solution ni kama ifuatavyo ( zingatia).
1. KATIBA: tuungane pamoja kuhakikisha kuwa katiba mpya inatungwa, siyo kuweka viraka kwenye hii katiba ya serikali ya CCM, kwa mfumo wa katiba tuliyo nayo hatuwezi kuitoa CCM madarakani, kwa maana ni katiba ya mfumo wa chama kimoja. kutokana na mabadiliko ya katiba, tuunde chama shirikishi cha upinzani, kwa vyama vyenye mfanano wa kisera, bila kuuwa vyama husika, kwa pamoja wakubaliane kuunda serikali shirikishi na kuweka mgawanyo sawia wa kiutawala i.e (Rais, makamu, waziri mkuu) hawa watatu watakuwa kutoka katika viongozi wakuu wa vyama vishiriki, mgawanyo mwingine utapangwa kutokana na idadi ya viti ambavyo chama kimepata katika bunge.
2. (2015) Japokuwa unapaona ni mbali, lakini si kihivyo, tujipange.
Kila mwananchi ahakikishe kuwa anakitambulisho cha kupigia kura, ajue kituo chake cha kupigia kura ni wapi.
3. Pawepo na uhakiki na maboresho ya Daftari la wapiga kura mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ( kutakuwa na wapiga kura wapya zaidi ya milion 15 hadi ifikapo mwaka 2014 ambao unatakiwa kuwa ni wa ku update daftari la wapiga kura, kumbuka kuwa wote hao ni vijana wanao taka mabadiliko. Lazima tuhakikishe wanahusika katika kupiga kura,
4. Wananchuo. Kura nyingi za vijana ambao wako vyuoni zilpotea kwa kuwa wengi hawakupewa fursa ya kupiga kura katika vituo katika vyuo vyao. Paandaliwe mpango ambao utaweza kuwaruhusu wanachuo kama wakati wa kupiga kura watakuwa bado chuini, waweze kupiga kura katika vyuo vyao.
5. Watanzania waishio nje ya nchi, wapewe fursa ya kupiga kura. uandaliwe mfumo rahisi na wa uwazi ambao hautaweka mashaka ya kuletwa kutoka nje kura feki.
6. Tume ya uchaguzi iwe huru isiyolinda masilahi ya chama fulani.