Uko wapi Udikteta wa Rais Magufuli?

Uko wapi Udikteta wa Rais Magufuli?

Inaonekana hawajui maana ya dikteta! Dikteta gani atakupa hata nafasi ya kumwita yeye dikteta tena hadharani, halafu upate fursa ya kuhoji udikteta wake mahakamani?

Nawashauri waombe fursa ya kwenda kunywa chai ikulu wamweleze kwa ustaarabu hayo madai yao. Watapata maelezo na watamwelewa vizuri. Natumaini atawakaribisha.

Kwa mambo ya UKUTA wataumiza vijana bure.
 
najiuliza huyu magufuli anachokiogopa ni nini kuhusu mikutano ya upinzani(cdm)!!!!au kuna ukweli anauogopa ambao anahisi wakina lowassa wanaujua?!!!!
 
Inaonekana hawajui maana ya dikteta! Dikteta gani atakupa hata nafasi ya kumwita yeye dikteta tena hadharani, halafu upate fursa ya kuhoji udikteta wake mahakamani? Nawashauri waombe fursa ya kwenda kunywa chai ikulu wamweleze kwa ustaarabu hayo madai yao. Watapata maelezo na watamwelewa vizuri. Natumaini atawakaribisha. Kwa mambo ya UKUTA wataumiza vijana bure.
naona hukumuelewa lissu!!hakumuita dikteta kamili,alimuita dikteta uchwara.
 
Ukweli mchungu kwa machadema
Ukweli gani wakati kabla ya kuja huko ccm kaandika makala ya kumuomba msamaha Lowasa? Unafiki mtupu.

Hivi nyie ccm mnashindwa kumtambua mtu anayetafuta kula na yule mwenye mapenzi ya kweli? Huyu si aligombea ubunge kwa tiketi ya chadema akakosa? Je angepata angeuacha ubunge ajiunge ccm kwa sababu eti Magufuli anafanya vizuri? Kuweni makini na hawa watafuta vyeo!
 
Mr Mpendazoe, tatizo siyo hilo bali tatizo ni Magufuli kuendesha nchi kiimla, kukiuka misingi mingi ya katiba, kuamini kuwa nchi hii kuna CCM pekee na ni lazima kila Mtanzania awe mwana CCM.
Kajitoa ufahamu. Kaandika ili naye aonekane yuko pamoja
 
Mpendazoe aliwahi kuwa Mkristo. Sielewi kwa sasa yuko upande gani.

Kwa imani ya Kikristo mtu akiacha njia mbaya kwa mahubiri ya mwinjilisti, padre, askofu au mchungaji anakuwa mtu mpya. Itakuwa ni ajabu kwa kiongozi wa kiroho kumkataa mtu aliyemhubiria akabadilika. Hiyo ndo kazi waliyoifanya chadema kwa Lowassa. Lengo la kumkemea mtu mwovu ni ili abadilike. Akisha badilika nongwa ya nini?

Hivi wewe Mpendazoe una nongwa gani na Lowassa? Kama chama kinakemea waovu kwa nini kisiwapokee wakibadilika? kwa hiyo lengo la chama kukemea maovu ni nini? Je, waendelee na ouvu? au waache? Na wakiacha kwa nini wasifanya kazi pamoja ya kuwakemea wengine ili wabadilike?

Kuna mtu mmoja kwenye Biblia alikuwa anaitwa Sauli. Aliwaua wale wote waliokuwa wakimhubiri Mungu. Alikuja kubadilika na kuitwa Paulo. Alipo badilika akaungana na walewale wahubiri wa Mungu kueneza habari za Mungu.

Mbona wewe Mpendazoe ulitofautiana na wana CCM utahamia Chadema. Leo umeungana na uliokuwa ukipingana nao. Je, huna haki ya kuwa kiongozi au kugombea nafasi yoyote huko CCM?
 
Mpenda zoe, muda huu si wa kuwapinga chadema na ukawa kwa ujumla, ni kujiharibia siku tu maana chadema na ukawa hawajui hata wanajiita ukawa kwa kutaka mabadiliko ya katiba iliyopo kuwa ina mapungufu makubwa! Katiba inaruhusu nchi kuongozwa kijeshi kupitia rais wa nchi huyohuyo na ndio maana yeye ni amiri jeshi mkuu!
kama yy ni kiongozi wa majeshi basi na sisi wananchi ni wanajeshi pia
 
..,we jamaa mpendazoe ni vigumu kukuvumilia....wakati umeshindwa ubunge ccm ulikimbilia upinzani....ukapewa nafasi kugombea ubunge upinzani nako ukakosa... Na kila upande ulipotoka ulikuwa unapaponda...sasa umerejea ulikotoka unaponda upinzani...we jamaa huna unachosimamia zaidi ya tumbo lako...utakimbia hadi utachoka...lakini ujue kote unakopita unaacha maandishi yako...ambayo ndiyo utahukumiwa nayo... Hata hao ccm wanaokusifu sasa ndani ya mioyo yao wanakucheka na kukudharahu....
 
sizani kama waliopo chini yake huwa wanamshauri kwani wanafanya kazi kwa pressure sana(woga) mfano ni pale aliposema serikali ihamie dodoma angalia matamko yaliyotolewa na viongozi wake wa chini ni balaa
 
Vyama vinavyounda UKAWA vimetangaza kufanya maandamano yenye lengo la kupinga udikteta, UKUTA. Maana yake ni Kwamba serikali ya Rais Magufuli in ya kidikteta.

Niwakumbushe UKAWA yafuatayo:
1. Serikali ya Rais Magufuli imechaguliwa na watanzania kikatiba katika Uchaguzi mkuu 2015.

2. Kulingana na katiba, Rais hushauliwa na Baraza la mawaziri. Na pia Rais hushauriwa na Chama chake. Hivyo, Rais Magufuli anafanya maamuzi Kwa kushauriwa na taasisi hizi. Hivyo madai Kwamba anaamua bila kushauriwa hayana mashiko.

3. Madai Kwamba anawagandamiza baadhi ya watanzania, ni jambo la kushangaza. Tukumbuke wakati WA sakata la EPA, Chadema walipiga kelele sana wakati JK alipowaomba wezi WA fedha za EPA wazirudishe. Wakasema anaongea na wezi. Rais Magufuli amechukua msimamo tofauti, amekuwa dhabiti. Sasa Chadema wanadai dikteta. Hapana.

4. Rais Magufuli amekuwa na msimamo Mkali dhidi ya Ufisadi, wakwepa kodi, ubadhirifu kwenye serikali na halmadhauri na mashirika ya umma. Anapigania utajiri WA Nchi Yetu uwanufaishe watanzania wote. Ukweli Rais Magufuli ni Jibu Kwa maombi ya watanzania wengi kutokana na hali ilivyokuwa imefika.

4. Upinzani wanachokifanya ni kutaka kuwapotodha watanzania ili waichukie serikali yao. Upotodhaji lengo ni uchochezi.

Ukowapi udikteta wa Rais Magufuli?, lakini uchochezi wa UKAWA in dhahiri.
UKAWA wanadai demokrasia inaminywa. Tukumbuke, mgombea UKAWA alivyopatikana. Ilikuwa ndani ya chopa na watu wachache siyo kwenye vikao. Hapakuwa na mchakato ulio wazi. Ikowapi demokrasia kwenye UKAWA ?

Pia tukumbuke, walimtuhumuLowassa Kwa muda mrefu kuwa no fisadi na wakawaeleza watanzania kuwa wanao udhahidi. Ghafla wakaamua awe mgombea urais. Uko wapi Uzalendo WA kweli ndani ya UKAWA ?

Watanzania tumuunge Mkono Rais Magufuli.
Rais kukataza mikutano ya siasa ni udikteta.

Udikteta ni kuacha utawala wa sheria na kusema unachotaka wewe ndiyo kiwe sheria.

Katiba inaruhusu mikutano ya siasa.

Rais Magufuli anatupilia mbali katiba. Anataka neno lake ndiyo liwe sheria.

Huo ni udikteta.
 
Mleta mada mwenyewe kakimbia hana reply hata moja, ni wazi kabisa anaona alichoandika hakukaa chini kujipanga vizuri kabla ya kuandika.

Hili swali la "uko wapi udikteta wa Rais Magufuli" nakushangaa unaliuliza alafu arguments zako ni mambo positive aliyoyafanya, ilitakiwa uongelee yale ambayo upande wa pili wanayasema kila siku alafu utoe point kwa nini unahisi wanayosema si sahihi. Statement yako ni sawa na kusema "Iko wapi roho mbaya ya Osama bin laden" alafu arguments zako ukatumia "alikua mtu wa dini, alikua na familia blah blah" unaacha kuongelea yale aliyoyafanya negative hadi yakapelekea watu kumchukulia negative.

