asiyetabirika
Member
- Oct 14, 2019
- 46
- 56
Kwa wajuvi wa haya masuala ya ki-ndoa, hivi tokea siku ilipopelekwa barua ya posa kwa wazazi wa binti huwa inatakiwa kuchukua muda gani hadi kuja kutoa mali?
Hapa namaanisha ukomo wa kuishi uchumbani baada ya kujitambulisha na kutoa barua ya posa ambayo kimsingi kijana utakuwa umeshatangaza nia ya kuchukua jiko.
Msingi wa thread hii ni kutaka kujua hasa hawa vijana wanaokuja kutoa barua kwa binti zetu halafu wanasema wanaenda kutafuta mahari ili warudi kuchukua jiko, lakini wazazi tunabaki kusubiri tu muda ukiwa unaenda hadi zaidi ya miezi mitano kijana akiwa haonekani ila akiulizwa ujio wake anasema bado anatafuta.