Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 20, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kinatarajia kujenga ukuta kuzunguka eneo lote la chuo hicho, ili kukabiliana na kile ambacho uongozi wake umekiita tishio la uhalifu na uvamizi wa eneo hilo.

  Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandara alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee itakayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete huko Ikulu leo usiku ya kuhamasisha ujenzi wa kituo cha wanafunzi cha kujisomea kitakachogharimu takribani Sh18 bilioni.

  Profesa Mukandara alisema kuwa ujenzi huo umo katika mpango kabambe wa chuo hicho wa kubadili sura yake na akadokeza kuwa yatajengwa mabweni ya kuhifadhi wanafunzi wapatao 4,500. Alitaja huduma nyingine zitakazotengewa maeneo kuwa ni za Intaneti, ofisi za vyama na makundi tofauti ya wanafunzi, mgahawa, maduka ya vifaa vya kitaaluma, huduma za utoaji nakala, uchapaji na maktaba kwa ajili ya wanachuo wa shahada za juu.

  Tunaupongeza uongozi wa UDSM kwa kufikiria kubadilisha sura ya chuo hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakipanui huduma zake wakati idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kwa kiwango cha kutisha kila mwaka.

  Tunaupongeza uongozi huo pia kwa kubuni mbinu za kuchangisha fedha za kuwezesha kufanyika mabadiliko hayo, hasa pale tunapoambiwa kuwa wafanyakazi wa chuo hicho tayari wamechangia zaidi ya Sh1.3 bilioni. Ni kitendo kinachohamasisha kila mmoja wetu kuchangia mradi huo mkubwa na tunadhani Rais Kikwete usiku wa leo atatumia mafanikio yaliyopatikana kuwahamasisha wengine kutoa michango yao kwa chuo hicho kikongwe kuliko vingine hapa nchini.


  Pamoja na kupongeza juhudi hizo ambazo Profesa Mukandara alizitangaza juzi, tungependa kutoa angalizo kwamba UDSM kamwe haihitaji kupoteza mabilioni ya fedha katika kujenga ukuta wa kuzunguka chuo hicho na kwamba isirudie makosa yaliyofanywa na vyuo vingine, kikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kutumia mabilioni ya fedha kujenga mabweni ya kuhudumia maelfu kwa maelfu ya wanafunzi, badala ya kujihusisha na ujenzi au upanuzi wa miundombinu inayoweza kuhimili vilivyo idadi ya wanafunzi waliopo na watakaojiunga na chuo hicho miaka ya usoni.

  UDSM lazima itumie rasilimali zake kwa kuangalia vipaumbele. Kwanza, tatizo la wizi katika chuo hicho halitokani na wavamizi kutoka nje bali tatizo hilo kwa miaka nyingi kitovu chake kimekuwa humohumo, kwa maana ya baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi ambao wamekuwa wakiiba mali za chuo.

  Kwa ulinzi uliopo chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na kituo kikubwa cha polisi na kikosi imara cha mgambo wenye silaha, haiwezekani vibaka au mtu mwingine anayejitakia mema kuingia humo na kuiba pasipo ‘ruhusa’ ya wenyeji.

  UDSM iepukane na mbinu zilizopitwa na wakati. Uwapo wa ukuta hautasaidia kitu. Katika ulimwengu wa leo zinahitajika mbinu za kisasa kama kuweka kamera katika sehemu muhimu na kufunga mitambo na vifaa vingine vya kupekua magari, wafanyakazi na wageni wanaoingia na kutoka, bila kusahau kutoa ajira kwa wafanyakazi waaminifu tu.

  Mipaka ya UDSM imekaa vizuri iwapo mfumo wa ulinzi tulioutaja hapo juu utasimamiwa vizuri na ingefaa uongozi wa chuo hicho ujue kwamba vyuo vikuu popote duniani havijifungii ndani ya uzio kwa visingizio vyovyote vile.

  Kwa upande wa ujenzi wa mabweni, uongozi wa UDSM ungefaa pia ufahamu kwamba biashara ya ujenzi wa mabweni katika vyuo popote duniani hufanywa na sekta binafsi au mashirika ya biashara kama ilivyo kwa Hosteli za Mabibo. Kazi ya serikali au vyuo vyenyewe ni kuwapa fursa wawekezaji kufanya kazi hiyo, ingawa mabweni machache yanaweza kuwapo ili kuwasaidia wanafunzi wanaotoka nchi za nje katika mwaka wao wa kwanza.

  Vinginevyo, UDSM na vyuo vingine vijifunze kutumia rasilimali chache zilizopo kwenye miradi yenye vipaumbele kama vile vingine ambavyo Profesa Mukandara alitangaza juzi. Tunakitakia UDSM mafanikio katika harambee yake leo usiku.
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni aibu sana kama huo ukuta utajengwa. Hii itafanya chuo hiki kutokuwa tofauti na sekondari ya jitegemee
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hapo sasa siasa zimeingia chuo hakuna kuruka ukuta wala wanafunzi kutoroka udsm mnakua watoto wa geti kali
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ndio mara yako ya kwanza kusikia chuo kikuu kimezingirwa na ukuta?
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mhhhh bado sijaelewa huo ukuta,kweli tumevamiwa na wanasiasa.
   
 6. k

  kamanzi Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Upuuzi katika hili sio kwamba ukuta ni mbaya bali sio kipaumbele. Wakati wa lecture pale mlimani kuna wanafunzi wanakaa chini. Wengine wanakuwa nje ya darasa maana kumbi ndogo. Mtu asiye na akili "brand new" kama akina Mukandara angefikiria kujenga lecture halls kubwa na za kisasa au/na kuongeza idadi ya wahadhiri ili wanafunzi wasome kwa ustaarabu. Kwenye nchi zingine tena hapo hapo SADC darasa iwe ni la vidudu au chuo kikuu haliruhusiwi kuwa na zaidi ya wanafunzi 30. Sasa hizo pesa za kujenga ukuta kwanini wasifikirie kujenga modern and bigger lecture halls na kusomesha au/na kuajiri wahadhiri wengi zaidi? Kwanza tatizo la UDSm kwa sasa na sababu ya kushuka kiwango ni kukosa ku-attract wahadhiri wenye sifa za kimataifa. Ukiwauliza akina Mukandara watakwambia watanzania wanatosha lakini maana ya University ni uwezo wa chuo kuwa na universal representation ya wahadhiri na wanafunzi pia. Ndio sababu UDSM ilikuwa ikisifika mno miaka ile walipokuwepo watu kama Professa Walter Rodney (the author of the famed book, "How Europe Underdeveloped Africa") na akina Wamba Dia Wamba. Leo hii chuo kina vilaza kama Benson Bana wa REDET. Nyie jengeni ukuta wakati kiwango cha chuo kinazidi kuporomoka. Ndio maana pamoja na kuwa chuo bora tanzania, Colleagues wangu wanaiita UDSM "glorified secondary school.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mzee umenena lakini tatizo la sasa pale ni impact of politics entered at udsm kila siku yatazuka mapya poleni sana!!!
   
 8. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbinu za kuboresha ulinzi na usalama zilizopendekezwa na huyu aliyeweka thread hii ni bora zaid kuliko kuweka uzio. UDSM sio secondari hadi iwekewe uzio hayo mabilioni ya pesa yatakayotumika kuweka uzio ni bora yakatumika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Lecture theaters nyingi bado haziendani na idadi ya wanafunzi. Uwiano wa vitabu na idadi ya wanafunzi bado haviendani..
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwani chou ni gereza hadi kiwe na ukuta?
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Baada ya REDET kuishia, nini kinafuata katika utekelezaji? Waafrika, hata waliosoma tuna matatizo sana. Utakuja sikia hiyo cost ya kujenga ukuta ni kubwa ya kutosha kujenga madarasa ya kutosha wanafunzi wengi ambao leo hata madawati ya kukaa ni issue. Kweli kwa hali ya chuo kikuu ilivyo ukuta ni muhimu zaidi ya sehemu za kusomea? Wale wanafunzi wanasikiliza lecture kama wamepanda daladala za Mbagara posta inakuwaje?
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Na vile vyote vinavyozungushiwa ukuta duniani ni magereza?
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Issue ya mabweni ni suala la kuingia kwenye Ubia wa biashara na wawekezaji wa hapo ndani ya nchi tu

  Chuo kinatoa eneo, developer anajenga bweni, anakusanya hela yake kutoka kwa kodi, zikitimia bweni linageuka mali ya chuo.
   
 13. E

  Elias Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ujuwe nchi hii kila mmoja na ujanja wake wa kutafuta fedha... huyu jamaa na jopo lake wamefikiria jinsi ya kuboreha biashara zao wakaona hakuna njia nyingine...
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kwa mtindo huo ndio maana tumegawa bure karibu kila kitu kwa the so called wawekezaji, ambao leo tunaona fahari kutumia resources zetu ndogo kuzunguka dunia nzima kuwaita waje kuinvest.
  Kwani Hall 1 mpaka 7 alijenga nani? Au ndio tumeamua kuuza vichwa vyetu completely. Nchi hii kama sisi hatuoni sababu ya kuipenda nani atatuonea huruma akaipenda? Wawekezaji?
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuna ubaya gani kushirikiana na developer wa hapo ndani ya nchi (hata mwanzo nilizungumzia mwekezaji wa ndani) kama chuo hakina pesa za papo kwa papo na shida ya mabweni ni kubwa?

