Ukwapuaji wa simu Mbeya chukua Tahadhari!

Ukwapuaji wa simu Mbeya chukua Tahadhari!

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
380
Reaction score
534
Kuna kukithiri kwa ukwapuaji wa simu na mikoba hasa kwa wanawake na wadada kwa ujumla ndani ya jiji la Mbeya.

Mama mmoja katika eneo la Sae siku ya Jumapili anatoka getini kwake na kuingia barabari wakwapuaji wanaotumia bodaboda wakaondoka na kibegi chake cha mkononi kikiwa vitu kadhaa ikiwemo simu na kiasi kadhaa cha pesa!

Mkwapuaji mmoja eneo la Isanga alinusurika kuuawa baada ya jaribio lake la kukwapua simu kuingia dosari. Akiwa na pikipiki kwa mwendo wa kasi alikwapua simu na kuondoka nayo!

Mama aliyekwapuliwa alipiga kelele, Bahati nzuri palikuwa na watu waliojipanga vizuri. Muuza chipsi aliyekuwa kando ya barabara alimzuia mkwapuaji na kumpiga na stuli na kufanikiwa kumdondosha huyo kibaka.

Kilichoendelea hapo ni Mungu aliyemuokoa kibaka lakini pikipiki ilibaki majivu.

Kumbuka Ukikwapuliwa simu hakuna msaada wowote unaweza upata polisi zaidi ya loss report ili kurenew laini.
Hivyo Tuchukue tahadhari tusijiachie barabarani maana siyo salama kama unavyodhani.
 
Mbeya walikuwa nyuma sana ,wizi wa ukwapuaji ushaisha ,siku hizoi wezi wanakutolea mfukoni mwa suruali au kwenye pochi au begi....wizi wa VISHANDU ulishaisha.
 
Mbeya inawashamba wengi sana ni basi ushamba kashabebeshwa msukuma lakini mambo hayo mwanza yameisha miaka ya 2010!
 
Aina hii ya wizi imekithiri sana hasa barabara ya Meta na mbalz road .
 
Back
Top Bottom