Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM?

Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM?

Kilimasera, mimi sitetei kujengwa ukuta kwa sasa wakati kuna matatizo mengi zaidi wangeweza kutatua

Nilikuwa namjibu huyo aloshangaa idea ya chuo kikuu kuwekewa ukuta kama ni maajabu ya dunia wakati vyuo vikuu vikubwa dunia vimezingirwa kwa kuta.

nimekupata sana mkuu wala usihofu ni idea tu tunabadilishana mawazo then nadhani wahusika kama wanapita humu wanaweza kuyafanyia kazi mawazo yetu!
 
basi wangesema wanaweka mipaka na mpaka sio ukuta tu mpaka unaweza kuwa hata kupanda miti

Kwani weye umewekwa fence ya miti kwa hiyo house yako?. jamani watz waweza vamia wakijua ni pori la muwekezaji, acha watujengee fence siye tuwe tunasomea pembezoni mwa sam nujoma
 
Issue ya mabweni ni suala la kuingia kwenye Ubia wa biashara na wawekezaji wa hapo ndani ya nchi tu

Chuo kinatoa eneo, developer anajenga bweni, anakusanya hela yake kutoka kwa kodi, zikitimia bweni linageuka mali ya chuo.

Inategema developer atajenga bweni lenye kiwango gani, I mean anaweza jenga bweni ambalo by the time amemaliza kukusanya pesa yake na faida juu, bweni liko hoi au linabomoka kabisa.
 
chuo kikuu cha dar es salaam (udsm), kinatarajia kujenga ukuta kuzunguka eneo lote la chuo hicho, ili kukabiliana na kile ambacho uongozi wake umekiita tishio la uhalifu na uvamizi wa eneo hilo.

Makamu mkuu wa chuo hicho, profesa rwekaza mukandara alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee itakayoongozwa na rais jakaya kikwete huko ikulu leo usiku ya kuhamasisha ujenzi wa kituo cha wanafunzi cha kujisomea kitakachogharimu takribani sh18 bilioni.

Profesa mukandara alisema kuwa ujenzi huo umo katika mpango kabambe wa chuo hicho wa kubadili sura yake na akadokeza kuwa yatajengwa mabweni ya kuhifadhi wanafunzi wapatao 4,500. Alitaja huduma nyingine zitakazotengewa maeneo kuwa ni za intaneti, ofisi za vyama na makundi tofauti ya wanafunzi, mgahawa, maduka ya vifaa vya kitaaluma, huduma za utoaji nakala, uchapaji na maktaba kwa ajili ya wanachuo wa shahada za juu.

Tunaupongeza uongozi wa udsm kwa kufikiria kubadilisha sura ya chuo hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakipanui huduma zake wakati idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kwa kiwango cha kutisha kila mwaka.

Tunaupongeza uongozi huo pia kwa kubuni mbinu za kuchangisha fedha za kuwezesha kufanyika mabadiliko hayo, hasa pale tunapoambiwa kuwa wafanyakazi wa chuo hicho tayari wamechangia zaidi ya sh1.3 bilioni. Ni kitendo kinachohamasisha kila mmoja wetu kuchangia mradi huo mkubwa na tunadhani rais kikwete usiku wa leo atatumia mafanikio yaliyopatikana kuwahamasisha wengine kutoa michango yao kwa chuo hicho kikongwe kuliko vingine hapa nchini.


Pamoja na kupongeza juhudi hizo ambazo profesa mukandara alizitangaza juzi, tungependa kutoa angalizo kwamba udsm kamwe haihitaji kupoteza mabilioni ya fedha katika kujenga ukuta wa kuzunguka chuo hicho na kwamba isirudie makosa yaliyofanywa na vyuo vingine, kikiwamo chuo kikuu cha dodoma (udom), kutumia mabilioni ya fedha kujenga mabweni ya kuhudumia maelfu kwa maelfu ya wanafunzi, badala ya kujihusisha na ujenzi au upanuzi wa miundombinu inayoweza kuhimili vilivyo idadi ya wanafunzi waliopo na watakaojiunga na chuo hicho miaka ya usoni.

Udsm lazima itumie rasilimali zake kwa kuangalia vipaumbele. Kwanza, tatizo la wizi katika chuo hicho halitokani na wavamizi kutoka nje bali tatizo hilo kwa miaka nyingi kitovu chake kimekuwa humohumo, kwa maana ya baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi ambao wamekuwa wakiiba mali za chuo.

Kwa ulinzi uliopo chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na kituo kikubwa cha polisi na kikosi imara cha mgambo wenye silaha, haiwezekani vibaka au mtu mwingine anayejitakia mema kuingia humo na kuiba pasipo ‘ruhusa’ ya wenyeji.

Udsm iepukane na mbinu zilizopitwa na wakati. Uwapo wa ukuta hautasaidia kitu. Katika ulimwengu wa leo zinahitajika mbinu za kisasa kama kuweka kamera katika sehemu muhimu na kufunga mitambo na vifaa vingine vya kupekua magari, wafanyakazi na wageni wanaoingia na kutoka, bila kusahau kutoa ajira kwa wafanyakazi waaminifu tu.

