Stories of Change - 2023 Competition

Mzee Kobelo.

New Member
Mar 23, 2015
3
3
MICHEZO ni mazoezi yahusuyo mwili, ambayo huhusisha ushindani ndani yake.
Ushindani huo hua na taratibu na kanuni kutokana na jamii au mchezo husika.
Kumbuka:michezo ni ajira
Michezo ni afya pia huweza kuondoa msongo wa mawazo.
Kuna wachezaj mbali mbali walio jiajili na wana kipato kizuri ndani na nje ya nchi,
mf
Fiston Mayele,Clatous Chama,Aish Manula, HASSAN MWAKINYO, MESS & RONALD na wengineo.

AINA ZA MICHEZO
Dunian kuna aina nyingi sana za michezo.mfano
I. Mpira wa miguu
II. Mpira wa kikapu
III. Riadha
IV. Mpira wa pete
V. Ngumi n.k

Sasa tuzungumzie michezo maarufu katika nchi yetu na ambayo kama tukiwekeza huko, inaweza kutupa matokeo mazuri ndani ya muda mfupi na kurudisha fedha za uwekezaji kwa haraka . tunahitaj kuwekeza uwekezaji wa muda mrefu ili tuje furahia vipaji vyetu.
ABRAHAM LINCOLN alie wahi kua
Rais wa 16 wa marekani aliwahi sema

" If i had eight hours to chop down a three,i 'd spend six sharpening my axe" kwa kufuata ushauri huo na
Kwa maoni yangu naona katika nchi yetu tumekosa muelekeo mzuri wa wapi twende,kipi cha kufanya na tuanzie wapi?

Tumekua watu wa kutamani mafanikio ya haraka ilihali tukijua fika mafanikio ni mchakato wa muda mrefu ambao unahitaji maandalizi ya muda mrefu pia.

Pia naona ili tufanikiwe kwenye sekta hii ya michezo tunahitaj kuchagua baadhi ya michezo na kuwekeza nguvu zetu huko kama alivyo wahi sema mwanafalsafa

EPICTETUS "Happiness and freedom begin with a clear understanding of one principal,"something are within our control and something are not, the chief task in life is simply this
IDENTIFY and SEPARATE MATTERS so as i can say clear to myself which are external not under my control and which have to do with choises i actually control"

Yafaa tuchague kipi tunawaweza kukimudu, kuliko kung'angania kubeba mzigo wa kg 200 ilihali uzito wetu ni kg 30.

Kwa mimi napendekeza tuchague michezo maarufu katika nchi yetu na dunian ili tuisimamie hio tu na iwe kama alama yetu ya taifa.
Mfano kama nchi za kenya na Ethiopia wamejipambanua kwenye RIADHA.
Afrika kusini wao mchezo unao watambulisha duniani sana ni RUGBY,India wamejikita kwenye Criket,
wenzetu wa Afrika magharibi na kaskazini wao ni soka .
Mfano tunaweza chagua
1.Mpira wa miguu
2.Riadha
3.Masumbwi
Najua kuna michezo mingi imeachwa ila kwa hapa "it's a matter of choose and focus"
Kama wahenga walivyo sema "mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote"
Hivyo jamii na serikali inapaswa kuchagua vichache ili kutilia mkazo huko.

-->MPIRA WA MIGUU ndio mchezo maarufu zaidi dunian,ili sekta hii ikue nchiini na Nchi ipate sifa katika uga wa kimataifa.
Mimi mawazo yangu napendelea kuwe na mfumo mzuri wa ukuzaji vipaji nchini kupitia akademi mahsusi za michezo tajwa hapo juu.

Naamini kungelikua na akademi za michezo nyingi nchini basi vipaji vingi vinavyo potea mitaan kila siku vinge ibuliwa na kutupa faida kama nchi, wachezaji na jamii yetu yote.

Wenye vipaji wengi huishia mitaan na vipaji vyao kupotea na wachache huibuliwa kwenye mashindano kama NDONDO CUP

Katika nchi za dunia ya kwanza vilabu vya mpira na taasisi za michezo husika ndio mahsusi huandaa wachezaj hadi kufikia 'professional level'. Watoto huchukuliwa wakiwa wadogo miaka
6,7-16 na 17

Wachezaj karibia wote ligi za ulaya wanakua wametoka kwenye akademi
Uje kwetu Tanzania sasa 😆😆asilimia kubwa ni walio jikuza wenyewe mitaani.Ndio maana wengi wao hukosa muendelezo.

Ulaya wanakuza vipaji kwenye akademi Hii ni kutokana na wao kua na uchumi imara hadi vilabu vinaweza kujiendesha kwa faida.

Ila kwa nchi zetu za dunia ya tatu kusini mwa jangwa la sahara imekua ni vigumu kwa vilabu vya mpira au akademi za michezo kukuza wachezaj kwasababu ni mchakato wa muda mrefu unao chukua karibia miaka 10 na zaidi Na ni gharama ukizingatia vilabu vyetu karibia vyote havina uwezo huo wa kiuchumi wa kujenga miundombinu ya akademi na pia wazazi wengi hawawezi somesha watoto kwenye akademi hizo kwasababu ya gharama Ni kubwa na kipato ni kidogo.

"HIVYO MAWAZO YANGU KUA SERIKALI IINGILIE KATI KATIKA UKUZAJI HUU WA VIPAJI VYA WANAMICHEZO".
Serikali kwa kushirikiana na taasis za michezo husika zishirikiane kuanzisha akademi kwa muundo huu ufuatao.

MOJA kati ya mwanafalsafa mkubwa Alie wahi kuishi Duniani PLATO yeye aligawa akili za binadamu katika makundi matatu.
1.wenye uwezo mkubwa kiakili.
2.Wastani
3.Chini.

kwa kutumia mawazo yake serikali nyingi zilianzisha mfumo wa elimu ulioendana na mawazo hayo ya PLATO.
Hata nchi yetu pia tunatumia mfumo huu huu kugawa wanafunzi na shule wanazo takiwa kusoma.
Ndio maana shule zetu hasa kuanzia elimu ya sekondari ziligawanywa katika makundi.

Mfn tuna shule za vipaji maalumu (wale wenye ufaulu wa juu zaidi darasa la 7) kama IYUNGA TECH, ILBORU,IFUNDA TECH N.K

shule hizi ni maalumu na zipo kwenye mikoa michache tu ya Tz.
Pia tuna shule nyingi sana za kata na hizi ni kwa wale wenye ufaulu wa wastani.Mfano Ihanga mbarali sec,igomelo sec n.k

Kwakua tunamfumo huu wa kuchuja wanafunzi wenye IQ kubwa na kuwapeleka kwenye shule zao maalumu tunazo ziita vipaji maalumu.

basi pia tunaweza anzisha mfumo huu huu wa kuchagua wanafunzi wenye vipaji maalumu vya michezo na kuwapeleka kwenye akademi maalumu za kukuza vipaji vyao kwakua naamini kucheza ni kipaji maalumu kama kua na akili kubwa tu,

Vyote ni vipaji kwakua Mungu hawezi kutuweka wote katika eneo moja.

Kuna mwanamichezo mmoja yeye aliwahi sema "Mpira huchezwa akilini zaidi miguu ni kama kifaa tu"

Kwakua imekua ngumu kwa vilabu vyetu na taasis za michezo kuandaa akademi basi ni rai yangu
SERIKALI IANZISHE shule maalumu hizi za vipaji maalumu kwa wanamichezo tu katika kila kanda nchini tunaweza anzia hapo kwani kujenga kila mkoa ni gharama na itakua mzigo zaidi kwa serikali.

SERIKALI IANZISHE shule 7 tu nchi nzima katika kanda hizi👇👇
1.kanda ya kati(Dodoma)
2.kanda ya ziwa(Mwanza)
3.kanda ya mashariki(Morogoro)
4.Kanda ya nyanda za juu kusini (Mbeya)
5.kanda ya kaskazini (Arusha)
6.kanda ya magharibi (Kigoma)
7.kanda ya kusini (Lindi).

