Ukweli ambao prof.Muhongo ameficha

Ukweli ambao prof.Muhongo ameficha

Prof.Muhongo ana kipaji cha uwongo wanasema kusoma sana mbeleni ni giza nadhani tumemwona hata Prof.Anna tibajuika alivyo muhongo hii inaonyesha maprof.wengi wakiingia kwenye siasa wanachanganyikiwa kabisa JK asipowajibisha Muhongo ntambia uchi mpaka ikulu.
Umebaki muda wa kama saa 24 tu kitendawili kiteguliwe.

Baada ya kitendawili kuteguliwa, ndipo tutakapojua kama 'utatuachia' radhi au utakuwa umenusurika kutembea naked!
 
sasa wewe salary slip huu unaoita ukweli unahusiana vipi na sakata la escrow? mbona hili ni suala la mwajiri na mwajiriwa? na kama hakuna alichofanya si mngemshitaki kwa aliyemteua? sasa huku kutumika kwa niaba ya RAM kwa nini ??? hakuna alichofanya lakini hakuna alichopokea kwenye escrow, vilevile hakuna maamuzi mabovu aliyotoa kwenye escrow. sasa mmekosa ya kumtuhumu mnaanza kupapatika na "ukweli" wenu ambao hata mtu wa kawaida ataona hauna uhusiano na tuhuma mlizomtupia. Ningekushauri wewe na wote mnaotumiwa na RAM, mwacheni aliyemteua aamue bila kumshinikiza na ataamua kwa busara tu....vinginevyo mtusubiri 2015 kama mnavyodai ili muitumie hii kama kete yenu ya kutubwaga...
Nimekopi na kupesti kila kitu kuanzia heading na habari yenyewe hivyo sihusiki kwa lolote lile zaidi ya kuleta hii habari hapa JF na mimi kuchangia kama member wengine.
 
Ni kweli Muhongo hana kosa lolote. Kinachoendelea ni propaganda za Mengi na watu wake aliowahonga
una bifu na Mengi au amewahonga akina nani leta ushahidi acha porojo za kitoto
 
Nimekopi na kupesti kila kitu kuanzia heading na habari yenyewe hivyo sihusiki kwa lolote lile zaidi ya kuleta hii habari hapa JF na mimi kuchangia kama member wengine.

Kwa hiyo chochote unachokiona unafanya copy and paste bila ya kufikiri,waswahili bwana.
 
Why is this becoming too personal? something fishy here
 
ifike sehemu tuwe na utu, waziri muongo amefanikisha mengi japo anapaswa kuwajibika.....ila mchango wake kwenye wizara unajulikana

utaje maana kwa taarifa hii, hakuna jipya aliloanzisha labda la kusema wazawa ni maskini hatuna uwezo wa kuwekeza kwenye umeme na gas
 
chambua habari na utafakari usiwe mtumishi wa watu...
Nimekopi na kupesti kila kitu kuanzia heading na habari yenyewe hivyo sihusiki kwa lolote lile zaidi ya kuleta hii habari hapa JF na mimi kuchangia kama member wengine.
 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, anazidi kuandamwa na kashfa baada ya siri kufichuka kuwa katika uongozi wake hakuna kipya alichofanya zaidi ya kutekeleza miradi na mipango iliyobuniwa na watangulizi wake.

Taarifa za kiuchunguzi kutoka vyanzo mbalimbali na ndani ya Wizara hiyo, zimebaini kuwa sifa anazojipa katika kujinasua na sakata la Escrow, zimejaa propaganda kwa ajili ya kuwadangaya wananchi.

Taarifa za uhakika kutoka vyanzo hivyo, zinaeleza tangu aingie madarakani Mei 2012 baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko Baraza la Mawaziri, hajawahi kubuni kitu kipya kikubwa ambacho kinalenga kuwasaidia Watanzania.

Taarifa zinaonyesha kuwa miradi na mipango yote anayopigiwa debe ilianzishwa kabla ya kuingia madarakani na mingine ilikuwa imeanza kufanya kazi kwa ufanisi.

MGAWO WA UMEME
Moja ya eneo ambalo Profesa Muhongo, anatamba kufanikiwa ni kero ya mgawo wa umeme.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, katika kuhakikisha mgawo huo unadhibitiwa, Rais Jakaya Kikwete aliagiza zitolewe Sh. bilioni 2.4 kila siku kusaidia Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kununulia mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufulia umeme nchini.

Utaratibu huo ulianza kutekelezwa miezi saba kabla ya kuingia madarakani, ambapo wakati huo William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema alikuwa akiongoza wizara.

Chanzo cha habari kinaeleza pesa hizo zinatolewa nje ya bajeti ya serikali na kufanya wizara hiyo kupokea zaidi ya Sh. bilioni 70 kwa mwezi, kitu ambacho kimesababisha baadhi ya wizara kushindwa kufanya kazi kikamilifu kutokana na ukosefu wa pesa.

“Waziri Muhongo ni bingwa wa propaganda anaposema amedhibiti mgawo wa umeme siyo kweli, serikali iliamua kusaidia jambo hili kwa kutoa pesa nyingi, hata angekuwa nani angefanikisha labda aseme lingine,” kilisema chanzo hicho.

Kumbukumbu za wizara zinaonyesha utoaji wa fedha hizo pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

“Sisi kama wabunge tumeziona fedha hizo, tumeamua kukaa kimya kutokana na kutumika katika jambo muhimu katika uchumi wa nchi, lakini inaleta athari kubwa kutokana na miradi mingi katika wizara mbalimbali kushindwa kuendelezwa baada ya pesa nyingi kupelekwa huko nje ya bajeti,” kilidai chanzo chetu.