Nadhani umenielewa, kama ndiyo basi jipange alafu rekebisha post yako kutoa arguments ya kwa nini unahisi watu wanayoyapigania hayafai, sio kuhusu CDM, wala CUF, UKAWA wala nini, ni kuhusu Rais, weka argument zako pale.

Nikupe mfano kabisa unaweza ongelea swala la kukataza vyama vya siasa kufanya siasa kua kinyume na katiba, baadhi ya matamshi na vitu kufanywa kiholela mfano kusema "traffic anapokea 5000 sio rushwa", "wanafunzi hawa ni vil.aza", "mkiniharakishia kesi hiyo haraka kidogo", "serikali haitolipa" (hii baada ya kampuni kushinda kesi ya madai dhidi ya serikali).

Sema kwanini unahisi haya mambo sio negative kila mtu anajua kayafanya coz yapo kwenye media. Hiyo mifano inatosha kabisa kukuonyesha jinsi ulivyotakiwa uweke arguments zako.
 
..,we jamaa mpendazoe unatia kinyaa....ni vigumu kukuvumilia....wakati umeshindwa ubunge ccm ulikimbilia upinzani....ukapewa nafasi kugombea ubunge upinzani nako ukakosa... Na kila upande ulipotoka ulikuwa unapaponda...sasa umerejea ulikotoka unaponda upinzani...we jamaa huna unachosimamia zaidi ya tumbo laki....utakimbia hadi utachoka...lakini ujue kote unakopita unaacha maandishi yako...ambayo ndiyo utahukymiwa nayo... Hata hao ccm wanaokusifu sasa ndani ya mioyo yao wanakucheka na kukudharahu....we jamaa huna tofauti na ma.laya ama shoga anaebadili wanaume ili kujipatia kipato.....akili zenu moja....kinyaa...
Kapi lao limerudi.
Linajifanya halijui kuwa UKUTA haipingi hayo aliyoyataja bali kufutwa kwa mikutano na maandamano ya vyama vya kisiasa hadi 2020, wakati nyinyiem wanafanya.
 
Huwa nashangazwa na akili za watu kama akina Fred Mpendazoe!! Leo anaongea hiki kesho anaongea hiki!! Kwa mtizamo wako unadhani Wajinga bado wengi sana hapa Tz?
 
Awali nilidhani walipiga debe wa ccm humu JF ni vijana wadogowadogo almaarufu kama lumumba buku 7 kumbe ni vijeba yenye na mamvi kabisa. Hii nchi ina safari ndefu sana.
Mpendazoe hebu tusaidie, hivi maisha yako yameshindikana kabisa mjini hadi kuamua kuishi kwa hisani ya chama kwa ujira wa buku 7 kwa kila post?
Anyway! Mwanachama mpya wa ccm katika ubora wake!!!
 
Fred Mpendazoe
NASHINDWA KUAMINI kama ww ulikuwa hadi Mbunge wa Jimbo la uchaguzi la Kishapu
Nakubali sasa na nashukuru kwa wana Segerea na baadae Kishapu kukukata
kwenye haki za binadamu ndani ya katiba freedom of speech/expression ndiyo kila kitu
Katiba IMERUHUSU watz kukutana kujadili siasa
Rais anapoipinga katiba aliyo apa kuilinda ni UDIKTETA mbaya sana
Rais anapotaka maneno yake ndiyo yawe sheria ni UDIKTETA mbaya sana

Ninachokijua toka kwako Mpendazoe ni kuwa unavizia huruma ya Rais akukumbuke ktk teuzi zake
Njaa mbaya sana inaharibu akili
 
1.Kuudhibiti ufisadi
2.Kuasisi mmahakamaya mmafisadi.
3.Kudhibiti MMatumizi.
4.Kusimamia nidhamu ya utumishi wa umma.
5.Kufufua ATC,TRL,Meli....Nk
6.Kuimarisha huduma za afya,elimu nk.
7.Kuongeza mapato ya serikali nk..
yote sawa lakini ailinde katiba ya nchi aliyoiapia, aruhusu mikutano na maandamano ya amani ya kisiasa.
 
Rais amezuia mikutano yote ya siasa kwa wanasiasa nje ya majimbo yao. kinyume na katiba inavyosema.

Hiyo namba mbili kama ni kweli, ccm ni zaidi ya uozo!
 
kwanza naandika hivi bila kusoma andiko lako nimesoma kichwa tu.nishachoka sana undumila kiwili aueleweki uliandika sana raia mwema nikakuona wa maana kumbe njaa tu ndo inakusumbua njaa mbaya sananhuna lolote shida sana mazee kama hya ndani ya nchi
 
Back
Top Bottom