo za kina mbayumbayu na nepi.
   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Acheni kuwaadaa watanzania nyie wezi wa hii nchi, kazi yenu ni kung'ang'ania kuwa ni hali ya dunia. Hivi mikataba mibovu ya madini inayoipotezea nchi mabilioni ya shilingi ni hali ya dunia? Hivi mikataba mibovu kwenye sekta ya umeme inayoisababishia nchi kulipa mabilioni hewa ni hali ya dunia? Hivi misamaha ya kodi kwa kampuni za madini zinazoinyima nchi mabilioni ya shilingi ni hali ya dunia? Hivi usimamizi mbaya wa fedha za umma na kusababisha watu wachache kuchota pesa kama shamba la bibi ni hali ya dunia? Acheni kuleta siasa maji taka hapa.
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na hizi thread za vichaa waliotoroka mirembe
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  We kweli ngoromiko,na Richmond iko dunia nzima ,?epa,kagoda,wizi wa twiga na uchafu mwingine vyote viko dunia nzima? tukae kimya eti kwa sababu na kwingine yapo? kweli huo ndo upeo wako ulipoishia Great Sinker! aibu yangu mimi
   
 16. m

  msengo2012 Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wazee wangu nchi hii tuna kila kitu isipokuwa tunachokosa ni kimoja tu uongozi bora na siasa safi.Tatizo hapa ni watawala ambao bila shaka ni ccm.Watawala hawa kwa miaka 50 wamekosa dira ya kuingoza nchi hii kuelekea kufaidi neema tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.Wamekuwa ni wabinafsi, wamekosa uadilifu,sio wazalendo,wamekosa pia akili na uelewa wa masuala ya uchumi na hivyo kuachia raslimali za nchi hii kuchukuliwa na wageni bila huruma huku wao wakipewa kitu kidogo sana kwa ajili yao na famiilia zao.Tuache masihara ya kiitikadi ktk masuala nyeti kama haya.Ndugu zangu angalieni mfano wa vinchi vidogo kama Mauritius hawana rasilimali yeyote ni kisiwa kidogo ktk bahari ya Hindi,wanategemea utalii na kilimo cha miwa pekee,angalia walivyopiga hatua.Wana uchumi mzuri,ni mojawapo ya nchi pekee nne Africa zenye uchumi mzuri sana zingine ni Botswana,Gabon na Africa ya Kusini wana literacy rate 85% na ni moja ya nchi zenye utawala bora na democracy nzuri,wamewahi kupata nishani ya Ibrahim kuhusu utawala bora.Sasa sisi tuna tatizo gani hadi tuwe masikini kiasi hiki licha ya rasilimali lukuki na ardhi nzuri tuliyo nayo.
  Tujiulize wananchi tunahitaji kuchukua hatua,na hatua nzuri kwa sasa ni kubadilisha uongozi wa nchi kabisa tuwaone na wengine watafanya nini badala ya kutegemea walewale ambao wametuangusha kwa muda wote huo.Mbona nchi za wenzetu hubadilisha utawala mara kwa mara na wanaendelea mbele,sisi tunaogopa nini?Ni wakati muafaka wa kubadilisha watawala kwani hata wengine wakifanya vibaya si tutawaondoa tu shaka ya nini?
   
 17. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wakubwa!naombeni kufahamishwa jamani,huyu mzee ni nani na yuko wapi anafanya nini,simjui kabisa.anyways yeye anapungukiwa nini ama kuongezewa nini chadema ikiongozwd kiharakati?aseme kipi viongozi wa chadema wametudanganya wananchi juu ya chochote walichosema kwa serikali iliyo oza ya CCM?
   
 18. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  huwi mpumbavu kwa kuitwa,ni sifa uliyonayo,hata usipoitwa utabaki hivyo!
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,829
  Trophy Points: 280
  CCM wanajitekenya alafu wanancheka wenyewe.
   
 20. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Haya maneno hayawezi kueleweka kwa hawa vijana wa cdm wasiojua siasa. Ukweli ndio huo, chadema ni wanaharakati na si wanasiasa.
   
Loading...