Ukweli juu ya kukamatwa magari bandarini

Haya yote yanawezekana hapo Tanzania.

Naona mtoa mada na baadhi yawatu wanachangia vizuri na kuwa wa kweli.

Ila wanaokataa kuwa haiwezekani hawajui tu hali ilivyo hapo Tanzania ama wao ni wahusika sasa wanaona kuwa mbinu zao zinawekwa wazi.

Mfano, Jana Dr. Siang'a mkurugenzi wa madawa ameisha wang'ang'ania mahakimu 2 waliokuwa wanapoteza ushahidi kutoka kwa mkemia mkuu wa serikali.

Yaani. Mtu inaonekana anatumia au amekamatwa na drugs/ sembe ila hao mahakimu wanabadilisha majibu ya vipimo na wanasoma kuwa mtuhumiwa hakuwa ama hatumii sembe.

Binafsi, nimekuwa mahala fulani hapo Tanzania miaka imepita kidogo, ila niliyoyaona nikaelewa Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Y

Yaani kumaliza kabisa kirusi cha wizi kutachukua karne kwa taifa letu hili
Muwe mnaanzisha uzi size yenu umekurupuka kuanzishia Uzi kwa vitu usivyovijua.umeulizwa na mdau gari inapokuwa transit half umeishusha ndani inasajiliwajwe Tra.km umeweza kujua ya ndani ya Bandari anashindwa vp kujibu hilo swali.vijana wa Lumumba mnatumika km Condom hajielewi hivi hapo usishangae na ww unasubiri uteuzi wa ukuu wa Wilaya au ubunge wa Africa ya Mashariki.hakuna mjinga anayeweza kufanya michezo hiyo kwa sasa apoteze pesa zake ule ulikuwa ni usanii kuzima swala na mkutano wa Nape na kosa lingine walisahau kubandua no za mbele za lile range aibu ikawakumba
 
Mh kaazi kweli kweli.
Nadhani makosa yalifanyika katika hatua za mwanzo kabisa za design & formation of the great Tanzania.
Maana inaonekana Kama kuna kundi linazuia uporaji Na udanganyifu Na wakati huohuo kuna kundi linawalinda na kuwatetea hao waporaji Na wadanganyifu. Lakini makundi hayo yote ni watanzania!! Kichwa kinauma.
haya ndio matunda ya CCM kwa kutawala TZ kwa miaka 55 hakuna lolote la maana
 
Hivi unapodanganya mfano gari ni ya transit halafu ikabaki humu humu Tanzania hio gari ukitaka kuisajili TRA unaisajili kivipi? maana importation documents si zitahitajika?

Kama aliweza kulipitisha bandarini,sidhani kama atashindwa kulisajili TRA. Pesa itaongea.
 
Siku hizi mizigo ya transit sio dilo tena, maana ili mzigo utoke bandarini dar, lazima kodi iwe imelipwa kwenye nchi unakoenda, na tra hawawezi kitoa release bila kodi kuwa imelipwa
 
rwanda tu ndio wanalipa kodi kwanza ndio mzigo utoke
 
Wanajamvi.
Umuofia kwenu....
Jana nimepata habari za ndani juu ya hili sakata la kukamatwa kwa kontena zikisemekana ni mitumba. Kiufupi hapo zamani watu walidanganya sana nature ya mizigo iliyo ndani ya kontena tena ujanja wao wote walikuwa wakifanya kwa kivuli cha transit cargo.

Ujue transit cargo hapo mwanzo zilikuwa hazilipi VAT na hata ukaguzi wake kwenye scanner ulikuwa hafifu kwani ilikuwa haina maslahi kimapato ingawa hii mizigo ilikuwa inabaki humuhumu. Ujio wa scanner mpya na msimamo wa JPM kuwa lazima kila mzigo upite scanner ndio umefumua madudu mengi.

Kulingana na mtoa taarifa wangu anasema "kweli JPM amefanikiwa kuwapoteza wapiga dili wengi bandarini" kwani pale scanner kuna wanajeshi,TISS,TRA na watu wa bandari. Pia port manager ameweka informers kibao. So ili upige dili hawa wote mpaka uwaweke sawa.

