Ukiwa Rais unafanya kila kitu, ukiondoka unafanywa kila kitu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
UKIWA RAIS UNAFANYA KILA KITU, UKIONDOKA UNAFANYWA KILA KITU

MIAKA 38 ya mamlaka, amri, ushawishi na nguvu ya kufanya kila kitu, tamati yake ilikuwa Septemba 2017. Baada ya hapo, zikaingia zama za kufanywa chochote. Ni story kutoka Angola. Mhusika ni Rais wa Tatu, Jose Eduardo dos Santos.

Kabla ya Septemba 2017, familia ya Eduardo dos Santos ‘Zedu', iliweza kufanya kila kitu. Nani angethubutu kusimama katikati kuzuia mke au watoto wa Zedu wasifanye walichotaka Angola? Nchi ikawa mali yao. Familia namba moja. The most powerful family in Africa. Thubutu kubisha nikupe kelbu!

Baada ya Septemba 2017, imegeuka familia inayoishi kwa mahangaiko na wasiwasi. Angola yao si taifa salama kwao. Memba wa familia ya Zedu, wamekuwa raia wa Angola wanaosakwa kwa tuhuma za uhalifu kuliko wengine wote nchini humo.

Kipindi Zedu akiwa Rais, aliweza kumkabili, kumdhibiti na hata kumuua mpiganaji roho ya paka, Jonas Savimbi, aliyekuwa anaongoza jeshi la uasi la Unita. Siku hizi Zedu hana ubavu wa wowote. Hakuna askari anayemtii. Haitwi tena Amiri Jeshi Mkuu.

Zedu alipotangaza kung’atuka baada ya kukaa madarakani miaka 38 (1979-2017), alidhani maisha yangekuwa rahisi. Madaraka ya nchi aliyaacha ndani ya chama chake cha MPLA. Halafu aliyeshika usukani ni kijana wake, João Lourenço ‘JLo’. Zaidi, JLo alikuwa Waziri wa Ulinzi chini ya Zedu. Shaka ingetoka wapi?

Matarajio ya Zedu yalikuwa kuacha uongozi wa nchi na serikali lakini angeendelea kuwa kiongozi wa chama tawala, MPLA. Hilo halikuwezekana. Zedu aliiona nchi ngumu mara tu JLo alipochaguliwa kuwa Rais wa Angola.

JLo alipoingia madarakani, alianza kwa kumfurusha Isabel dos Santos, kwenye kampuni ya Sonangol, ambayo ni taasisi ya umma inayosimamia shughuli zote za uvunaji na uuzaji wa mafuta Angola. Isabel ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Sonangol. Aliteuliwa na baba yake, Zedu, wakati akiwa madarakani.

Isabel ni mtoto wa kwanza wa Zedu. Alimpata na mwanamke wa Kirusi, Tatiana Kukanova. Zedu alilazimika kuachana na Tatiana ili kutimiza matakwa ya kuwa kiongozi mkubwa wa kisiasa Angola. Uraia wa Tatiana, ungemuwekea kauzibe.

Baada ya Baba wa Taifa la Angola, Agostinho Neto, kufariki dunia Septemba 10, 1979 kwa maradhi ya homa ya ini na kansa, Lucio Lara, ambaye alikuwa bosi namba mbili ndani ya MPLA, alikaimu Urais wa Angola kwa muda, lakini aligoma kushika madaraka ya kudumu.

Lara akaendesha uchaguzi, Zedu akaingia madarakani mwaka 1979. Tatiana alimchukua Isabel wake, wakaenda kuishi Uingereza. Isabel alipokua, akarejea Angola. Zedu akampokea, mtoto wa kwanza tena!

Kuanzia hapo, Isabel akaibuka kuwa mfanyabiashara tajiri, kisha mwanamke tajiri kuliko wote Afrika. Utajiri ambao kwa miaka mingi ulihusishwa na uporaji wa mali za umma Angola. Kama haikutosha, Zedu alimteua Isabel kuwa Mwenyekiti wa Sonangol. JLo aliposhika madaraka akamtimua.

Isabel sio mtoto pekee wa Zedu aliyetemeshwa kazi serikalini baada ya JLo kushika mpini. Yupo pia Jose Filomeno dos Santos ambaye Zedu alimpata na mwanamke raia wa Angola, Filomena Sousa.