  Huo mfumo mbona ni moja unaoesemwa umepeleka maendeleo sana THAILAND?

  Tatizo si mwekezaji mkuu, tatizo ni mikataba tunayowekeana nayo. Walimu wa UDSM wana makampuni makubwa tu ya construction, kwa nini wasitumiwe kwama developer kisha mali ikageuka ya chuo.
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli hakuja haja ya ukuta kwa sasa kwasababu chuo kilikwishaanza siku nyingi ni bora kuimarisha miundombinu kwanza na mazingira ya kusomea then kama watakua na fungu la ziada likabaki ndipo wajenge ukuta kwasababu hatujasikia kamba wanafunzi wanatoroka chuo kwasababu hakuna ukuta au wanaibiwa mali zao kwasababu hakuna ukuta kwa sasa tatizo kubwa ni kwamba quality ya chuo inashuka kutokana na matatizo mbalimbali kikubwa ni waalimu,madarasa vitabu na vifaa vya maabara kamilisheni hayo kwanza!
   
 17. O

  Ome Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  mi sioni baya kuweka fence na sababu aliyoielezea ilikuwa ya msingi kabisa, mji unakua huu mwisho tutaona kuna makazi ya watu ndani ya chuo. ni vzuri na itasaidia kulinda mipaka yake. assume mabibo hostel isingekuwa na fence ingekuwaje?. Hata baadhi ya vyuo vya nje pia vina fence ili kuonyesha mpaka wa eneo lake na pia inamjuza mtu kuwa hapa sasa nipo katika himaya ya shule,chuo,hospt,magereza, kwa lymo, kwa fulani so what is wrong, na fence si lazima iwe ya ukuta mrefu kama wa kuzuia mwizi asiruke.
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kikwete kuichangishia fedha UDSM

  19th January 2011
  Rais Jakaya Kikwete , ameandaa hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), itakayofanyika Ikulu kesho.
  Ujenzi wa kituo hicho unalenga kupunguza msongamano wa wanafunzi wanapojisomea katika maktaba.
  Akizungumza na wanahabari jana, Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema Rais Kikwete atahamasisha uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho na miundombinu yake.
  Alisema wengine wanaotarajiwa kuchangia ujenzi huo, ni wahitimu wa zamani wa UDSM pamoja na wadau wa chuo hicho.
  "Ukiwa nje utawaona wanafunzi wengi wanasoma kwenye miti na nyasi kwa sababu kuna uhaba mkubwa wa maktaba ya kujisomea japokuwa kuna wengine wanapenda kukaa kwenye miti kwa ajili ya kupunga upepo," alisema Profesa Mukandala.
  Alisema kwa sasa wahadhiri na wafanyakazi wa chuo wameweza kuchanga na kupata Sh. bilioni 1.34 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho unaotarajiwa kugharimu Sh. bilioni 17.
  Profesa Mukandala alisema kukamilika kwa kituo hicho, kutachukua wastani wa wanafunzi 5,000.
  Kituo hicho kitakuwa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutolea huduma muhimu kwa wanafunzi, yakiwamo ya kusomea na kupumzika wakati wa mchana, kupata huduma za internet, posta na benki, ofisi za vyama na makundi mbalimbali ya wanafunzi na maktaba kwa ajili ya wanafunzi wa shahada za juu.
  Alisema UDSM ina mpango wa kujenga mabweni ya wanafunzi kwa awamu tatu, yatagharimu Sh. bilioni 18 na kwamba, watalipatia ufumbuzi tatizo la wanafunzi kupanga nje ya chuo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 19. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  basi wangesema wanaweka mipaka na mpaka sio ukuta tu mpaka unaweza kuwa hata kupanda miti
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kilimasera, mimi sitetei kujengwa ukuta kwa sasa wakati kuna matatizo mengi zaidi wangeweza kutatua

  Nilikuwa namjibu huyo aloshangaa idea ya chuo kikuu kuwekewa ukuta kama ni maajabu ya dunia wakati vyuo vikuu vikubwa dunia vimezingirwa kwa kuta.
   
Loading...