Ukumbi wa St. Peters Oysterbay(Rugambwa Hall) hauna Management. Ni Aibu Kubwa Kwa Kanisa

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,663
2,000
Mimi ni msimamizi wa kamati ya mapambo tumekodi huu ukumbi wa Rugambwa Hall ambao ni ghali sanaa unaomilikiwa na kanisa katoliki.

Kwa kujua ukumbi ni wa kanisa letu takatifu katoliki tulitegemea certain level of professionalism and clientele. Ukijumlisha na bei yake tukajua sio ubabaishaji.

Chakusikitsha kufika hapa leo mapemaaa msimamizi kalewa Chakusikitsha hana Lugha, hana nini sio Management kabisaa kudeal na meneja cha pombe ukumbi wa kanisa.

Hela wanatoza flat rate na ukilipia ukumbi unatakiwa upewe viti na meza bbila kujali idadi ya watu waliopo maana unalipia ukumbi hivo vingine ni bure.

Sasa wametoa meza chache, kuomba kuongezea meneja analazimisha mazingira ya rusha kwamba si haki Ila tuongee nae pembeni. Jamani mpaka kanisani? Na hela yote ya ukumbi tulioToa?

Anasema nenda Kokote huu ukumbi haupo management ya kanisa una management yake na Maneno kibao ya shombo. Sio kama utegemeavo ukumbi wa kanisa ghali kama huu.

Mimi najua paroko St Peters Hajui Wala Kadinali. Ingekuwa mali ya mtu binafsi ningenyamaza Ila mali ya kanisa imebidi niongee mameneja Rugambwa Hall hakuna Kuna ubabaishaji tu. Zisipochukuliwa hatua siku si nyingi hii investment inabaki story.

Naomba Hili swala litizamwe kwa kina.
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,727
2,000
Huu sasa unafki, kwanini usilifikishe kunakohusika au unataka kuwaharibia wenzio
 

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,663
2,000
Hapa ni mahali sahihi kuhakikisha taarifa zinafika haraka. Mimi simsingizii mtu ndo maana nimeongea hadharani Tatizo litafutiwe ufumbuzi. Mficha miradhi...............
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,702
2,000
Dah tukisema tulete Mada za hivi si tutakuwa tunajaza serve hapa.. Changamoto kama hizi ZIPO na kumbuka ule sio ukumbi WA serikali HiVyO wanajiendesha wenyewe... Nadhani kama una maoni ungefanya vizuri kuyafikisha kwenye uongozi Wao
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,841
2,000
Sidhani kama umelileta mahali sahihi. Kama we ni muumini peleka taarifa kwa uongozi wa kanisa!
Kuna kosa gani kuleta katika ukumbi huu!. To somebody's convenience. Believe it or not, watu wengi , waelewa wanasoma JF, therefore for quick dissemination , this is the right audience.
Kama Nchemba alijibu tuhuma dhidi yake kuhusu Ben, this is a clear indication that his fellow government heads are also reading this. And any intelligible person should take JF as a source of information to work on!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,655
2,000
Ni kweli hili sio jukwaa sahihi lakini malalamiko yanaweza kuwa sahihi. Mimi nadhani hao Roman sio ukumbi ndio bei juu hata shule zao ada ni juu sana. Nilitaraji kama kanisa wangekuwa na ada nafuu kwani mapato yao yanatokana na sadaka zetu waumini. Lakini bei zao hata huduma za mashetani zisingekuwa hizo.
 

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,497
2,000
Leo mdogo wangu lala1 umekamatika.umeingia cha kiume mpaka umepaza sauti huku.nilijua umeleta ubuyu wa Malovie Dovie
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,756
2,000
Ukitaka risiti ya EFD ukumbi wa Rugambwa ni 3M, bila ya Risiti ni 2.5 M , Yule Meneja ni Mishe Mishe sana na sometime anakuomba kadi ya Mwaliko aje Afakamie Pombe za Bure
 

gambanjeli

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
393
250
Dah tukisema tulete Mada za hivi si tutakuwa tunajaza serve hapa.. Changamoto kama hizi ZIPO na kumbuka ule sio ukumbi WA serikali HiVyO wanajiendesha wenyewe... Nadhani kama una maoni ungefanya vizuri kuyafikisha kwenye uongozi Wao
Mada hii haina vigezo vya kuwekwa kwenye jukwaa la siasa. Hakuna siasa ndani yake bali matatizo ya kibiashara. Je mtoa mada amewasiliana hoja zake ngazi za juu zinazomiliki ukumbi au kusudi lake ni kuchonganisha Jamii Forum na uongozi wa kanisa la Mtakatifu Petro la Oyesterbay?
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,566
2,000
Kanisa linasheherekea Jesus birthday, wewe unaenda kutafuta ukumbi wao kwa mambo yako, wapi na wapi? Meneja kalewa kwa sababu ni X-mas. Kwanza ukumbi ulitakiwa kuwa umefungwa siku kama hiyo maana watumishi wote wa kanisa pamoja na huyo meneja wanakuwa mapumziko ya X-mas ambayo yanawaruhusu kupiga kilevi kidogo. Hivyo shukuru angalau ulipata hiyo huduma kiduchu kutoka kwa huyo meneja.

Masuala ya namna hii siku nyingine uwe unayapeleka kule kwenye jukwaa la habari mchanganyiko. Hapa ulipoleta ni kwenye jukwaa la malumbano kati ya wana Lumumba na wana Ufipa. Unawaharibia malumbano yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom