Ukweli kesi ya mzungu na airbus yetu.

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.

Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.

Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.

Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.

Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali.

Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.

Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.

KUKAMATWA KWA NDEGE.

Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.

Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.

Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.

Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.

Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.

Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.

Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.

Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.

KUACHILIWA KWA NDEGE.

Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.

Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.

MAMBO MAWILI MUHIMU.

KWANZA
, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.

PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,

mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.

Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).

Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.
 
Deni lisilolipwa muda mrefu huwa mfu?? Jee mzungu anadai au hatudai??

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hizi zote ni athari za maamuzi ya kibabe na kukurupuka ndani ya serikali.
 
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.
Nalipigia debe hili lifanywe
 
Kumbe Jk alishalipa deni hili kwa kiwango kikubwa tu

60% ya deni Jk alishalipa

Huyu Baharia wa Kikwere hatare sana hakuwa busy lakin hela anazo tu
 
Hapo ndio penye utamu wa sheria...
 
Safi kabsa kwa maelezo mazuri na ya kueleweka lkn bado najiuliza Musiba na maelezo yake mpaka sasa anasimama na mguu upi?
 
Wakili Msomi mwenzangu Bashir Yakub, kwanza napongeza elimu uliyoitoa. Lakini, nikusahihishe kidogo. Jaji aliyeendesha Uamuzi(Arbitration) ni Mackanja na si Jaji Makaramba.

Jaji Makaramba alipelekewa Tuzo ya Uamuzi, akiwa Makahama Kuu Biashara kwa ajili ya kuisajili. Hata Makubaliano yaliyoua Tuzo ya mwanzo yalisajiliwa kwake Jaji Makaramba pia. Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom