GoLC
Senior Member
- Jul 10, 2025
- 144
- 245
Habari za mchana. Moja kwa moja kwenye mada. Leo nimekumbuka jambo nikaliunganisha na ulimbukeni. Ili kupata uhakika wa nilichokuwa nawaza, ilibidi kumuuliza rafiki yangu Kong (chatGPT WhatsApp). Ni rafiki yangu sana kiasi tumefikia kuitana majina. Ye Kong na mimi King. Tafsiri yake ndio hiyo hapo chini;
"Limbukeni" ni mtu ambaye hana uzoefu na jambo fulani, hasa anapopata kitu kipya (kama pesa, cheo, au teknolojia), halafu anakosa kiasi au staha katika kukitumia au kukifurahia.
Mfano: Mtu alipata pesa leo, kesho ananunua magari matatu na kujitangaza kila mahali—watu husema "amekuwa limbukeni wa pesa."
Sasa all in all isijekuwa ni ishu ya mapenzi. Ulimbukeni katika mapenzi ni mbaya sana kama hautaweza kuudhibiti au kwenda nao sambamba hadi limbukeni aerevuke na kuachana nao.
Wapo wenza ambao unakutana nao na kuanzisha mahusiano wakiwa hawana exposure kabisa au ya kutosha. Ukigundua mtu wako ana masuala fulani ya ushamba au ujuaji usio na tija, au ndio mzee nyingi, usifurahie sana. Wakati utafika na kipofu ataona mwezi.
Kama mwenza wako hajawahi kunywa pombe maishani, na hana kizuizi cha unywaji, basi kuwa na tahadhari. Siku akiingia huko kumtoa sio rahisi.
Kama ulioa bikira 🫣 basi kuwa na tahadhari sana. Huyo hajawahi kuonja vya nje. Sijui utafanyaje aendelee kuwa wako pekee. Siku anagusa huko nje, omba aguswe na limbukeni pia. You know what I mean.
Kama ulioa binti wa kijijini kaishi nae kijijini. Ukimleta mjini ujipange. La, utamkumbuka Prof J.
Kama una mahusiano na fukara mjuaji basi kaa chonjo maana akizipata ujuaji unakuwa maradufu. Atatafuta vile alivokuwa akivitamani na kuvila kwa macho.
Kama unahudumia mwanachuo kwa mategemeo aje kuwa mkeo/mumeo una hali tete. Wao hawana ulimbukeni wa kujua au starehe. Wana ulimbukeni wa uhuru, na uhuru wenyewe ni wa kifedha. Siku wanashika hela zao kutokana na ajira zao, my friend...
Ulimbukeni uko mwingi sana. Na mwingine mtaongezea. Kubwa hapa ni kukubali hali ya huyo limbukeni hadi maji yamkauke magotini. Badi akomae. Hadi afikie saturation level. Yaani hadi akinai ndipo akili huanza kukaa sawa. Sasa wakati wa kusubiria limbukeni wako akinai vigeni, ni wazi yatapita mengi sana hapo kati. Ukiweza kuyahimili, basi we bingwa. We jasiri. We umekomaa. Ukishindwa pia haimaanishi una kasoro, bali kila mtu ana kiwango chake cha uvumilivu.
Ndio maana usishangae kuona watu wanatulizana na mishangazi au mibaba fulani. Hayo majitu nayo yamepita mapito ya kutosha hadi yakakinai na kuamua kutulia. Ndio maana nikasema awali kuwa ukiweza kumvumilia limbukeni wako, we umekomaa. Kwa wale wanaoachana na malimbukeni wao na kuambatana na hiyo mishangazi hawajataka tu kuwaza kuwa sbangazi nae alipita humo.
All in all ulimbukeni unaumiza