ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,347
Habari za jioni wakuu,
Jaribu kumtazama mwanamke ama mwanamume uliyenae kwa umakini. Mtizame anavyohangaika sababu ya mapenzi mazito aliyonayo juu yako.
Muangalie anapoamka asubuhi akikiacha kitanda tena akiwa bado na usingizi mzito. Lakini kwa kuitambua thamani yako na mahitaji muhimu katika maisha anasahau hilo la usingozi na kuliacha shuka tayari kwa mapambano yakuingiza chochote kitu.
Anatoka na kukuacha ukiwa kitandani ukivuta shuka.Anaingia mihangaikoni. Huko anakutana na maneno ya masimango kutoka kwa bosi na wafanyakazi wenzie.
Wakati mwingine anakumbana na udhalilishaji wa kijinsia hata kutakiwa na mabosi wake,lakini kwa kutambua thamani yako anasimamia maamuzi yake na kukataa kutii kile alichoombwa.
Sio kwamba alifanya hivyo kwa kuwa hana shida la hasha aliitambua thamani yako na kuliweka penzi lako mbele kulikokazi yake.
Baada ya kupambana na hayo yote mwanaume/mwanamke anaporudi nyumbani huhitaji faraja.Faraja kutoka kwa familia yake hasa mpenzi/mume/mke. Hahitaji kukasirishwa na kufokewa.
Unapotengeneza mipasuko katika mahusiano yako, tambua unauandaa moshi ambao siku moto ukiwaka utashindwa kuuzima na kwa kutambua hilo utakuwa umepoteza kila kilichounguzwa na moto Huo.Ni wajibu wetu sote kuishi kwa kupendana, kulindana nakuheshimiana.
Kila mwenye kuishi na mwenzake amuonyeshe ukweli kutoka moyoni kuwa anampenda na kamwe hatoweza kumuacha.Faraja pekee yenye thamani ni ile unayopewa na mtu anayekupenda na umpendae.
TUACHE KUUDHARAU MOSHI UNAOFUKA KWA KUWA UKIWAKA UTAUNGUZA KILA KITU TULICHONACHO
NA HATA MTAKAPOHITAJI KUJENGA TENA HAUTOKUWA IMARA TENA KAMA MWANZO.
ZINGATIA HILO