Ukizabwa kibao hadharani...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,398
39,547
Unatembea na mamsap kwenye Mall au mtaani na katika pitapita mnapishana na kigori ambaye ni 'fwine' kweli kweli. Umejaribu kujizuia kugeuza shingo lakini kutokana na udhaifu wako unageuza kufuatilia kama paka aliyemuona panya kwenye kingo ya jicho lake.. Unajaribu kurudisha kichwa mbele na unakutana na mamsap ambaye amefura na kabla hujasema lolote anakuzaba ZAAP!!! unaona nyota halafu anakuambia;

"kama unamtaka umfuate!" halafu huyo anaanza kuendelea....

what do you do next... ?

NB: Sijachapwa kibao namzungumzia jamaa yangu mmoja hivi (wink wink)
 
...mkjj, kutokana na mashairi yako kule kwenye ukumbi wa lugha, napelekeshwa na hisia kuamini kuwa, huyo aliyekumbwa na kibano ni mtu wako wa karibu sana, tena sana sana sana sana sana sana tu.........


....what do yo do next - you apologize and assure her that you won't do that again, ni mambo ya Mungu haya nafikiri maana macho hayana pazia wahenga walishasema, similarly, - ordering your meal doesn't prevent you from perusing the menu!!

;)
 
..ungekuwa wewe ungefanyaje?

..si unaenda kupata moja moto moja baridi!kupunguza hasira na maumivu,lol!
 
Simply dont react at all!

Ni reaction yako itakayoendeleza hiyo topic ambayo kwa vyovyote vile ..you will loose in all direction! and you know it!

Whatever the case...dont ...dont react and never respond to it in any way!

Why?

Hakuna kilichotokea!

Kwani ni nini kilichotokea!

Nothing!!

Ndio maana Huna responce wala reaction!

Kuanzia hapo topic hiyo ikija/kama itakuja.. you have to learn to express sense, nobility and wisdom...You know what ?That is what they need to hear not the silly arguments....!

If you r very good she wont see that you r ar changing that topic to more usefull ones!!
 
Mhhh!!! Mkjj, kwani kuangalia ni vibaya?? Ndio maana tukapewa macho tuyatumie. Nadhani huyo mamsapu anatakiwa kuwa muelewa kuwa kazi ya macho ni kungalia/kutazama sasa mambo ya kuzibuana vibao hadharani si uungwana hata kidogo kama ni mimi siwezi kunyamaza.... Tutaenda kumalizana tukifika maskani...
 
...mkjj, kutokana na mashairi yako kule kwenye ukumbi wa lugha, napelekeshwa na hisia kuamini kuwa, huyo aliyekumbwa na kibano ni mtu wako wa karibu sana, tena sana sana sana sana sana sana tuKweli kabisa huyu katudanganya nahisi kuwa yeye ndiye kazabwa hicho kibao!!!! LOL

ordering your meal doesn't prevent you from perusing the menu.............This is a good one,but you cant compare the two literaly, nyie waume ndio wenya hii tabia, and what i wd say kama unatembea na bibie basi, avoid straying your eyes huku na kule, give her utmost attention, make her feel that she is the only one 'u can see', macho yatangishe kama hampo pamoja, the apology is gd, yaitwa damage control.


but hicho kibao pia poa, kama ndiyo adabu yako!! ama mwasemaje!!!
 
acheni nidhamu ya waoga nyie watu sioni sababu ya kukauka shingo liwe limenyooka mbele kama army tanker kisa mamsapu inapobidi kuangalia anagalia kama atatafsiri tofauti ni suala la kumuelewesha tu...
 
Kweli kabisa huyu katudanganya nahisi kuwa yeye ndiye kazabwa hicho kibao!!!! LOL

ordering your meal doesn't prevent you from perusing the menu.............This is a good one,but you cant compare the two literaly, nyie waume ndio wenya hii tabia, and what i wd say kama unatembea na bibie basi, avoid straying your eyes huku na kule, give her utmost attention, make her feel that she is the only one 'u can see', macho yatangishe kama hampo pamoja, the apology is gd, yaitwa damage control.


but hicho kibao pia poa, kama ndiyo adabu yako!! ama mwasemaje!!!

..... tunasema hivi; hicho kibao angepigwa mwanamke kwa kosa/tukio hilo hilo, jambo zima lingebadilika na kuwa kosa la jinai!!

