Ukiwa na familia kubwa kubali kuwa na wachagua vyakula

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Wenye familia wana mizigo mikubwa kwenye kulisha idadi ya watu waliomo ndani ya familia.

Kwa huku kwetu hii kitu inazidi kuongezeka kwenye familia ambazo unakuta umerundika kila aina ya watu.

Unakuta huyu sijui maharage hatumii, mwengine wali, nyama fulani, samaki ila kasoro kuku na n.k

Yaani kama una mzigo kama huu tegemea kupika chakula cha harusi maana kila mtu hupenda anacho kula kwa kisingizio cha vidonda, alipotoka, mazoea, aleji na n.k
 
Kama ni baba wa familia hakuna atakayepanga kwamba anakula nini ndani ya nyumba yako,usimnyime mtu chakula ni dhambi muhimu msisitize mkeo azingatie ratiba ya chakula kwa ajili ya familia yako yaani wewe wanao na yeye anayetaka kula tofauti na chakula kilichopo ndani ya ratiba ya familia ya siku hiyo akawashe moto jikoni huko ajipikie anachotaka na akanunue kwa hela yake siyo aingie store ajichotee.

That's it!!!
 
wenye familia wana mizigo mikubwa kwenye kulisha idadi ya watu waliomo ndani ya familia.

kwa huku kwetu hii kitu inazidi kuongezeka kwenye familia ambazo unakuta umerundika kila aina ya watu.

unakuta huyu sijui maharage hatumii,mwengine wali,nyama fulani,samaki ila kasoro kuku na n.k


yani kama unamzigo kama huu tegemea kupika chakula cha harusi maana kila mtu upenda anacho kula kwa kisingizio cha vidonda,alipotoka,mazoea,haleji na n.k
Kiuhalisia ndiyo maana Kwa advanced famili kila mlo mmoja wanapika Aina tofauti za vyakula ,ili anaetaka ugal dagaa atapata,wali mahaharage nae atapata Nk .lakini Kwa kuwa uchumi wetu ni WA kawaida hatuwezi kufanya hivyo nini kifanyike Sasa ,ukijiona katika familia Una watu wengi .jitahidi upike ugali,wali upande WA vyakula na mboga jitahidi iwe mboga za majani ,na maharagwe .afadhari
 
Sasa kwa uchumi wetu huu, baba Nani asiye na akili akubali machaguzi ya hovyo ya chakula,Cha kuhakikisha ni kuwa familia yako inakula vizuri hao wengine wasiotaka kula wakale hotelini huko labda Kama Kuna anayedhurika kwa kula chakula fulani hapo sawa atafikiriwa,Mambo ya kuchagua vyakula na kupika mtu apendacho ni kwa familia kidogo zenye uchumi mzuri...
 
Ndiyo ukubwa huo, Kuitwa KICHWA cha familia siyo kazi ya mchezo mchezo.

Kama una UWEZO wa kulisha CHAKULA wanacho hitaji fanya hivyo.

Wako wenye MZIO (ALLEGY) kweli na pia wako wenye MADONDA YA TUMBO kweli.

Na katika KUWALISHA hao wasiokula baadhi ya VYAKULA kwa MAGONJWA fulani ndipo MIBARAKA yako katika UTAFUTAJI inapatikana au KUONGEZEKA kupitia wao.
 
Tena inajulikana wazi kuwa asubuhi ni chai ya rangi na mihogo, mchana wali dagaa na usiku ni wali maharage!
Siku hizi uswahilini hiyo ratiba ya kula mara tatu wengi hawana
Huwa wanafanya hivi watoto wanapewa visambusa na vitumbua asubuhi ili wasilie
Wale wakubwa wanavuta mda mpaka saa sita au tano wanakula chakula ambacho kitawafikisha mpakani mwa mchana na usiku

Kwa maana hiyo wanakula mara mbili tu bwashee
 
Kuna mzee mmoja enzi za kikwete alikuwa mambo Safi kwako maana anafanya kazi sekta nyeti ,nilinda kwake mara kadhaa hizo draft za msosi kwake ni balaa.

Nyama kuna zilizoungwa ,zilizokaushwa ,chips ,ndizi ,ugali ,wali ,mboga za majani ,dagaa ,maharage ,matunda ,juice ,soda .

Vyote vinakuwa mezani na ni kwa kila siku,bia,wine zipo kwenye friji mda wote na makreti yapo tu store za bia na soda.

Magufuli alipoingia tu ,wakapunguza kazini ,aisee ni stress maana hakuwa na mishe zingine zaidi ya kazi ,hizo Kodi kufukuzana na wapangaji kila siku hata hela ya bia ni ishu
 
Siku hizi uswahilini hiyo ratiba ya kula mara tatu wengi hawana
Huwa wanafanya hivi watoto wanapewa visambusa na vitumbua asubuhi ili wasilie
Wale wakubwa wanavuta mda mpaka saa sita au tano wanakula chakula ambacho kitawafikisha mpakani mwa mchana na usiku

Kwa maana hiyo wanakula mara mbili tu bwashee
Hapo hakuna kubagua chakula!
 
Duh
Siku hizi uswahilini hiyo ratiba ya kula mara tatu wengi hawana
Huwa wanafanya hivi watoto wanapewa visambusa na vitumbua asubuhi ili wasilie
Wale wakubwa wanavuta mda mpaka saa sita au tano wanakula chakula ambacho kitawafikisha mpakani mwa mchana na usiku

Kwa maana hiyo wanakula mara mbili tu bwashee
 
Back
Top Bottom