Ukiukwaji Katiba, Tanzania tunafeli Wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Nchi si shamba la mtu. Nchi huendeshwa kwa kufuata katiba.

Inatia moyo majahili kama kina Alpha Conde wanapotiwa adabu kwa kukiuka katiba:

"Rais Alpha Conde alitaka kuvunja Katiba ya Nchi ili imruhusu kugombea kwa muhula 3 na bunge kumuongezea mshahara."

Sote hatupendi katiba ya nchi kuchezewa. Sote tungependa tabia hizi zikome. Lakini nani wa kumfunga paka kengele?

Wapo wanaomsubiri kwa dhati fulani achukue hatua, lakini si wao. Wana mawazo wakiyaita bora kabisa ambayo wangetaka fulani huyo ayachukue na hata hatua zipi afuate, lakini si wao.

Hao hao ni mafundi wa kuona makosa, kusema na kukosoa wakionyesha wapi fulani huyo anakwenda kombo. Wana ujasiri wa kubeza na hata kutukana wakiona fulani huyo anachelewa mno au hafanyi sawa sawa kulingana na matarajio yao.

Lolote baya likimkuta fulani huyo, hao hao hutokea na kumtupia lawama, kejeli na hata matusi kwa wasichoacha kukiona kuwa ni ujinga wake tu.

Hao hao kunako mafanikio huwa wako mstari wa mbele kwa ajili ya matunda yaliyo bora zaidi kuliko hata fulani yule aliyejitoa muhanga.

Hili ni rundo la "opportunists" wasio wa kuendekeza. Wanataka matokeo tu lakini si washiriki. Hawa wananunulika. Wako kimaslahi zaidi. Hawa ni mzigo na kimsingi hawafai.

Mjini wanajulikana kama wapenzi watazamaji.

Ni heri kuwekeza zaidi kwa wanachama ambao hata wanaojulikana kwa majina kama ni wetu, kuliko kwenye blanketi lenye kila Tom na Jerry ndani yake.

Hata kwa idadi ya wanachama wa Sipunda peke yake walio tayari kuyajaza magereza, mbona katiba ingeheshimiwa?

Mikutano ya vyama vya siasa na makongamano ni kwa mujibu katiba. Si kwa hisani ya mtu yeyote, chama au serikali.

Uvunjifu wa katiba haukubaliki.
 
Umenikumbusha hadithi moja ambapo panya walipochoka kutafunwa na paka waliamua kufanya kikao kutafuta mbinu za kumdhibiti paka asiendelee kuwatafuna,wakati wanaendelea na kikao chao mara paka huyoo kaibukia kwenye kikao chao,mara sauti ikasikika chwiichwii kwa vile tayari paka alikuwa ameshafanikiwa kumdaka panya mmoja,badala ya panya kutumia mbinu walizokuwa wanapanga kwenye kikao kumdhibiti paka aliyekuwa anawatafuna,wote walitimkia shimoni kujificha, kilichofuata ni mwenyekiti wao kuhahirisha kikao kwa kuchungulia kutoka ndani ya shimo aliko kuwa amejificha na kumwacha paka akifaidi kula msosi wa panya mpaka leo hii.

Ni kweli watanzania wengi tunahitaji mabadiliko ya katiba kwa kuwa hata hii katiba mbovu iliopo haifuatwi,kila mtu ana mawazo mazuri sana na mipango mizuri sana ambayo inaweza ikatufanya tukapata katiba nzuri sana yenye kuwadhibiti wenye mamlaka wasijifanyie wanavyotaka wenyewe. Lakini hatuna uthubutu wa kusimamia mawazo yetu mazuri na mipango yetu mizuri ambayo tukiitekereza inaweza ikatupelekea kupatikana kwa katiba mpya ambayo itamdhibiti mwenye mamlaka kujifanyia chochote kile anachotaka pasipokuwa na hofu yoyote huku akijua kuwa kukubali katiba mpya ni sawa na kukitia mchanga kitumbua chake.

Hata kama kuna atakayejitokeza kuwaongoza wenzake kudai katiba mpya kwa manufaa ya nchi, ni kweli wengi watamuunga mkono, pia watakuwa naye katika kutoa ushauri wao, mawazo yao mazuri na mipango yao mizuri lakini linapokuja suala la wenye mamlaka ambao wanaona kitumbua chao kinaenda kutiwa mchanga kuanza kumshughurikia yule anayewaongoza wenzake kupata katiba mpya, wote walio kuwa wanampa ushauri mzuri na kupanga mipango pamoja,wanakuwa hawaonekani tena, wanamwacha akihangaika peke yake utafikri kazi aliokuwa anaifanya ilikuwa yake pamoja na familia yake.

Kama wote kwa pamoja tungekuwa tunasimama kwa pamoja na kwa nguvu moja kusimamia kwa pamoja kupigania kile tunachoamini kuwa ndicho sahihi,tunakinukisha mitaani kupigania haki yetu tunayonyimwa,mbona tungekuwa tumeshafanikiwa tangu zamani.

Wewe fikria nchi imetumia gharama kubwa sana kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya na mamilioni ya watanzania katika maoni yao wakapendekeza uwepo wa katiba mpya,lakini maoni yote ya mamilioni ya watanzania yanakuja kuzimwa na kundi moja dogo tu,ambalo linafaidi keki ya taifa bila kujali gharama kubwa iliotumika kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni hayo, na kwamba maoni wanayokwenda kuyasambaratisha yametokana na mamilioni ya watanzania.
 
Mkuu heshima kwako. Umegonga mle mle kwenye mada. Kilichompata panya kukamatwa na mkutano kuahirishwa na mwenyekiti indefinitely tokea shimoni ndimo tulimo sisi.

Hali hii ni lazima ibadilike. Hali hii ni lazima ibadilike sasa.

Opportunists hatuna haja nao. Ni lazima tupeane makavu. Watu kama hao hatuwahitaji.

Kwa maoni yangu haipo haja ya elimu tena:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyehitaji haki, usawa, uhuru wala utawala wa kidemokrasia.

Kitabu cha Waamuzi 6:1 - 7:25 kiko wazi kwenye hali kama hizi. Kwa ufupi:

"Gideon was the son of Joash, from the Abiezrite clan in the tribe of Manasseh and lived in Ephra (Ophrah). As a leader of the Israelites, he won a decisive victory over a Midianite army despite a vast numerical disadvantage, leading a troop of 300 "valiant" men."

Heri tuwe wachache tuliodhamiria kuliko kuwa lukuki na watu mizigo.

Hatuna haja ya kuendelea kupambana na kuelimisha watu indefinitely.

Watu wetu katika vyama tunatosha sana wengine tutakutana huko huko mbele kwa mbele.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Bado kidogo! Kuwa na subira! Kutakucha muda si mrefu.

Maneno kuntu kabisa haya.

Hata hivyo suala la kutoa elimu japo elimu haina mwisho, kwa hakika sasa limetosha.

Tuwapurure ma opportunists wote.

Hayupo mtanzania yeyote mwenye akili timamu asiyejua hadi sasa kuwa anahitaji kuhakikishiwa usawa, haki, uhuru na utawala wa kidemokrasia ni muhimu ili kuwa na maisha bora.

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Ni heri tuwe wachache tuliodhamiria. Tuwaache ma opportunists kubakia majumbani salamasi shida.

Haina taabu wadada kubakia majumbani. Lakini midume mizima kuwa mi opportunists na kubakia majumbani?!

Ni heri kwa wadada na wamama kubakia maana hao tutawaomba watuangalizie wanetu majumbani.

Kwenye kitabu cha Waamuzi 6:1 - 7:25 Kwa ufupi kupo hivi:

"Gideon was the son of Joash, from the Abiezrite clan in the tribe of Manasseh and lived in Ephra (Ophrah). As a leader of the Israelites, he won a decisive victory over a Midianite army despite a vast numerical disadvantage, leading a troop of 300 "valiant" men."

Tuko vizuri. Kwa ku focus kwenye wanachama wetu tu hii ngoma tunaimudu.

Hatuhitaji watu mizigo. Na waufyate tu kwa sababu hatuwahitaji.
 
watanzania wenyew hatueleweki tunatafuta nini

Kauli hii si sahihi. Kauli hii inaweza kuhalalishwa kama umekutana na watanzania wote wakakwambia hivyo.

Tuwaweke watanzania unaowaongelea pembeni.

Vipi kuhusu wewe au hawa kina fazili na Jeh ninaoona vibendera vyao wakikuunga mkono? Nanyi pia kama watanzania hamjui mnataka nini?

Hiiiiii bagosha!
 
Wale wote ambao tunapenda kuiona nchi yetu ikiongozwa kwa HAKI, UHURU na USAWA wa raia, vyombo vya habari na vyama vya siasa kupitia Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi tuendelee KUPAMBANA kunakaribia kucha. Na dalili kwamba mapambano yetu yanafanikiwa ni hii kauli ya leo ya mhuni muthungi. Tusichoke kupambana na hatuna haja ya kuunda jeshi wala kubeba silaha na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu wa ndugu kwa ndugu au rafiki kwa rafiki au jamaa kwa jamaa tukayarudia yale ya 1994 ya TUTSI na HUTU kule Rwanda. Hakuna sababu ya hilo kutokea.
Alutta!!! ✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾
 
Kwa Afrika nchi zinazofuata katiba Ni chache Sana...

Nchi zisizofuata katiba zinaendeshwa kama mashamba ya bibi. Hizo aliziita shit hole countries bwana Trump. Hizi ziko sehemu zingine duniani ila Afrika ndiyo kwao.

Wapongezwe Guinea na hasa bwana Mamady Doumbouya kwa kututoa kimasomaso kama waafrika. Kwa hakika wameonyesha kwa vitendo kuwa panapo nia nchi hii pia itatawaliwa kwa mujibu wa katiba.
 
Wale wote ambao tunapenda kuiona nchi yetu ikiongozwa kwa HAKI, UHURU na USAWA wa raia, vyombo vya habari na vyama vya siasa kupitia Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi tuendelee KUPAMBANA kunakaribia kucha. Na dalili kwamba mapambano yetu yanafanikiwa ni hii kauli ya leo ya mhuni muthungi. Tusichoke kupambana na hatuna haja ya kuunda jeshi wala kubeba silaha na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu wa ndugu kwa ndugu au rafiki kwa rafiki au jamaa kwa jamaa tukayarudia yale ya 1994 ya TUTSI na HUTU kule Rwanda. Hakuna sababu ya hilo kutokea.
Alutta!!! ✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾

Hatuhitaji kubeba silaha:

"Wingi wetu na utayari wetu kuyajaza magereza yao ni silaha na ngao kubwa mno dhidi yao na silaha zote walizo nazo."

Tuko katika njia sahihi na ushindi ni dhahiri na ushindi ni karibu.
 
I agree...

Tunatafuta tiba, swali ni utayari wa kutafuta tiba na kulipa gharama kupata tiba upo?

Nyuzi mbili hizi mmoja ukiwa huu wenye mada hii:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

zinajueleza kwa ufasaha:

1. Elimu haina mwisho, ila kuhusu katiba mpya hadi hapa inatosha.
2. Hakuna haja ya kupoteza muda zaidi na opportunists.
3. Ni heri kuwekeza kwa wanachama wakereketwa wachache wenye kudhamiria kuliko kuhangaika na watu mizigo wasio na manufaa.
4. Mapambano yetu yatakuwa ya amani pasipo na kubeba silaha au kumwaga damu.
5. Wingi wetu na utayari wetu kuyajaza magereza yao ndiyo iliyo silaha na ngao yetu kuu.

Waamuzi 6:1 - 7:25 inawaangazia opportunists kama tulio nao pasipo na shaka yoyote. Kwa ufupi inasema hivi:

"Gideon was the son of Joash, from the Abiezrite clan in the tribe of Manasseh and lived in Ephra (Ophrah). As a leader of the Israelites, he won a decisive victory over a Midianite army despite a vast numerical disadvantage, leading a troop of 300 "valiant" men."

Tuko hatua ya mwisho ya kuweka mambo sawa sisi na washirika wetu.
 
Watu wachache wanajitoa kwa ajili ya wengi kila siku, wanaumizwa, wanatekwa, wanabambikiwa kesi, yote kwa ajili yetu, sijui lini nasi tutaanza kuwatetea hao waliojitoa kwa ajili yetu.

Nimekaa nikajiuliza, ingekuwa nchi zinazojielewa hii kesi ya Mbowe serikali wangerudi wenyewe kwa Mbowe kumuomba awatulize wanachama wake, huu upuuzi anaofanya jaji hauvumiliki.

Mpaka kufikia hapa Mbowe kaonewa mara mbili (kubambikiwa kesi, na kunyimwa ushindi wa kesi leo), lakini sisi wengine tupo tu, hatuamki, ndio maana jamaa wanafanya mambo ya ajabu kuvunja sheria na mengine kwasababu wanajua hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kuandika huku.

Narudia, laiti kama tungekuwa nchi zinazojielewa, leo CCM na serikali yake wangekuwa wanampigia magoti Mbowe kumuomba aitulize nchi.
 
Mkuu hatuko vibaya. Ni kweli lazima tukiri tulidhani sote tunaweza kujitoa kupigania kesho bora ya watoto wa wajukuu wetu.

We learnt it the hard way. Si haba leo tuko hapa:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Ni wazi kuwa leo tunaujua ukweli huu:

1. Elimu haina mwisho, ila kuhusu katiba mpya hadi hapa inatosha.
2. Hakuna haja ya kupoteza muda zaidi na ma opportunists.
3. Ni heri kuwekeza zaidi kwa wanachama wakereketwa wachache wenye kudhamiria kuliko kuhangaika na watu mizigo wasio na manufaa.
4. Mapambano yetu yatakuwa ya amani pasipo na kubeba silaha au kumwaga damu.
5. Wingi wetu na utayari wetu kuyajaza magereza yao ndiyo iliyo silaha na ngao yetu kuu.

Waamuzi 6:1 - 7:25 inawaangazia opportunists kama tulio nao pasipo kuwa na shaka yoyote. Kwa ufupi inasema hivi:

"Gideon was the son of Joash, from the Abiezrite clan in the tribe of Manasseh and lived in Ephra (Ophrah). As a leader of the Israelites, he won a decisive victory over a Midianite army despite a vast numerical disadvantage, leading a troop of 300 "valiant" men."

Tuko hatua ya mwisho ya kuweka mambo sawa sisi na washirika wetu.

Hatuna cha kuficha. Si mbaya wakajua tulipo na kinachokuja.

Mapambano yetu kudai haki, usawa, uhuru na utawala wa kidemokrasia ni mapambano matakatifu.

Pamoja na yote Mh. Mbowe anaendelea kuwa hai mawazoni mwetu. Ni suala la muda tu. Tutakuwa naye Segerea kwa maelfu.

Nadhani tuko vizuri.
 
Hatua ya kwanza ni kujua kwamba unaumwa.... hatua ya pili ni kujua ugonjwa.... tatu ni kutafuta tiba

Tupo hatua ya kwanza...
ugonjwa tunaujua dawa inafahamika tatzo tunaogopa kuchoma sindano
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom