Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 4,930
- 12,474
Mkuu LC series 70 ni heavy duty sasa air suspension sio muhimu. Wao wameweka coil spring mbele na leaf spring nyuma sababu gari itafanya kazi nzito na mazingira magumu.Nazungumzia body kwa ujumla, yaani mimi sizungumzii engine wala gearbox. Gari ya milioni 200 inatumia shocks za spring wakati mwenzako anatumia air suspension tena ride ina comfort!
Hizo Armoured vehicles ni special purpose vehicles, huwa hazitumiwi kama vigezo kabisa vya kufananisha na gari za kawaida.
Hiyo air suspension nenda nayo kwenye njia korofi hata hiyo comfort ride hutoisikia zaidi ya gari kuhamahama.
Mfano ukichukua Lc pick up na L/Rover Defender pick up yenye coil spring mbele na nyuma ukazipa mzigo tani 1 kisha uingie njia mbaya mwisho wa safari mwenye L/Rover lazima ucheki bush na kuna uwezekano wa kukatika spring.