Uchaguzi 2020 Ukurasa wa Ikulu-Mawasiliano kupost habari za CCM ni sawa?

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,511
4,224
"Ikulu ni mahali patakatifu"

Ni moja ya kauli aliyopata kunena Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyekaa ikulu kwa takriban miaka 23 akimaanisha kuwa ikulu ni mahala pa Watanzania wote pasipo kuangalia vyama vyao,Dini ama Uzanzibari na Utanganyika wao.

Anayeishi ikulu anaiwakilisha Serikali ya Watanzania wote.

969715_566344646743906_519440834_n.jpg
 
Page za wana harakati kuwa kasuku wa CHADEMA ni sahihi, kila mtu ashinde mechi zake, achane kulialia, na wewe anzisha account Ikulu Ufipa post picha na habari za Lissu.

Lialia FC.
 
Page za wana harakati kuwa kasuku wa CDM ni sahihi, kila mtu ashinde mechi zake, achane kulialia, na wewe anzisha account Ikulu Ufipa post picha na habari za Lissu.
Lialia FC.
Hatuzungumzii habari za chama.Binafsi sina uchama kabisa na post hii imelenga matumizi ya ikulu ambapo ni makazi ya rais wa wananchi kutumika kwa maslahi ya chama ni sahihi?
 
Hatuzungumzii habari za chama.Binafsi sina uchama kabisa na post hii imelenga matumizi ya ikulu ambapo ni makazi ya rais wa wananchi kutumika kwa maslahi ya chama ni sahihi?

Yoyote anaweza anzisha account, ile account ya Ikulu mawasiliano utakuta imeanzishwa na Msigwa kumrahisishia kazi yake, si mali ya Ikulu, sio gari au nyumba ya Ikulu ile account, CHADEMA na wao waanzishe account Ikulu ufipa watume wanachotaka, account kuanzisha ni bure tunacho lialia hapa ni nini ?
 
Yoyote anaweza anzisha account, ile account ya Ikulu mawasiliano utakuta imeanzishwa na Msigwa kumrahisishia kazi yake, si mali ya Ikulu, sio gari au nyumba ya Ikulu ile account, CDM na wao waanzishe account Ikulu ufipa watume wanachotaka, account kuanzisha ni bure tunacho lialia hapa ni nini ?
Unaposema si Mali ya ikulu si sahihi kwa kuwa inatumia resources za ikulu na pia taarifa nyeti za Ikulu zilikuwa zinatolewa kupitia page hizo zilizoidhinishwa.
 
Unaposema si Mali ya ikulu si sahihi kwa kuwa inatumia resources za ikulu na pia taarifa nyeti za Ikulu zilikuwa zinatolewa kupitia page hizo zilizoidhinishwa.

Acc ya Msigwa na ya Magufuli pia ilikuwa inapost taarifa nyeti, je ni mali ya Ikulu? Vipi JK account zake zimebaki Ikulu pia?
CHADEMA na wao waanzishe acc yao waiite Ikulu Ufipa waweke taarifa zao, Ikulu ya Tz haina hati miliki ya social media acc yoyote, utawala ukibadilika Msigwa anaweza vizuri kabisa kuondoka na hiyo acc.
 
Ikulu mpaka sasa ni miliki ya ccm ,hakuna ubaya wowote
Nikirejea kesi maarufu ya Premji Vs Aman Kaboruu huko Kigoma miaka 1990s, kuhusu mipaka ya chama tawala kutumia rasilimali za serikali kwa kampeni, Msigwa na CCM wanakiuka sheria ya uchaguzi.

Sema ndio basi tena hata Muhimili wa mahakama kule Rufaa, kunaongozwa na Ngosha, kumemezwa hakufurukuti mbele ya maslahi ya CCM.
 
Acc ya msigwa na ya Magufuli pia ilikuwa inapost taarifa nyeti, je ni mali ya Ikulu ? Vipi JK account zake zimebaki Ikulu pia ?
CDM na wao waanzishe acc yao waiite Ikulu Ufipa waweke taarifa zao, Ikulu ya Tz haina hati miliki ya social media acc yoyote, utawala ukibadilika Msigwa anaweza vizuri kabisa kuondoka na hiyo acc.
Je,Ni sahihi watu binafsi kutumia majina ya taasisi nyeti za serikali na kuziidhinisha (Verified Accounts) hali ya kuwa zinatumika kwa matumizi na maslahi binafsi? Tutoke nje ya masuala ya uchama na tujaribu kudadavua usahihi wa haya.
 
"Ikulu ni mahali patakatifu"
Ni moja ya kauli aliyopata kunena Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyekaa ikulu kwa takriban miaka 23 akimaanisha kuwa ikulu ni mahala pa Watanzania wote pasipo kuangalia vyama vyao,Dini ama Uzanzibari na Utanganyika wao.Anayeishi ikulu anaiwakilisha Serikali ya watanzania wote.View attachment 1556258
Msigwa hajitambui, Kuna kila sababu afikishwe Tume ya Maadili
 
Mali za umma zimegeuzwa mali za CCM, hata magari wanayotumia kwenye kampeni ya serikali isipokuwa wanabadili plate no
 
Je,Ni sahihi watu binafsi kutumia majina ya taasisi nyeti za serikali na kuziidhinisha (Verified Accounts) hali ya kuwa zinatumika kwa matumizi na maslahi binafsi? Tutoke nje ya masuala ya uchama na tujaribu kudadavua usahihi wa haya.

Zinatumika kwa matumizi na maslah ya boss wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom