Uchaguzi 2020 Ukurasa wa Ikulu-Mawasiliano kupost habari za CCM ni sawa?

Wakati umefika wa kuunga kwa mkono yale yaliyosemwa na wazee wetu waliotangulia mbele za haki. Turejee sifa za mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi kwa CCM kama vile ambavyo zilivyotolewa na marehemu Kingunge Ngombale Mwiru.

Pasipo kumung'unya maneno alitamka hadharani sifa za bwana huyu, kutamka kuwa anafaa ktk majukumu yake "special" na wala sio kwa nafasi nyeti ya uraisi. Tunashuhudia ukweli huu kupitia kampeni zake, mara ununuzi zaidi wa ndege, mara ujenzi wa meli, mara ahadi zile za ujenzi wa miundombinu.

Hayo yote ndiyo matumizi ya kila siku ya maduhuli na kodi za wananchi kwa Rais yule duniani. Watu wanataka kusikia Sera mpya za kuwainua zaidi kimaisha wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wavuvi, wazee, wastaafu, wanafunzi na makundi mengine muhimu ktk sekta zao husika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom