Ukombozi wa Tanganyika utatoka Arusha,Mwanza.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukombozi wa Tanganyika utatoka Arusha,Mwanza....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rweye, Nov 4, 2011.

 1. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Ukiitizama Tanzania ya leo na ukawatizama watanganyika wa leo katika kudai upya na kupigania uhuru wao kwa mara ya pili hakika utaona kama ni Tripoli basi ni Arusha,kama ni Alexandria basi ni Mbeya,kama ni Tunis basi ni Mwanza,kama ni Benghazi basi ni Kagera na kama ni Cairo basi ni Shinyanga

  Sijaitaja Dar Kwa makusudi kabisa kwani mbali ya kuwa mji muhimu kibiashara hauna vitu (rasirimali) kama ilivyo miji hapo juu,hii miji ndo mahali ambapo harakati zinatakiwa kuanzia kutokana na ukweli kwamba zaidi ya 60% ya mapato ya nchi yanatoka kanda ya ziwa na kwa kusini ni Mbeya,kwa vile maeneo haya yana mchango mkubwa katika kuendeleza nchi yetu na bado maendeleo yao ni mabovu kwa vyovyote vile mikoa hii inanyonywa na watu wanabaki maskini

  Ndugu zetu amkeni mtuongoze kwenye harakati maana resources nyingi mnazo nyinyi ikiwa ni pamoja na watu,sitegemei miji km Moro,Sing,Dom,Tabo,Pwani na Tanga wanaweza kuamka ikiwa wao hawana kinachowapa uchungu,hawana madini,hawana kilimo wala mambo makubwa eti waamke kabla nyinyi kuamka na hata rasirimali watu (wasomi) miji tajwa hapo juu mna hazina kubwa ya wasomi na hakika tunaamini mko mbali kielimu,tunaomba muwe taa zetu ili vuguvugu hili lifike kila kona ya Tanganyika

  Naililia Tanganyika inayotimiza miaka 50 ya uhuru wa bendera huku yenyewe ikiwa imetiwa minyororo jela
   
 2. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Kwani hao uliowataja walianza kwa kulalamika au walingia kazini moja kwa moja? wabongo mkiona washa washa tu , mbio

  haina haja ya kufanya kama ya hao ulio wataja,
   
 3. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  solution ni kama ifuatavyo ( zingatia).

  1. KATIBA: tuungane pamoja kuhakikisha kuwa katiba mpya inatungwa, siyo kuweka viraka kwenye hii katiba ya serikali ya CCM, kwa mfumo wa katiba tuliyo nayo hatuwezi kuitoa CCM madarakani, kwa maana ni katiba ya mfumo wa chama kimoja. kutokana na mabadiliko ya katiba, tuunde chama shirikishi cha upinzani, kwa vyama vyenye mfanano wa kisera, bila kuuwa vyama husika, kwa pamoja wakubaliane kuunda serikali shirikishi na kuweka mgawanyo sawia wa kiutawala i.e (Rais, makamu, waziri mkuu) hawa watatu watakuwa kutoka katika viongozi wakuu wa vyama vishiriki, mgawanyo mwingine utapangwa kutokana na idadi ya viti ambavyo chama kimepata katika bunge.

  2. (2015) Japokuwa unapaona ni mbali, lakini si kihivyo, tujipange.
  Kila mwananchi ahakikishe kuwa anakitambulisho cha kupigia kura, ajue kituo chake cha kupigia kura ni wapi.

  3. Pawepo na uhakiki na maboresho ya Daftari la wapiga kura mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ( kutakuwa na wapiga kura wapya zaidi ya milion 15 hadi ifikapo mwaka 2014 ambao unatakiwa kuwa ni wa ku update daftari la wapiga kura, kumbuka kuwa wote hao ni vijana wanao taka mabadiliko. Lazima tuhakikishe wanahusika katika kupiga kura,

  4. Wananchuo. Kura nyingi za vijana ambao wako vyuoni zilpotea kwa kuwa wengi hawakupewa fursa ya kupiga kura katika vituo katika vyuo vyao. Paandaliwe mpango ambao utaweza kuwaruhusu wanachuo kama wakati wa kupiga kura watakuwa bado chuini, waweze kupiga kura katika vyuo vyao.

  5. Watanzania waishio nje ya nchi, wapewe fursa ya kupiga kura. uandaliwe mfumo rahisi na wa uwazi ambao hautaweka mashaka ya kuletwa kutoka nje kura feki.

  6. Tume ya uchaguzi iwe huru isiyolinda masilahi ya chama fulani.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Kuna principle moja ya fizikia inasema material yoyote inayopata jota taratibu pia hupoteza joto hilo taratibu!! Ukiona jamii yoyote inayoonewa kukandamizwa na kunyonywa kwa muda mrefu ikawa kimya tu usiwachukulie ni waoga huwa wanatoa chance kwa opponents wao wajirudi ila siku wakisema basi it is enough inawachukua muda mrefu sana kutulia . Watch out!!!
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hoja inaungwa Mkono!
  Arusha ndiyo Benghazi ya Tanzania
   
 6. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,540
  Likes Received: 1,535
  Trophy Points: 280
  Napita, ntarudi!
   
 7. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  may be!
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hata kama approach yetu itakuwa ni tofauti na ya wenzetu kask naamini twendako ni kulekule na hatimaye saa6 itatimia na yote yatakwisha
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kwani chadema wao wanafanya nini kwa sasa hivi?mbona hatuwasikii au wameridhika hapo walipofika?
   
Loading...