Jose Filomeno ‘Zenu’ ni mtoto wa kiume wa kwanza wa Zedu. Mwaka 2012, Zedu alimteua Zenu kuwa Mwenyekiti wa Mfuko Mkuu wa Uwekezaji (FSDEA). Mfuko unaosimamia mali nyingi za umma. JLo baada ya kuingia madarakani, alimpiga chini Zenu.

Haitoshi, Zenu baada ya kung'olewa FSDEA, alikamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha, kujitajirisha kwa njia batili na kushiriki uhalifu wa mipango. Alibainika kuhamisha fedha, dola 500 milioni (Sh1.2 trilioni) kwenye akaunti yake katika benki moja ya Uingereza.

Zenu alikaa mahabusu mwaka mmoja na miezi sita, kabla ya kuachiwa Machi mwaka jana. Fedha hizo, dola 500 milioni, zilirejeshwa Benki Kuu ya Angola.

Kama utataka kuelewa utaelewa; ukiwa Rais unakuwa na mamlaka yote, unaweza kufanya chochote. Ukishatoka madarakani, mrithi wako anaweza kukufanya chochote.

Hivi karibuni, mwanamke aliyekuwa untouchable DRC, Jaynet Kabila, alishuswa kwenye ndege, akahojiwa kwa saa kadhaa na maofisa uhamiaji wa Kinshasa, baadaye akarudushwa kwenye ndege, kabla ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

Jaynet ni dada wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila. Tena si dada wa kawaida, ni pacha wake. Na ndiye msimamizi mkuu wa mali za Kabila. Kipindi kaka yake ni Rais wa DRC, Jaynet ungethubutu vipi kumsogelea?

Huyo ni Jaynet ambaye pacha wake bado ana nguvu nyingi DRC. Urais wa Felix Tshisekedi unashikiliwa sana na Kabila. Pamoja na hivyo, uhamiaji wamekuwa na uthubutu wa kumchomoa Jaynet kwenye ndege. Ingekuwaje Kabila asingebakisha nguvu yoyote?

Ongezea hapo kuwa Jaynet ni mbunge katika Bunge la DRC, akiwakilisha jimbo la Kalemie. Hapohapo, Kabila ni Seneta wa Maisha. Ukiwa Rais unakuwa umeshika mpini. Unaweza kumwelekezea makali yeyote. Ukiondoka, mpini unashikwa na mwingine. Akiamua kukuelekezea makali, hakuna dua utakayoisahau.

Tuendelee na story ya Angola. Kwa Zedu na familia yake. Desemba mwaka jana, binti mwingine wa Zedu, Tchize dos Santos, alivuliwa ubunge, kwa hoja ya utoro bungeni.

Kipindi Zedu akiwa Rais, Tchize alikuwa mwakilishi kupitia MPLA, aliyekuwa na ushawishi mkubwa. Baada ya kuona familia yao inaandamwa, alikimbia nchi. Akaweka maskani Ureno. Bunge likapitisha maazimio ya kumvua ubunge kwa utoro.

Julai 2017, kabla hata uchaguzi kufanyika, Zedu alisafiri kwenda Barcelona, Hispania mara mbili. Taarifa iliyotolewa ni kwamba alikwenda kwenye matibabu. Septemba 2017, kipindi cha makabidhiano ya uongozi, Zedu alisafiri kwenda Barcelona.

Kabla ya kusafiri, Zedu alikataa kutumia usafiri wa Shirika la Ndege la Angola (TAAG), aligoma kuongozana na msafara wa kiitifaki kama Rais mstaafu. JLo alijaribu kumshawishi Zedu abadili mawazo lakini alikataa. Mwisho Zedu alisafiri na ndege ya Shirika la Ureno (TAP), na taarifa ya safari ilitolewa nusu saa kabla ya safari.

Tangu wakati huo, Zedu alijichimbia Barcelona, na alirudi Angola, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa MPLA Agosti 2018. Alikabidhi uenyekiti wa MPLA kwa JLo, kisha akarejea tena Barcelona. Amejichimbia mazima.

Juni 16, mwaka jana, Isabel, mwanamke tajiri Afrika, alipost Instagram picha yenye kumwonesha Zedu akiwa na wajukuu wake, Barcelona. Akaandika caption: “Tunafurahia Jumapili na familia. Maficho yetu salama tunapotumia nishati na kupata upendo. Kwetu familia ni kila kitu, nguzo yetu.” Chukua tafsiri, Barcelona ni maficho yao salama.

Isabel pia amekuwa akipost picha mbalimbali za baba yake na wanaye wengine pamoja na wajukuu, katika matukio mbalimbali ya furaha, kuanzia chakula cha jioni mpaka salamu za Krismasi na Mwaka Mpya. Ni kuonesha kila kitu kipo sawa. Hata hivyo, maonesho hayo yapo mbali mno na kitovu cha ukweli.

Desemba 23, mwaka jana, Mahakama ya Angola, ilitoa hukumu ya kutaifisha mali za Isabel zenye thamani ya dola moja bilioni (Sh2.3 trilioni), akaunti zake benki zikafungwa na hisa zake zote kwenye kampuni za ndani, zitaifishwe.

Kwa uamuzi huo, Isabel amenyang'anywa hisa zake za umiliki wa kampuni ya mtandao wa simu wa Unitel, BFA (benki) na kampuni ya saruji ya Cimangola. Yote hayo sababu ikitajwa ni matumizi mabaya ya ofisi alipoongoza kampuni ya Sonangol kwa miezi 18. Zingatia, Angola ni nchi ya pili Kusini ya Jangwa la Sahara kwa utajiri wa mafuta.

Kuna mdukuaji anaitwa Rui Pinto. Kwa sasa yupo mahabusu Ureno, akikabiliwa na mashitaka udukuzi na uvujishaji wa siri za Serikali ya Ureno. Huyo ndiye aliyesababisha seleka. Alidukua na kuvujisha nyaraka zaidi ya 700,000 zenye kuonesha Isabel na washirika wake, walivyoitumia Sonangol, kupiga hela zaidi ya dola bilioni moja.

Siku mbili baada ya waendesha mashitaka Angola, kumtaja Isabel na aliyekuwa msimamizi wa akaunti za Sonangol, Nuno Ribeiro da Cunha, mtu huyo wa benki (Nuno), alikutwa amekufa kwenye moja ya nyumba zake Ureno. Ripoti za uchunguzi wa maiti zilibainisha kuwa Nuno alijiua.

Wakati akifikwa na mauti, Nuno alikuwa mtendaji mkuu wa Benki ya EuroBic, inayofanya kazi zake Lisbon, Ureno. Isabel anamiliki hisa asilimia 42.5 za benki hiyo. Na ndiye mwanahisa mwenye uamuzi (majority shareholder) kwa sababu ana hisa nyingi kuliko wengine wote.

Kutokana na kashfa hiyo ya uchotaji wa fedha za umma Angola, EuroBic wametangaza kuuza hisa za Isabel ili kujitenga na mwanamke huyo tajiri, mtoto wa Zedu, Rais wa zamani wa Angola.

Mwishoni mwa Juni mwaka jana, Isabel alipost picha ya kaka yake waliyechangia baba, José Eduardo Paulino ‘Coreon Du', ambaye ni msanii maarufu Angola, akionesha kuwa tayari naye ameshajiunga nao Barcelona.

Post hiyo, ilimaanisha kuwa katika watoto saba wa Zedu, ni mmoja tu, Zenu (Jose Filomeno) ndiye bado yupo Angola, na kinachombakisha bila shaka ni mashitaka aliyonayo, maana haruhusiwi kutoka nje ya Angola. Na hati ya kusafiria kanyang'anywa.

Coreon Du mama yake anaitwa Maria Luisa Abrantes Perdigao. Watoto wa Zedu na mama zao kwenye mabano ni Isabel (Tatiana), Zenu na Tchize (Filomena Sousa), Coreon Du (Maria Luisa), kisha wadogo wao watatu, Eduane Danilo, Joseana na Eduardo Breno ambao mama yao ni Ana Paula dos Santos.

Ana Paula alikuwa mwanamitindo na mhudumu wa ndege. Zedu alipomtupia jincho, alikamatika na kuanza kutoka naye kimapenzi kabla ya kufunga ndoa mwaka 1991. Wakati wanaoana, Ana alikuwa na umri wa miaka 28, Zedu 49. Na Ana alikuwa tayari mjamzito.