....wanaume tunavumilia mambo mengi sana ambayo wanawake huyafanya, lakini wakifanyiwa wao, wako reactionary na mara nyingi wanaongozwa na emotions badala ya wisdom au logic katika utatuzi.

....mfano, ni mara ngapi unaona demu/mke/mwanamke aliye katika relationship aki scream at the highest pitch possible kama msichana mdogo aliyetishiwa nyau, baada ya kumwona mwamuziki/mwanandanda au actor wa movie wa kiume anayemzimia?!! Si hivyo tu, bali demu/mke/mwanamke huyo huyo aliyekatika relationship nawe anaweza kuwa anamwongelea star huyo kila wakati bila kujali hisia zako... lakini jaribu wewe, lahaula...ndipo utakapojua kuwa ndimu siyo kiungo!!
 
If my memsap ever slap me, regardless of wherever we'll be (apart from home, kwani si picha nzuri kwa watoto kuona baba anachapwa kibao na mama) mimi nitaangalia around nione km kuna mtu anyenijua kashuhudia tukio, na km hakuna I'll simply ignore the whole matter.

Lakini ikija tokea siku huyo memsap anafanyiwa 'psssiiii' naye akaangalia upande huo then that'll be an opportunity for my revenge.

Wanawake wivu bure wakati wanajitongozesha kwa wanaume - omba uwee choka mbaya na jirani yako ana gari na nyie mnapanda basi.
 
Mzee hujakutana na mwanadada mnaangalia television anakwambia anampenda Nelly, 50 Cents au Thiery Henry???? jaribu wewe kusema unamzimia Rehanna au demu yeyote mkali uone macho yatayokutazama...ingekuwa ni AK-47 mzee umekwisha...Hayo mambo yapo ni suala la kuelewa tu,
 
Haya ndio yaliyokukutaaaaaaaaaaaaaaaaaa

watch attached video
 

Attachments

  • attention.zip
    627.3 KB · Views: 76
Kama una kijicho kwa nini uwe na mamsap?

Kama una mamsap kwa nini una kijicho?

Kuwa kama mimi, ukiwa na kijicho huna mamsap unatafuta, ukipata unaacha kijicho.
 
Duu
mwanakijiji mama aliku arrest.

Mimi nafikiri hakuna haja ya kugombana lazima ujue mwanamke na mwanaume tupo tofauti kidogo namna ya ku handle mambo hayo.

Ukizabwa kibao wewe mgeukie na mwambie SALALEEEE!!!NAsifia uumbaji.
 
tatizo MKJJ una vitendawili sana..anyway ngoja nitege sikio nielewe kitendawili hiki kinamaanisha nini..ila kama yamekukuta pole mzee ndio matatizo ya kuoa kabla hujamaliza kutest sampuli mbalimbali
 
Tatizo ni kuwa jamaa sasa kanyimwa hakuna cha msosi wala "nini" ati hadi amuombe "apology" ya Kiswahili...
 
Unajua huyo Demu alifanya poa sana kwani alihisi kama huyo jamaa ni mtu wa kuruka huku na kule.Unajua ukianza kuangalia,utatamani na kisha utafuata.

Pia huyo demu alihisi ni kama vile huyo jamaa haridhiki na huyo aliye nae.She felt offended na inaudhi kweli kweli.

Hata hivyo huyo jamaa nae inawezekana aliangalia tu kama kawaida ya macho kuangalia huku na huko lakini hii ya kugeuza shingo tena mi siko na yeye hapo
 
Unatembea na mamsap kwenye Mall au mtaani na katika pitapita mnapishana na kigori ambaye ni 'fwine' kweli kweli. Umejaribu kujizuia kugeuza shingo lakini kutokana na udhaifu wako unageuza kufuatilia kama paka aliyemuona panya kwenye kingo ya jicho lake.. Unajaribu kurudisha kichwa mbele na unakutana na mamsap ambaye amefura na kabla hujasema lolote anakuzaba ZAAP!!! unaona nyota halafu anakuambia;

"kama unamtaka umfuate!" halafu huyo anaanza kuendelea....

what do you do next... ?

NB: Sijachapwa kibao namzungumzia jamaa yangu mmoja hivi (wink wink)

...lizime soo chap chap, 'jidai' kumgeuzia na shavu la pili 'azibue, kisha unajizimua kwa kumwambia; "aaahh nawe huachi wivu wako weye, mwanamke yule ndio wa kunirusha roho mimi?, kakuzidi nini!?"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom