Uko wapi uzalendo wa viongozi wa kanda ya kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uko wapi uzalendo wa viongozi wa kanda ya kusini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilago, Feb 18, 2012.

 1. k

  kilago New Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kanda ya Kusini imependelewa kwa kuwa na Wabunge ambao wengi wao ni Mawaziri ambapo kwa Mkoa wa Mtwara: Mtwara Vijijini Mbunge wake ni Mh: Hawa Ghasia ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Newala Mbunge wake ni Mh: Capt Mstaafu George Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kwa Mkoa wa Lindi kuna jimbo la Mtama ambalo mbunge wake ni Mh: Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa; Ruangwa Mbunge wake ni Kassim Majaliwa ambaye ni Naibu Waziri TAMISEMI; Nachingwea mbunge wake ni Mathias Chikawe ambaye ni Waziri Ofisi ya Raisi Utawala Bora.


  Kwa nini viongozi hawa si wazalendo; Uchumi wa wananchi wa kanda ya Kusini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara unategemea sana zao la korosho ambalo kwa mwaka wa uchaguzi wa mwaka 2010 bei ya korosho ilifika mpaka shilingi 2300/=kwa kilo moja ambapo mfumo wa stakabadhi ghalani unatumika ambapo malipo yaweza kufanyika mara tatu; Msimu wa mwaka 2010 wakulima wapata malipo ya kwanza sh.850/= malipo ya pili sh.350/= na malipo ya tatu ambayo ni ya majaliwa mpaka sh.850/= makato mengine ni ya ushuru wa halmashauri, vyama vikuu, usafirishaji, ushaufu.

  Msimu wa mwaka jana wakulima walivutiwa sana na soko la mwaka 2010 na kuzalisha kwa wingi sana korosho lakini mpaka sasa kuna mwingiliano wa viongozi wakubwa kwa mkoa wa Mtwara na Lindi kiasi kwamba mpaka sasa wakulima hawajapata kabisa malipo ya kwanza ya sh.850/=. Mpaka sasa si wabunge wala madiwani wa Chama cha Mapinduzi ambao wamethubutu kuwaeleza wananchi tatizo liko wapi, kitu ambacho kimepelekea wananchi kukata tamaa ya maisha maana pesa zilitumika ktk kuandaa mashamba ya korosho, kiasi kwamba sasa imekuwa ngumu hata kulipia ada watoto wa shule. Mbaya zaidi Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho ni Mh: Mama Anna Abdallah ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nagaga Wilaya ya Masasi. Kuna haja ya wananchi kubadili viongozi kwa chaguzi zijazo ili wananchi wapate viongozi watakaowatumikia. Naomba michango yenu wana JF
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama ilo jopo lingekuwa latoka kanda fulani apa ungeona mabadiliko faster
   
 3. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wewe unapenda kila waziri apendelee kwenye jimbo lake? Waziri anaongoza wizara. Wizara haina jimbo moja. Ni nchi nzima inategemea wizara hiyo moja. Badala ya kuwalaumu viongozi hao hapo juu, ulitakiwa uwapongeze kwa kutokuwa na upendeleo.
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Alitaka wafanye kama anavyofanya mkweree kila kitu Bagamoyo!!
   
 5. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Najiandaa kugombea Jimbo la Mtama au Mtwara vijijini!!!mnipe sapoti tubadilishe kusin yetu,tuwaweke pemben wazee wote
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hoja yako ni nzuri kiongozi,
  Si lazima watumie raslimali za wizara zao kujinufaisha, lakini wanaweza kuwekeza huko majimboni kwao,
  Maana utaona watu kama hao zaidi ya nyumba yake ya kuishi hana uwekezaji wowote labda kashamba ka kuzugia wakati anaomba kura!
   
 7. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Najaa.
   
 8. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio asili yetu watu wa kusini hatuna umoja,uzalendo wala kubebana.tofauti na watu wa maeneo mengine.wakusini akipata hana muda tena na watu wake wala jamaa zake.
   
Loading...