Ukomunisti, Ujamaa ubunifu wa Karl Marx au Mipango ya Watu?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Kwenye historia ya uchumi anatajwa mjerumani mwenye Asili ya kiyahudi Karl Marx ndio inasemekana ndio Muasisi wa hii kitu.

Kwa Mujibu wa kitambo kimoja The History of Modern Economics Great thinkers wameelezewa watu nguli wote wa uchumi akiwemo Karl Marx. Cha ajabu hoja ya huyu jamaa ilionekana kama ni vyongo na haiwezekani unalinganisha hoja ya Adam Smith mchumi mwingeleza.

Maswali ni kwa nini na Nani yuko nyuma ya kutapakaa kwa communism na usocialism duniani?

Inasemekana hata hiyo communism manifesto inayosemekana aliitunga library moja maarufu huko uingereza alipewa hakuiandika yeye?

Kuna source nyingine zinasema Karl alipewa hiyo tenda ya kuandaa communist manifesto na kikundi cha watu kiitwacho 'The League of Just Men'. Ni wakina Nani hawa na kwa malengo gani?
 
Labda nijaribu kukujibu ninavyojua ujamaa ulianza kama ideas ya watu yaani utopian basi watu baadhi kama Robert Owen, Adam Smith na St Simon wakaanza kuimplement hasa kwa wafanyakazi, muda ukapita hasa kipindi cha mapinduzi ya viwanda kina Karl Marx na Frederick Engels wakafanya publication kama kitabu kiitwacho communist manifest ambacho kilipelekea kutokea kwa wafuasi wengine kama Vladimir Ilyich Lenin mpaka Bolshevik revolution, kwa swali lako nathani walitaka kiteneneza mfumo utakao jitenga na ubepari hasa unyonyaji
 
Ukiangalia vizuri Karl Marx alianza kuuchambua Ubepari way back karne ya 16 na ye alianzia mbali zaidi kwe Agrarian Capitalism akaja mpaka kwe Industrial Capitalism na Workers movements zitokanazo na Industrial Capitalism lakini Adam Smith kachambua zaidi Industrial Capitalism na faida zake kwe maendeleo ya jamii kwa ujumla,kwa hiyo si sawa kuwalinganisha watu hawa wawili

Lakini Ujamaa na Ukomunisti uliasisiwa karne ya 18 na Karl Marx na Fredrick Angel wakielezea uzuri wa kuweka uchumi kwa serikali na watu kwa ujumla kuwa una manufaa zaidi kuliko kuegemeza kwa mtu binafsi na makampuni maana waliona kuwa kuegemeza kwa mtu binafsi kunakuwa na unyonyaji,unyanyasi na ukandamizaji uliokithiri hasa katika uchumi wa viwanda
Kwa hiyo kuwalinganisha hawa watu wawili inakuwa si sawa maana wanaendana kwa kiasi kidogo sana ila kiasi kikubwa hawaendani maana walikuwa na mitazamo miwili ambayo ni kama paka na panya

Niko tayari kukosolewa naweza kuwa siko sawa!!
 
Back
Top Bottom