Naimani serikali na vyama vya michezo haviwezi shindwa kujenga 'sports center' 7 nchini kwa kushirikiana.
Tukijenga hizi 'sports center' 7 kwenye kila kanda ni imani yangu baada ya miaka kadhaa nchi yetu itaweza kuzalisha na kukuza vipaji vingi tutakavyo vitumia katika nchii hii

Kwa kushirikiana na mawakala na akademi za nje ya nchi pia tunaweza uza wachezaj hao kwenda kwenye nchi zilizo endelea zaidi kimichezo na kimaslahi.

--->kwakua tunatakiwa kuchagua na kufocus basi kwenye vituo hivi tuchague michezo michache inayopendwa zaidi na inayoweza kutupa matokeo ya haraka.
Kama
1.MPIRA WA MIGUU
2.RIADHA
3.NGUMI
Kwenye vituo hivi tuanze kuchukua watoto wenye vipaji kuanzia miaka 10-12. Ambao watafunzwa misingi yote ya michezo husika kwa miaka kadhaa hadi kuhitimu.
Pia kufundishwa uzalendo na kujituma katika michezo.

Watoto hawa watachujwa kwenye michuano ya UMITASHUMTA na UMISETA pia na wale waliokosa nafasi ya kusoma shule hizi za msingi na sekondari nao wakionekanaa wana vipaji vya Kuendelezwa wajumuishwe kwenye akademi hizi.

Wakati wanafunzi wakiendelea kusoma kuhusu michezo pia kwa kiasi wanaweza endelea kufunzwa elimu rasmi ila itakayotoa nafasi kwa vijana hao kutumika zaidi kwenye michezo
(Tunaweza kuiga mitaala ya wenzetu hasa ulaya kwa wenye akademi)

WALIMU WA AKADEMI ZA MICHEZO
walimu katika shule hizi wawe ni wale waliopitia mafunzo ya ukocha na kufuzu.

Pia serikali ianzishe elimu hii ya ukocha kwenye baadhi ya vyuo ambao walimu hao ndio watakao kwenda kwenye shule zetu za msingi na sekondari kuchagua vipaji vya wanafunzi na kuvilea pia watakua wanachuja wanafunzi hao kupitia mazoezi ya kila siku na kwenye mashindano ya UMITASHUMTA NA UMISETA.

na pia wao ndio watakao pendekeza majina ya watoto wanaostahili kwenda kwenye vituo hivyoo vya malezi ya vipaji.

MFUMO WA MALIPO YA ADA
ELIMU siku zote ni ghari.
Ukiona elimu n ghari basi jaribu ujinga ambao ni ghari zaidi.
Kwakua serikali inagharamia kwa kiasi kikubwa kwenye shule za vipaji maalumu (high IQ).
naimani ikiweka nia pia inaweza gharamia vipaji hivi maalumu vya michezo kwa wanafunzi wenye vipaji vya michezo, wanafunzi wanao hitaji msaada huu wata vumbuliwa na kuibuka.

Kwakua wanafunzi wenye vipaji ni wengi ila wengi wao hawana uwezo wa kulipa hizo ada basi serikali ishirikiane na BMT,TFF na mashirikisho mengine ya michezo. Wanaweza lipia ada kwa zaidi ya asilimia 70% , zilizo baki wazazi walipie. Ila kwa wanafunzi wenye wazazi wenye uwezo huo wa kulipia walipie( in full payment).

Kwa wasio na uwezo kabisa ila wana vipaji vya hali ya juu (promising player) wanaweza someshwa kwa mkopo kwani michezo ni ajira na inalipa pesa nyingi hivyo kukopesha vipaji hivyo ni uhakika pesa ya mkopo itarudi.

HITIMISHO
Michezo ni ajira kubwaa kwa sasa, Michezo hutuletea taifa heshima, Michezo hutupatia fedha za kodi na kukuza vipato vya wanamichezo na jamii inayo wazunguka,Michezo pia ni afya.
TUKIWEKEZA TUTAWEZA
 
Uje kwetu Tanzania sasa asilimia kubwa ni walio jikuza wenyewe mitaani.Ndio maana wengi wao hukosa muendelezo.

SERIKALI IANZISHE shule 7 tu nchi nzima katika kanda hizi

Lkn kwel
 
Back
Top Bottom