Ukumbusho: Kodi mbalimbali za kulipa

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Feb 25, 2018
420
939
Habari zenu

Kuelekea mwisho wa mwaka jitahidi kodi za ndani mbalimbali za kila mwezi na za kila robo ya mwaka kuwa umelipa au umewasilisha kwa wakati. Kodi hizo ni

1. Kodi za kila mwezi zitokanazo na ajira ambazo ni PAYE na SDL kumbuka kuwasilisha ndani ya muda
2. Uwasilishaji wa ritani za ongezeko la thamani ie VAT kabla au siku ya mwisho ya kila mwezi ie 20
3. Kodi ya makadirio uliojikadiria kwa kampuni/kukadiriwa kwa mtu binafsi
4. Ziandae vema risiti na vielelezo mbalimbali vilivyotumika katika miamala ya kibiashara kwani kuna kuandaa hesabu za mizania kwa wenye sifa na vigezo

Muhimu zaidi kumbuka kujisajili online kwa uwasilishaji wa ritani za kodi mbali mbali

Pia usisahau kulipa 'annual returns BRELA' kwa kampumi na 'maintanance fee' kwa jina la biashara ndani ya wakati

Kwa changamoto za ushauri katika biashara|masuala ya kodi| uhasibu| ukaguzi karibu tujadili

Hotline: 0777777766 |0659211222
Email: info@cityaccountax.co.tz
20201103_023323.jpg
 
Mfano mtu umesajili kampuni BRELA lakini bado haijaanza Operations, baada ya miezi kadhaa ukaenda TRA kufatilia Tax Clearance ili ufatilie leseni, Je hizo SDL na Withhold taxes watazidai before Tax clearance au utaanza kuhesabiwa baada ya kukabidhiwa Clearance certificate??
Taratibu zake ni hizi
1. Baada ya kusajili kampuni BRELA
Ukikamilisha hatua hii inatakiwa uende TRA kuomba TIN ya kampuni. Hapa kampuni itajikadiria kodi kulipa kwa mwaka huo wa kodi. Lakini kwa kuwa umesema haitafanya biashara kwa wakati huo, kampuni itajaza makadirio sifuri na kutoa taarifa ya kutoanza kufanya biashara/huduma.

Sasa kampuni itakapotaka kuanza kufanya biashara/huduma itatakiwa kujaza tena fomu ya makadirio ya awamu ya pili kuonyesha makadirio ya awali yasitumike tena ie review provision tax estimates

2. Kuomba cheti cha Tax Clearance
Baada ya kulipa kodi nyinginezo kama kodi ya zuio, ushuru wa stempu na ikibidi makadirio ya awali ya kodi utaomba cheti cha Tax Clearance

3. Ulipaji SDL na PAYE
Katika uwasilishaji wako wa taarifa za kuomba TIN ya kampuni kuna sehemu ya kujaza idadi ya wafanyakazi. Kwa taarifa hizo ndiyo utaanza kulipa kodi hz. Kama una wafanyakazi /zaidi ya 4 utawajibika kulipa SDL.

Na kama mishahara kuanzia 270+ utalipa PAYE pia (hii haijalishi idadi bali kiwango). Kwa mantiki hii si kila kampn lazima ilipe hz kodi kwn kuna baadhi bd changa sana na hazina wafanyakazi zaidi ya wamiliki/wanahisa wenyewe
 
Back
Top Bottom