St. Peters Oysterbay Liangalieni hili

St. Peters Oysterbay Liangalieni hili

ngonyango

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2017
Posts
1,887
Reaction score
1,623
Mimi kama muumini wa kanisa katoliki ningependa kutoa maoni yafuatayo kuhusu kanisa la St. Peters Oysterbay ukilinganisha na lile la Katoliki Mwananyamala (haya ndiyo ninauzoefu nayo)katika kurahisisha huduma kwa waumini.Kuna mambo mawili ambayo huwa yananikera na ambayo najua yapo ndani ya uwezo wa wahusika;

1. Upatikanaji wa viti pale nje ya kanisa kwa wale wanaochelewa, utaratibu wa Mwananyamala ni mzuri sana ..yaani unakuta viti vingi vimeshapangwa nje kuzunguka kanisa.Hata ukichelewa kiasi gani, utakuta kuna viti vimepangwa.Hii ni tofauti na St Peters, viti huwa vipo vimerundikwa makundi makundi,mtu akichelewa inabidi awasumbue wengine ili akachukue kiti kimoja tu.

Huwa najiuliza,sasa inamaana wahusika hawalioni hili ? kwa nini wasipange viti viingi pale nje waumini waje kukaa tu? tena wakati mwingine hata hivyo vilivyorundikwa unaweza usivikute mpaka uende kule Rugambwa Hall madarasani...

2.Upatikanaji wa Maji ya baraka- utaratibu wa Mwananyamala ni kwamba kuna sehemu mbalimbali kule nje ambapo haya maji yamewekwa hivyo siyo lazima uingie ndani hivyo kama ulikuwa nje basi unamaliza mambo yako nje na kuondoka. Sasa pale St Peters , maji ya baraka yapo sehemu zilezile ambako miaka iliyopita ilikuwa ni sawa sababu labda waumini walikuwa wachache yamewekwa ndani ya kanisa tu. Sasa Misa ikiisha ni vurugu kati ya waliomaliza Misa wanahitaji kutoka na wanaoingia Misa inayofuata au walikuwa wanasalia nje nao wanahitaji kuchovya maji ili waondoke...wanakutana na wale waliokuwa ndani nao wanatoka nje ni chaos, chaos isiyo na sababu kwa kweli.

Tunaomba wahusika walifanyie kazi suala hili ambalo halihitaji gharama kubwa katika kulitekeleza
 
Umeogopa nini kufika ofisini na kuwaambia haya!!!
Kama muumini na mchelewaji jitolee tu kuwa unakusanya viti vyote mwishoni na wanaopanga hao fikiria watakuwa wa kulipwa au kujitolea ili wachelewaji mfike mkae tu..
 
Kazi ya sadaka n'nini? Mtu anatoka nyumbani anakuletea hela ofisini kwako unasindwa kumuandalia sehemu ya kukaa! That's very rude.
 
Kwani kazi ya sadaka ni kukupangia viti wewe unayechelewa? Usikute sadaka yenyewe unatoa jero, ofisi za kanisa hazipo kufikisha malalamiko yako?
Mbona unakuwa kivuruge ndugu
 
Sasa wewe kama unamuogopa Paroko, si ukaonane hata na katekista umueleze hizi changamoto? Nenda hata kwa viongozi wa baraza la walei utoe maoni haya mazuri kanisa lenu liboreshe...huu ndo tunauita uumini wa manati!!
 
Kazi ya sadaka n'nini? Mtu anatoka nyumbani anakuletea hela ofisini kwako unasindwa kumuandalia sehemu ya kukaa! That's very rude.

Sadaka ni majitoleo yako kwa Mungu. Sadaka inaambatana na maombi yako kwa Mungu aidha ya shukrani kwa mambo aliyokutendea au kwa mahitaji mbalimbali. Ndo maana kanisani tuna kipindi cha sadaka na kuna kipindi cha michango kama ujenzi wa kanisa nk.
 
Hapa jukwaani ... waumini watoe maoni yao wale wa mwananyamala na huko kwa pita
Halaf wakitoa Maoni yao hapa jukwaani ndo watakuwa wamefikisha kwa wahusika?
 
Hiyo kero ipo ndani ya uwezo wako amka saa11,kawahi kupanga viti,ukiafanya mara mbili tu,utaungwa mkono na wengi
 
Sio kivuruge umesshindwa kupeleka malalamiko yako Kwa unaowapa sadaka kama kweli una uchungu na sadaka yako una uhakika hao unawao waambia wamo humu, kuna mambo mengine unayamaliza huko huko sasa isiwe kila kitu kinaletwa mitandaoni
Kweli JF the place we dare to talk openly
 
Kwani kazi ya sadaka ni kukupangia viti wewe unayechelewa? Usikute sadaka yenyewe unatoa jero, ofisi za kanisa hazipo kufikisha malalamiko yako?
Hata tukiwahi wote haimaanishi kuwa tutaenea ndani kanisa ni dogo waumini wameongezeka. Ni wajibu wa uongozi wa kanisa kufikiria jinsi ya kuaccomodate wateja wao
 
Sasa wewe kama unamuogopa Paroko, si ukaonane hata na katekista umueleze hizi changamoto? Nenda hata kwa viongozi wa baraza la walei utoe maoni haya mazuri kanisa lenu liboreshe...huu ndo tunauita uumini wa manati!!

Hapa tunachangiana mawazo kwa upana wake..labda kuna sababu....lakini mbona Mwananyamala inawezekana?
 
Back
Top Bottom