"Fred Mpendazoe, post: 17295947, member: 382107"]
1. Serikali ya Rais Magufuli imechaguliwa na watanzania kikatiba katika Uchaguzi mkuu 2015.
Mpendazoe nani amekuambia uchaguzi unaondoa haiba ya udikteta duniani?
Kuna nchi ngapi zinafanya uchaguzi chini ya madikteta.
Hoja hapa ni kuwa,uchaguzi ni hatua moja, kusimamia sheria za nchi ni hatua nyingine.
Ni sawa na mzazi anayejifungua mtoto. Uzazi haumaanishi mzazi huyo mwema lazima atatoa mtoto mwema. Umeelewa! Uchaguzi una lengo la kupata viongozii! hauelezi Zaidi
2. Kulingana na katiba, Rais hushauliwa na Baraza la mawaziri. Na pia Raishushauriwa na Chama chake. Hivyo, Rais Magufuli anafanya maamuzi Kwa kushauriwa na taasisi hizi. Hivyo madai Kwamba anaamua bila kushauriwa hayana mashiko.
Hivyo ana dhima ya kukubali kila ushauri?
Kwa Mpendazoe hata kama ingalitokea kipande cha nchi kikauzwa, midhali kuna ushauri basi mamlaka zifuate tu.
Rais anashauriwa, dhima ya kupima ushauri na matokeo ya ushauri huwa mikononi mwake. Rais alipoapa kwa katiba, hakushirikisha CCM au baraza
3. Madai Kwamba anawagandamiza baadhi ya watanzania, ni jambo la kushangaza. Tukumbuke wakati WA sakata la EPA, Chadema walipiga kelele sana wakati JK alipowaomba wezi WA fedha za EPA wazirudishe. Wakasema anaongea na wezi. Rais Magufuli amechukua msimamo tofauti, amekuwa dhabiti. Sasa Chadema wanadai dikteta. Hapana.
Hapa unapindisha hoja. Sijui kama kuna hoja ya kupinga hatua zinazochukuliwa. Hoja ni kupinga marufuku ya mikutano.
Mpendazoe, huu ulaghai unakusiadiaje katika kujenga taswira na haiba yako?
Labda onyesha sehemu moja tu wapinzani waliposema hatua zinazochukuliwa dhidi ya ufisadi na rushwa ni za kidikteta ili nasi tuunge tela
4. Rais Magufuli amekuwa na msimamo Mkali dhidi ya Ufisadi, wakwepa kodi, ubadhirifu kwenye serikali na halmadhauri na mashirika ya umma. Anapigania utajiri WA Nchi Yetu uwanufaishe watanzania wote. Ukweli Rais Magufuli ni Jibu Kwa maombi ya watanzania wengi kutokana na hali ilivyokuwa imefika.
Hali ilifika pabaya kutokana na usimamizi wa hapo CCM! Hakuna anayepinga hatua ilimradi tu ziwe ndani ya sharia
4. Upinzani wanachokifanya ni kutaka kuwapotodha watanzania ili waichukie serikali yao. Upotodhaji lengo ni uchochezi
Tusaidie kuelewa, marufuku ya mikutano ya kisiasa yapo katika sharia gani za nchi, yanatumika wapi na kwasababu zipi.
Hapo tutajua uchochezi wa vyama vya siasa
Kama huna kifungu cha sheria, kuna tatizo gani ukakaa kimya! kuliko kuendelea na 'uchochezi' huu unaoufanya! Kumbuka kuongea jambo bila ushahidi ndio uchochezi
Ukowapi udikteta wa Rais Magufuli? Lakini uchochezi wa UKAWA in dhahiri. UKAWA wanadai demokrasia inaminywa. Tukumbuke, mgombea UKAWA alivyopatikana. Ilikuwa ndani ya chopa na watu wachache siyo kwenye vikao. Hapakuwa na mchakato ulio wazi. Iko wapi demokrasia kwenye UKAWA ?
Mpendazoe, unawekaje demokrasia ya chama cha siasa katika mizani na demokrasia ya Taifa?
Kumbuka Rais alipoapishwa alitumia katiba ya JMT ya mwaka 1977.
Ni Rais wa kila mmoja, anachokifanya ni kwa ajili ya Taifa.
Unapochukua mambo ya vyama ukayaweka katika mizani na hadhi ya Rais, humtendei haki. Hadhi ya Rais ni kubwa kuliko chochote kile unachokifikiria.
Please hebu jaribu kuheshimu mamlaka za nchi kwa kutoziweka katika mizani na vyama vya siasa.
Pia tukumbuke, walimtuhumu Lowassa Kwa muda mrefu kuwa ni fisadi na wakawaeleza watanzania kuwa wanao ushahidi. Ghafla wakaamua awe mgombea urais.Uko wapi Uzalendo WA kweli ndani ya UKAWA ?
Uzalendo ungeanzia kumshtaki kwanza.
Hapo CCM hawakuweza kumfikisha katika sheria, walikuwa naye hadi hatua ya mwisho ya mchujo wa Urais. Hawakuweza hata kumzuia.
Aliotuhumiwa nao wapo Bungeni tena wakiwa na nyadhifa.
CCM imekaa kimya , uzalendo upi unaongelea Mpendazoe?
Hivi magamba tuliyoambiwa yalivuliwa?
Wizi unaoendelea hadi kwenye taasisi nyeti ukifunikwa kwa 'wamalize kazi' ndio uzalendo? Mpendazoe, unaongelea uzalendo gani?