Mipaka ya udsm imekaa vizuri iwapo mfumo wa ulinzi tulioutaja hapo juu utasimamiwa vizuri na ingefaa uongozi wa chuo hicho ujue kwamba vyuo vikuu popote duniani havijifungii ndani ya uzio kwa visingizio vyovyote vile.

Kwa upande wa ujenzi wa mabweni, uongozi wa udsm ungefaa pia ufahamu kwamba biashara ya ujenzi wa mabweni katika vyuo popote duniani hufanywa na sekta binafsi au mashirika ya biashara kama ilivyo kwa hosteli za mabibo. Kazi ya serikali au vyuo vyenyewe ni kuwapa fursa wawekezaji kufanya kazi hiyo, ingawa mabweni machache yanaweza kuwapo ili kuwasaidia wanafunzi wanaotoka nchi za nje katika mwaka wao wa kwanza.

Vinginevyo, udsm na vyuo vingine vijifunze kutumia rasilimali chache zilizopo kwenye miradi yenye vipaumbele kama vile vingine ambavyo profesa mukandara alitangaza juzi. Tunakitakia udsm mafanikio katika harambee yake leo usiku.

huo ukuta utausisha na majengo ya mlimani city au? Maana nasikia ni eneo la chuo kikuu cha dsm
 
Naona kuna mawili hapa.kweli pale chuoni wizi ni mkubwa sana hasa kwa wanaokaa pale,geti maji,darajani,kileleni nk kila kukicha unakuta magari yamevunjwa,vitu vimeibwa,njia za panya zipo nyingi za kwenda changanyikeni,ubungo msewe,na makongo,huenda ukuta ukasaidia kupunguza wizi.la pili mabweni yatawasaidia wanafunzzi kuepuka adha ya kupanga mitaani,kusoma zaidi bila matatizo,mimi binafsi nakaa ndani ya chuo naelewa uhalisia wa hali yenyewe.Lakini kwa mtizamo wangu suala la kipaumbele hapa ni kujengwa kwa madarasa ya kutosha na mabweni,ukuta unaweza kupewa last priority kwani kitaaluma hauna maana sana,vyuo vingi havina ukuta,cha msingi waongeze walinzi wa kutosha, waboreshe kituo cha afya,mabweni,miundombinu ya chuo bado mibovu.La mwisho na la uhakika UDASA hawakipendi chama Tawala na ktk uchaguzi uliopita mbunge wao pale chuo alipata kura 7 tu kikwete ndo alianguka vibaya naona kuaandaa sherehe ikulu ni njia mojawapo ya kurudisha imani ya wahadhiri wa UDSM kwake ana kwa chama tawala.
 
Naona kuna mawili hapa.kweli pale chuoni wizi ni mkubwa sana hasa kwa wanaokaa pale,geti maji,darajani,kileleni nk kila kukicha unakuta magari yamevunjwa,vitu vimeibwa,njia za panya zipo nyingi za kwenda changanyikeni,ubungo msewe,na makongo,huenda ukuta ukasaidia kupunguza wizi.la pili mabweni yatawasaidia wanafunzzi kuepuka adha ya kupanga mitaani,kusoma zaidi bila matatizo,mimi binafsi nakaa ndani ya chuo naelewa uhalisia wa hali yenyewe.Lakini kwa mtizamo wangu suala la kipaumbele hapa ni kujengwa kwa madarasa ya kutosha na mabweni,ukuta unaweza kupewa last priority kwani kitaaluma hauna maana sana,vyuo vingi havina ukuta,cha msingi waongeze walinzi wa kutosha, waboreshe kituo cha afya,mabweni,miundombinu ya chuo bado mibovu.La mwisho na la uhakika UDASA hawakipendi chama Tawala na ktk uchaguzi uliopita mbunge wao pale chuo alipata kura 7 tu kikwete ndo alianguka vibaya naona kuaandaa sherehe ikulu ni njia mojawapo ya kurudisha imani ya wahadhiri wa UDSM kwake ana kwa chama tawala.
mbaya chuo kimeruhusu siasa kuingia hapo sasa mtakoma mpaka quality ishuke mie nilidhani vyema chuo kingejitenga kabisa na siasa!ila tu ihusike pale kwenye jambo muhimu kama kutatua matatizo lakini cha ajabu mpaka viongozi wa serikali ya wanachuo wamejiingiza kwenye siasa za nchi kitu ambacho nio nje kabisa ya chuo!
 
Mbinu za kuboresha ulinzi na usalama zilizopendekezwa na huyu aliyeweka thread hii ni bora zaid kuliko kuweka uzio. UDSM sio secondari hadi iwekewe uzio hayo mabilioni ya pesa yatakayotumika kuweka uzio ni bora yakatumika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Lecture theaters nyingi bado haziendani na idadi ya wanafunzi. Uwiano wa vitabu na idadi ya wanafunzi bado haviendani..

Hii imekaa kifisadi. Itapigwa manunuzi ya umma, watu tachukua 10% - 50%. Hivi kweli ni busara kujenga madarasa ilhali lecture theatres na ofisi za waalimu hazitoshi? Wako wapi wataalamu wa strategic plan? Iko katika vipaumbele ambavyo vimeainishwa katika mpango mkakati?
 
Back
Top Bottom