UMEME VIJIJINI
Suala lingine ambalo Profesa Muhongo anadaiwa kudanganya ni kwamba amefanikiwa kusambaza umeme katika vijiji vingi pamoja na kupunguza malipo ya kuunganisha hadi kufikia Sh. 29,000.

Taarifa zinaonyesha mpango kabambe wa umeme vijijini unaosimamia na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ulianza mwaka 2009 na kuimarika mwaka 2012 chini ya uongozi wa Ngeleja.

Fedha za kutekeleza miradi hiyo imetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) na mfuko wa Marekani wa changamoto za Melenia (MCC) na serikali.

“Wakati REA inasambaza umeme tulikuwa na kigugumizi namna ya watu wa vijijini watakavyomudu kupata huduma hiyo, tukaamua kuanzisha majaribio ya kupunguza malipo ya kuunganisha kwa wilaya mbili,” alisema mtaalamu mmoja kutoka wizarani hapo.

Mpango huo ulifanyiwa majaribio mwaka 2010 na 2011 katika Wilaya za Kilombelo na Mbozi na kuonyesha mafanikio.

“Mpango ulipoonekana unawezekana kuutekeleza ulianza kusambazwa katika mikoa ya Kusini, hivyo hakuna ukweli kwamba yeye ameanzisha,” kilisema chanzo hicho.

MTAMBO WA KINYEREZI
Uchunguzi huo umebaini hata mkakati wa kuanzisha miradi mikubwa ya usafirishaji na kufua umeme ilianzishwa enzi ya Ngeleja, ukiwamo wa ujenzi wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi eneo la Kinyerezi, uzalishaji umeme maporomoko ya Rusumo, usafirishaji wa umeme wa pamoja kati ya nchi za Kenya, Zambia, Burundi na Rwanda.

MFUKO WA MADINI
Katika hatua nyingine, imedaiwa Waziri Muhongo, hakuhusika katika kuubuni mfuko wa kusaidia wachimbaji wadogo kama inavyodaiwa.

Mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2011 ulianza kufanyakazi kwa kusaidia wachimbaji wadogo kwa kuwakopesha mitaji na vifaa vya uchimbaji wa madini.

“Kwa kutumia uungwana, Waziri Muhongo wakati anajisifu kufanya mambo hayo angewataja kwa kuwashukuru waliomtangulia kwa kubuni mipango na miradi hiyo, kuliko kujigamba kwa kitu ambacho binafsi hajahusika nacho,” kilidai chanzo hicho.


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
prof Muongo maisha yake yote amekuwa akishughulika na mawe, miamba na vifusi vya udongo mpaka akapata uprof. Ghafla bin vuu, kapewa hisani kuwa waziri kupitia mgongo wa wassira. Hii ilikuwa kama ajali kazini. Matokeo yake anaongea na watanzania kama ni mawe, miamba na vifusi. hategemei mtoe majibu kwa sababu alivyojisomea na kushughilika navyo havitoi majibu au malalamiko yeyote.
 
ifike sehemu tuwe na utu, waziri muongo amefanikisha mengi japo anapaswa kuwajibika.....ila mchango wake kwenye wizara unajulikana

You must be having a mental block, or mentally challenged if you can not understand the obvious!!bs
 
Hapa badala wa watu kujibu hoja kwa hoja,watakuja na ngonjera za kumuhusisha mmiliki wa chombo cha habari na habari yenyewe.

Huo ndo ukweli wa sio kumuandama Mengi.... tunamjua Mengi kuwa anamchukia Mhongo. Anatumia vyombo vyake kumuandama Waziri kisa alimnyima vitalu vya Gesi.
 
Ngeleja alitoa figures za Wizara alovyoiacha na ilivyo sasa.

If thise figures were accurate they are damning to Muhongo.
 
Kwa mtu mwenye Akili timamu ,hawezi changia na kuanza kuponda bila kujua chanzo cha habarii

Hapo mengi yuko kazini

Etii chanzo NIPASHE
 
Kifupi mi jina hilo najisikia mpaka vibaya kulisikia yaan MUHONGO,CHENGE hawawatu basi tu
 
Nipashe hawawezi kwenda kinyume na bosi wao. Hakika Mengi anatumia kila aina ya silaha aliyonayo kupambana na Prof Muhongo

Kwa hiyo nipashe walichoripoti ni uongo?
Au wameripoti ukweli kwa hasira Au kwa lengo la kumshushia heshima mzee wangu prof. Muhongo?
 
ifike sehemu tuwe na utu, waziri muongo amefanikisha mengi japo anapaswa kuwajibika.....ila mchango wake kwenye wizara unajulikana
Utu mbona upo,yule hana tofauti na kocha wa Chelsea kama unafulsa ya
kupata wachezaji bora duniani kwanini usionekane kocha bora?Vivyo hivyo
Prof,Muhongo alipewa nyenzo karibu zote hata ungekuwa wewe tungekusifia tu!
 
utaje maana kwa taarifa hii, hakuna jipya aliloanzisha labda la kusema wazawa ni maskini hatuna uwezo wa kuwekeza kwenye umeme na gas

Mlitegemea aache yale mazuri waliyoyaacha watanguliziwake? mbona mabaya mf kuvunja mkataba na Mkono & Advocate ameukata ? mkono alikuwa akichota pesa za Tanesco pasina kushinda kesi yoyoteya Tanesco, nani anakumbuka watu wanaoitwa vishoka Tanesco? je bado wapo, sasa hivigharama za kuunganishiwa umeme kwa line mpya unaweza linganisha na za wakati gani tuwe wakweli wadau chuki hazitatusaidia lolote.
 
Back
Top Bottom