Katika watoto saba wa Zedu, ni Coreon Du pekee aliyempata nje ya ndoa. Wengine wote, mama zao alifunga nao ndoa.

Kipindi akiwa madarakani, Zedu alifanya kila alichotaka. Aliweza kulifanya Bunge kutunga sheria za kumruhusu kuchota fedha za umma alivyotaka, leo ameondoka madarakani, nyumbani hakukaliki. Si yeye wala watoto wake.

Alipokuwa madarakani, alianzisha cheo cha Waziri Mkuu na kumteua mdogo wake, Fernando da Piedade Dias dos Santos. Kisha akamteua kuwa Makamu wa Rais. Nani angemzuia?

Leo Fernando ni Rais wa Bunge la Angola, lakini hana uwezo wa kumsaidia kaka yake ili watoto wake wasisumbuliwe. Fernando alishindwa hata kuzuia mtoto wa kaka yake, Tchize, asifukuzwe ubunge wakati yeye ndiye mkuu wa Bunge.

Elewa hili; ukiwa Rais unaweza kufanya chochote. Ukiondoka utatendwa chochote, inategemea na utashi wa atakayeingia madarakani baada yako. Rais mstaafu na watoto wake wapo uhamishoni. Aliyebaki, ana kesi, haruhusiwi kutoka.

Isabel, mwanamke tajiri sana, hajulikani anaishi wapi kama makazi yake rasmi. Mara Uingereza, mara Ureno. Mwenyewe anadai nchi ya makazi yake ya kudumu kwa sasa ni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), lakini mara kwa mara yupo Barcelona kwa baba yake. Anasema Angola si salama kwa maisha yake na familia yake. Yeye na mumewe, Mkongomani Sindika Donkolo, wanasakwa waelekezwe kibila.

Wana fedha nyingi. Wana majumba na mali za kuwawezesha kuishi maisha ya daraja la kwanza kila nchi watakayo duniani, ila amani hawana. Ni kipindi hiki, pengine watoto wa Zedu wanatamani bora baba yao asingekuwa Rais. Pengine, Zedu anawaza bora angepatana na Savimbi miaka ile ya Vita ya Kiraia Angola, na hata angempa Urais Savimbi kuliko alivyomwachia JLo. Wanapata tabu sana.

Ni simulizi ya Zedu, Rais aliyeliongoza taifa linaloshika nafasi ya tatu kwa uchumi mkubwa Kusini ya Jangwa la Sahara. Nchi yenye utajiri mkubwa mafuta. Inamhusu Isabel, mwanamke tajiri zaidi Afrika, akikadiriwa kuwa na utajiri wa dola 2.1 bilioni (Sh4.9 trilioni). Hiyo ni kwa mujibu jarida la kimataifa la utafiti na thamini za mali za watu, Forbes.

Utajiri huo unatajwa kuwa cha mtoto kwa ule alionao Zedu. Ripoti zinasema Zedu ana utajiri wa dola 20 bilioni (Sh46 trilioni). Jumba lake la kifahari linalotazama bahari, Miramar, Luanda, lipo tupu. Limepooza.

Afrika; ukiwa Rais unafanya kila kitu. Ukiondoka unafanywa kila kitu.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Hapo mwamba Jlo (kulia) kimoyo moyo anamwambia babu Dos santos (kushoto) "subiri nikamate nchi, ntakunyoosha"
Screenshot_20200218-153815_Chrome~2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi ni mrefu, nimesoma heading tu, nadhani ujumbe uko wazi, cha msingi ukiwa Raisi inakupasa kuheshimu katiba na sheria za nchi tofauti na hilo utabomoa nchi, utajenga maadui na uta hatarisha maisha yako baada ya u-Raisi. Ukiona mwenzako ananyolewa anza kutia maji (hawa ni wahenga wa zamani).
 
Bonge la uzi nahisi hata hawa wanaojifanya wanasiasa huwa wanachukua humu nondo kama hizi

Zamani matajiri wangeweza kufanya chochote kile ila kwny awamu yangu wanaweza kufanywa chochote kile-Bwn Yule
 
Back
Top Bottom