Ukiweza fanya biashara hii

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Nilipata kutembelea bonde la Kilombero(Ifakara) wakati fulani. Wakati wa msimu wa kilimo,kuna uhitaji mkubwa sana wa matrekta. Unakuta mtu mmoja ana oda ya kazi mpaka anachemsha. Yaani trekta linafanya kazi sana, wakulima wanalipa in-advance ili wapate huduma. Ukimaliza kulima trekta linageuka basi wakati wa masika, kumbuka huko mvua ni nyingi, kwa hiyo barabara hazipitiki.

Wakati wa mavuno, trekta linakuwa lori, kuna vijiji vina matatizo makubwa ya usafirishaji mazao. Jamani fursa za biashara ni nyingi mno.
 
Asante sana Malila, nakuunga nkono ni kweli kabisa shida ya matrecta bondeni kule ni kubwa mno! niliwahi kuoda kulimiwa nikakosa na nikapata hasara mwisho wa siku, kazi ni nyingi mno! niko kimya sana Bro, najipanga ile mambo yetu!!
 
Nilikuwapo huko miaka ya 2007/2008... Ni kweli usemayo... sema Mto ukijaa kaa tayari kulala na mamba chumbani..:biggrin1:
 
Ifakara, Idete, Ruipa, Mbingu, Mgeta, Chita, Mlimba!,Mahenge, Viwanja60,

Utatengeneza hela ila Hujuma uwe macho!,
 
Asante sana Malila, nakuunga nkono ni kweli kabisa shida ya matrecta bondeni kule ni kubwa mno! niliwahi kuoda kulimiwa nikakosa na nikapata hasara mwisho wa siku, kazi ni nyingi mno! niko kimya sana Bro, najipanga ile mambo yetu!!

Utakapokuwa tayari njoo, utatukuta mbele ya safari. Ila troup inakuwa kwa speed ya jumbo jet mkuu wangu.
 
kwa bei ya diesel inavyopaa mkulima atamudu kweli kukodi trekta?heka 1 sh ngapi kulima,lita 1 unalima eneo kiasi gani?
 
Nilikuwapo huko miaka ya 2007/2008... Ni kweli usemayo... sema Mto ukijaa kaa tayari kulala na mamba chumbani..:biggrin1:

Mimi na mamba damu damu, pale mkuranga walijichanganya wakaingia anga zangu nikawaitia Mzungu fulani, kawalamba wote hadi mayai yao. Hiyo nayo fursa nyingine.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom