Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kuna wakati madaktari wa nchini India walimudu kurejesha uume wa kijana mmoja aliyefumaniwa na kukatwa sehemu zake za siri, na hivi sasa uume huo unafanya kazi kama kawaida.
Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 18 wakati huo, Jagdish Jivan Baria, alikwenda kuzini wakati akitokea hekaluni kusali, ambapo alifumaniwa. Wafumaniaji akiwemo mwenye mke walimpiga kijana huyo na kukata uume wake.
Waliukata uume huo walikimbia nao, mmoja wao akiwa ameutia mfukoni. Hebu fikiria, mtu anakata uume wa mtu kisha anauweka mfukoni mwa suruali yake nakukimbia nao!
Hata hivyo wazazi wa kijana huyo waliwahi kutoa taarifa polisi, ambapo uume huo ulipatikana. Ulipopatikana waliuweka kwenye mfuko wa nailoni na kuuweka kwenye jokofu.
Ushonaji wa uume huo ulifanywa ikiwa imepita saa 13 tangu ukatwe. Daktari aliyefanya ushonaji huo ambao ulichukua saa tisa, Sandil Sharma alisema, kama ‘kitu' cha mwanaume kikiwahiwa kuhifadhiwa kwenye jokofu baada ya kukatwa, ushonaji wa kukirudishia unakuwa rahisi.
Hadi kufikia mwaka 2007 duniani kote ushonaji wa kurejesha sehemu za siri zilizokatwa, umefanyika kwa mafanikio mara 47 tu, hii inaonesha ni kwa kiasi gani ushonaji wa kurejesha sehemu za siri za mwanaume zinapokatwa , una ugumu wake.