Turudi kwenye mada
Inasenekana huyu Bwana ukwaju aliingiza hizi kontena tangu mwezi wa tisa mwaka jana. Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa ni kawaida ya bwana ukwaju kukwepa kodi kwa njia hiyo ya kusingizia mitumba na pia kufanya ni transit.

Sasa Bwana ukwaju alimtumia dogo flani aende kwenye kampuni ya clearing( sitaitaja) ili mzigo utolewe mwaka huu February. Ujue agent yeye huwa anafanyia kazi taarifa anazoletewa. Sasa Bill of lading ilionuesha ni mitumba. Hii bill of lading inajazwa ulaya wakati agent hayupo so hapa udanganyifu umeanzia kwa shipping line.

Ok agent akaendelea kufanya kazi yake mpaka akawa amepata release order. Lakini ikaja kugundulika mzigo unadaiwa zaidi ya $80,000 ikiwemo na storage charge(kumbuka mzigo wa tangu September mwaka jana) Bwana Ukwaju alikuwa ameshaanza kunegotiate apunguziwe gharama kwa kuwaandikia TRA bila ya agent kujua.

Sasa TRA wakawasiliana na agent kumjulisha juu ya negotiations alizoanzisha bwana ukwaju. Hapa kengele ya hatari ikalia kwa agent. Kumbuka wakati hili kontena linashughurikiwa tayari bwana ukwaju alishaleta kazi nyingine of the same nature kupitia kwa dogo aliyemtuma mwanzo.

Agent baada ya kuwa na mashaka akamwambia dogo anaomba akutane na mwenye mzigo ndipo bwana ukwaju akaenda kwa agent akamwambia yeye achape kazi tu kwani kila mtu ni wake mle bandarini.

Agent kwa kutotaka kuharibika akawaandikia TRA kuwa anajitoa katika shughuri za kushughurikia huo mzigo na atafutwe agent mwingine. Ikumbukwe haya yote yametokea kabla ya kontena kukamatwa au kupita scanner.

Sasa bwana ukwaju sijui alitafuta agent mwingine au la? Lakini inasemekana mzigo haukupita scanner na tayari alikuwa ameshapanga timu yake ili kutoa mzigo. Nadhani kulikuwa na mazingira ya kuzungukana mzigo ukakamatiwa getini ukiwa katika hatua za mwisho za kutoka. Au ni mainformer ndio walitoa taarifa hilo mie sijui. Ndipo mzigo ukaamuliwa urudishwe scanner na ubainika kumbe sio mitumba bali ni range rover.

Bwana ukwaju alishafanikiwa kutoa gari zingine mfano ile inayoonekana ina namba za zanzibar ilishatolewa ikaenda zanzibar na kupewa namba wakati ile gari documents zilionyesha ni transit to zambia.

Ile gari ilikamatiwa zanzibar na inavyoonekana alikuwa anawatumia agents tofauti tofauti. Ile picha inayooshesha gari yenye namba za Zanzibar ni kwenye kituo cha polisi bandari. Kwa hiyo hakuna uongo katika hilo.

Sema sio sawa kusema JPM alikamata yale magari. Magari yalikamatwa either kwa kuzungukana kwenye pesa au kwa mamlaka husika kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kama haya magari yalikamatwa baada ya kuzungukana. Je, nini maana ya kuwa na taasisi nyingi za usalama pale bandari? Inamaana wameamua kujiunga for common interest? Gari ilifanikiwaje kufika geti la kutoka bila ya kupita scanner? This is a home work for JPM.

TUNDU LISSU
Rais wa TLS ameshaingia katika kumtetea Bwana ukwaju. Naomba hili lisichukuliwe kisiasa kwani anatekeleza majukumu yake ya kutetea hata muuaji. Kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa hata akiwa ni muuaji. Lissu amelalamika kwa nini Bwana ukwaju anashilikiwa na polisi kwa siku 23 bila ya kufikishwa mahakamani au kupata dhamana.

Hili nalo ni la msingi ili haki za watuhumiwa zilindwe. Inasemekana Bwana ukwaju ana ukwasi wa kutisha. Inasemekana polisi wananufaika sana na ukaaji wake pale kituoni kwani ukikaa na waridi lazima unukie waridi.
Wasalaam

Ndimu mkata shombo

Nimeipenda iyo police wananufaika na ukaaji wake pale kituoni,,,,,police wa bongo ni mtihani kweli,,,,,,, kwaiyo jamaa atashtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi au vipi,,,, ila ni kijana mdogo ila mpiganaji wa maisha,,,tatizo alishindwa kusoma alama za nyakati,,,,kwamba utawala umebadilika nowdays ,,,,,kwakuwa sio jambazi,,basi Mungu amtilie wepesi ktk case yake,,, kama alivyowatilia wepesi majizi makubwa ya escrow
 
hii ndio bongo aliyeuza cheni kauza cheni bandia na aliyenunua alilipa pesa bandia. kwa kifupi ngoma ni droo.
 
Moderator kwa nini mnaruhusu huyu the banker anakuwa na Ids nyingi anaanzisha Uzi anaanza kujibu kwa I'd nyingine kuweni makini na kazi yenu unganisheni hizo ids
Kaka pliz naomba uniheshimu. Nieleze ni wapi nimejijibu kwa id tofauti. Samahani sana kama michango ya watu imekugusa. Naomba nipigwe ban pale itakapoonekana nimejijibu kwa account tofauti. Mimi humu nimekuwa nikishukuru kwa wanaoleta mwanga zaidi. Kumbuka kuna wanaojua kuliko hata mimi niliyeleta mada. Ishu za wazambia nilikuwa sijui lakini nimejulia humu. Nimejulia humu mbinu mbalimbali zinazotumiwa kusajiri magari ya transit humu n.k. kama wewe ni muhanga wa hii mada i am sorry
 
Mimi sio muhanga ila umeandika vitu usivyovijua hilo bandiko lako ungeliweka kwa mfano wa swali ili tukujulishe.hiyo michezo yote naijua pia Yale ma Range ya juzi ya Jpm ulikuwa ni usanii tu wa kuzima issue ya Nape
 
Lakini kaka bado hujathibitisha ni wapi nilipojijibu kwa id tofauti. Ni bora ungenishauri kama ulivyoshauri kuliko kunipakazia uongo. Then bora unge exhaust yale tu unayoyajua ingetupatua mawazo zaidi.
 
Basi km nimekuhisi vibaya samahani
 
Pesa inavunja milima na ngome.

Kila bonde litasawazishwa na kila goti litapigwa
Kiongozi mimi wala hata sibishani ila ninajiuliza maana ukitaka kusajili itabidi useme gari limetoka wapi limeingia lini Tanzania, wataangalia ushuru umelipwa au bado sasa sielewi kwa kweli..
I
 
Wanajamvi.
Umuofia kwenu....
Jana nimepata habari za ndani juu ya hili sakata la kukamatwa kwa kontena zikisemekana ni mitumba. Kiufupi hapo zamani watu walidanganya sana nature ya mizigo iliyo ndani ya kontena tena ujanja wao wote walikuwa wakifanya kwa kivuli cha transit cargo.

Ujue transit cargo hapo mwanzo zilikuwa hazilipi VAT na hata ukaguzi wake kwenye scanner ulikuwa hafifu kwani ilikuwa haina maslahi kimapato ingawa hii mizigo ilikuwa inabaki humuhumu. Ujio wa scanner mpya na msimamo wa JPM kuwa lazima kila mzigo upite scanner ndio umefumua madudu mengi.

Kulingana na mtoa taarifa wangu anasema "kweli JPM amefanikiwa kuwapoteza wapiga dili wengi bandarini" kwani pale scanner kuna wanajeshi,TISS,TRA na watu wa bandari. Pia port manager ameweka informers kibao. So ili upige dili hawa wote mpaka uwaweke sawa.

Turudi kwenye mada
Inasenekana huyu Bwana ukwaju aliingiza hizi kontena tangu mwezi wa tisa mwaka jana. Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa ni kawaida ya bwana ukwaju kukwepa kodi kwa njia hiyo ya kusingizia mitumba na pia kufanya ni transit.

Sasa Bwana ukwaju alimtumia dogo flani aende kwenye kampuni ya clearing( sitaitaja) ili mzigo utolewe mwaka huu February. Ujue agent yeye huwa anafanyia kazi taarifa anazoletewa. Sasa Bill of lading ilionuesha ni mitumba. Hii bill of lading inajazwa ulaya wakati agent hayupo so hapa udanganyifu umeanzia kwa shipping line.

Ok agent akaendelea kufanya kazi yake mpaka akawa amepata release order. Lakini ikaja kugundulika mzigo unadaiwa zaidi ya $80,000 ikiwemo na storage charge(kumbuka mzigo wa tangu September mwaka jana) Bwana Ukwaju alikuwa ameshaanza kunegotiate apunguziwe gharama kwa kuwaandikia TRA bila ya agent kujua.

Sasa TRA wakawasiliana na agent kumjulisha juu ya negotiations alizoanzisha bwana ukwaju. Hapa kengele ya hatari ikalia kwa agent. Kumbuka wakati hili kontena linashughurikiwa tayari bwana ukwaju alishaleta kazi nyingine of the same nature kupitia kwa dogo aliyemtuma mwanzo.

Agent baada ya kuwa na mashaka akamwambia dogo anaomba akutane na mwenye mzigo ndipo bwana ukwaju akaenda kwa agent akamwambia yeye achape kazi tu kwani kila mtu ni wake mle bandarini.

Agent kwa kutotaka kuharibika akawaandikia TRA kuwa anajitoa katika shughuri za kushughurikia huo mzigo na atafutwe agent mwingine. Ikumbukwe haya yote yametokea kabla ya kontena kukamatwa au kupita scanner.

Sasa bwana ukwaju sijui alitafuta agent mwingine au la? Lakini inasemekana mzigo haukupita scanner na tayari alikuwa ameshapanga timu yake ili kutoa mzigo. Nadhani kulikuwa na mazingira ya kuzungukana mzigo ukakamatiwa getini ukiwa katika hatua za mwisho za kutoka. Au ni mainformer ndio walitoa taarifa hilo mie sijui. Ndipo mzigo ukaamuliwa urudishwe scanner na ubainika kumbe sio mitumba bali ni range rover.

Bwana ukwaju alishafanikiwa kutoa gari zingine mfano ile inayoonekana ina namba za zanzibar ilishatolewa ikaenda zanzibar na kupewa namba wakati ile gari documents zilionyesha ni transit to zambia.

Ile gari ilikamatiwa zanzibar na inavyoonekana alikuwa anawatumia agents tofauti tofauti. Ile picha inayooshesha gari yenye namba za Zanzibar ni kwenye kituo cha polisi bandari. Kwa hiyo hakuna uongo katika hilo.

Sema sio sawa kusema JPM alikamata yale magari. Magari yalikamatwa either kwa kuzungukana kwenye pesa au kwa mamlaka husika kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kama haya magari yalikamatwa baada ya kuzungukana. Je, nini maana ya kuwa na taasisi nyingi za usalama pale bandari? Inamaana wameamua kujiunga for common interest? Gari ilifanikiwaje kufika geti la kutoka bila ya kupita scanner? This is a home work for JPM.

TUNDU LISSU
Rais wa TLS ameshaingia katika kumtetea Bwana ukwaju. Naomba hili lisichukuliwe kisiasa kwani anatekeleza majukumu yake ya kutetea hata muuaji. Kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa hata akiwa ni muuaji. Lissu amelalamika kwa nini Bwana ukwaju anashilikiwa na polisi kwa siku 23 bila ya kufikishwa mahakamani au kupata dhamana.

Hili nalo ni la msingi ili haki za watuhumiwa zilindwe. Inasemekana Bwana ukwaju ana ukwasi wa kutisha. Inasemekana polisi wananufaika sana na ukaaji wake pale kituoni kwani ukikaa na waridi lazima unukie waridi.
Wasalaam

Ndimu mkata shombo
Umeelezea vizuri mwisho ukaingiza siasa kama Bashite,
 
Dah! Hebu mwenye ule mziki wetu pendwa wa Ney Mtegaji aweke hapa turubudike baada ya darasa kuuubwa
 
Hivi unapodanganya mfano gari ni ya transit halafu ikabaki humu humu Tanzania hio gari ukitaka kuisajili TRA unaisajili kivipi? maana importation documents si zitahitajika?
Document zinatengenezwa kaka. hizo kazi za watu.
 
Back
Top Bottom