Vyama vinavyounda UKAWA vimetangaza kufanya maandamano yenye lengo la kupinga udikteta, UKUTA. Maana yake ni Kwamba serikali ya Rais Magufuli in ya kidikteta.
Niwakumbushe UKAWA yafuatayo:
1. Serikali ya Rais Magufuli imechaguliwa na watanzania kikatiba katika Uchaguzi mkuu 2015.
2. Kulingana na katiba, Rais hushauliwa na Baraza la mawaziri. Na pia Rais hushauriwa na Chama chake. Hivyo, Rais Magufuli anafanya maamuzi Kwa kushauriwa na taasisi hizi. Hivyo madai Kwamba anaamua bila kushauriwa hayana mashiko.
3. Madai Kwamba anawagandamiza baadhi ya watanzania, ni jambo la kushangaza. Tukumbuke wakati WA sakata la EPA, Chadema walipiga kelele sana wakati JK alipowaomba wezi WA fedha za EPA wazirudishe. Wakasema anaongea na wezi. Rais Magufuli amechukua msimamo tofauti, amekuwa dhabiti. Sasa Chadema wanadai dikteta. Hapana.
4. Rais Magufuli amekuwa na msimamo Mkali dhidi ya Ufisadi, wakwepa kodi, ubadhirifu kwenye serikali na halmadhauri na mashirika ya umma. Anapigania utajiri WA Nchi Yetu uwanufaishe watanzania wote. Ukweli Rais Magufuli ni Jibu Kwa maombi ya watanzania wengi kutokana na hali ilivyokuwa imefika.
4. Upinzani wanachokifanya ni kutaka kuwapotodha watanzania ili waichukie serikali yao. Upotodhaji lengo ni uchochezi.
Ukowapi udikteta wa Rais Magufuli? Lakini uchochezi wa UKAWA in dhahiri. UKAWA wanadai demokrasia inaminywa. Tukumbuke, mgombea UKAWA alivyopatikana. Ilikuwa ndani ya chopa na watu wachache siyo kwenye vikao. Hapakuwa na mchakato ulio wazi. Iko wapi demokrasia kwenye UKAWA?
Pia tukumbuke, walimtuhumu Lowassa Kwa muda mrefu kuwa ni fisadi na wakawaeleza watanzania kuwa wanao ushahidi. Ghafla wakaamua awe mgombea urais. Uko wapi Uzalendo WA kweli ndani ya UKAWA?
Watanzania tumuunge Mkono Rais Magufuli.
Hii nchi inavituko sana, huyu
fred mpendazoe alikuwa mbunge aliyekuwa na nafasi ya karibu kabisa ya kuwa waziri wa wizara fulani na hii ndiyo akili aliyokuwa nayo kuongea mambo kama mjinga.
Mtu mjinga si kwamba hana akili ila akili yake haijachangamshwa kuweza kufikia kiwango cha kufikiri kwa ufasaha na kutoa/kufanya maamuzi sahihi.
“better to write for yourself and have no public, than to write for the public and have no self." c. Connolly
“a people that values its privileges above its principles soon loses both.” d. Eisenhower
“people can't live with change if there's not a changeless core inside them.” s. Covey
"Wenye werevu huwa ni watu wenye mipango na wenye busara huwa ni watu wenye misimamo"
Lakini nathubutu kusema wewe bwana mkubwa
fred mpendazoe umekosa vyote, huna werevu wala busara.
Kukutoa shaka mimi si mwanasiasa na sina chama huwa napiga kura kutumia misimamo yangu.
Ila kwa kufatilia maandiko yako mengi nimeona kuwa wewe ni kati ya wale watu wasiojua nini wanataka wapo wapo tu na wanaongozwa na njaa au mahitaji ya tumbo lao.
"In matters of style, swim with the current; in matters of principle, stand like a rock." t. Jefferson
Watu wenye misimamo huwa hawajumbishwi na matukio au vitu. Huwa wanasimama kwenye misimamo ya hata kama wako peke yao sababu wanaamini kwenye wanachokisimamia lakini siyo wewe bwana mkubwa
fred mpendazoe .
Kwa msaada wako nenda kajaribu kilimo nchi hii inamapori mengi tu huko yanahitaji wakulima huna sifa za kuwa kiongozi, huwezi kuwa kiongozi bora kama umejaa unafiki.