Ukiwa mkweli utaishi kwa amani duniani

Ukiwa mkweli utaishi kwa amani duniani

Baba Kapompo

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
1,344
Reaction score
468
MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa bwana Harusi

BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii.
Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu.

MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa
 
Kumbe mke wako alishawishiwa na kanisa?
Ni mchungaji au padri alimshawishi?
Hiyo ndoa yako mkuu kama ilikuwa ya ushawishi wa kanisa nakupa muda utaleta mrejesho MMU
 
Kumbe mke wako alishawishiwa na kanisa?
Ni mchungaji au padri alimshawishi?
Hiyo ndoa yako mkuu kama ilikuwa ya ushawishi wa kanisa nakupa muda utaleta mrejesho MMU
Hapo umenena kweli kabisaa yaan
 
kujitambua kifikra nayo inasaidia sana kuliko utumwa wa fikra@all
 
Back
Top Bottom