maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,029
- 1,345
Nitaendelea kuamini ktk maisha yangu yote kwamba, kwa Chadema kumpokea Edward Ngoway Lowassa, fisadi mkubwa aliyetimka kutoka CCM na kumtimua kishenzi katibu mkuu wao Dk Wilbroad Slaa, Chadema walifanya dhambi kubwa ambayo itawagharimu na wataijutia kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
Eti Lowassa aliyechukuliwa na Chadema kama fisadi namba moja ghafla aligeuka kuwa mfalme asiye na doa na Slaa aliyechukuliwa na Chadema kama malaika ghafla akageuka kuwa shetani na mchawi ktk chama hicho.
Kwa matokeo ya uchaguzi wa leo napenda kumwalika Dk Slaa akae mkao wa kula ashuhudie anguko la mafisadi waliomfukuzisha kutoka chama alichokipigania kufa na kupona kwa zaidi ya miaka 20.