Fahamu namna ya kuuzima Moto unaotokana na shoti ya umeme

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
FAHAMU NAMNA YA KUZIMA MOTO WA SHOTI YA UMEME

Habari wadau,
Happy end of the month (January woyoooo),na happy new year kwa familia yooooote ya Home of Great Thinkers (HGT).

Baada ya salaam twende kwenye maada yetu,

FAHAMU NAMNA YA KUZIMA MOTO WA SHOTI YA UMEME
Kama tunavyojua kuwa nishati ya umeme Ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku,ila Mara nyingine nishati hii huweza kuleta hasara ya mali,afya na maisha.

Ukweli umeme ni rafiki sana ila ni adui anae tabasamu pia,watu huzubaishwa na mazuri yake na kusahau upande wake ule mwingine hivyo Mara nyingine huuchukulia poa umeme.

Anyway siku zote usiuzoee umeme,upe heshima yake.

Ili kuiweka jamii yako salama hakikisha unafuata ushauri huu kwa bahati mbaya pale umeme unapo sababisha moto.

1. Nenda Mara moja kazime Circuit breaker yako,au Distribution yako,pale unapohisi harufu ya kitu kuungua,mfano waya,plastiki au nguo (ila sio nyama au maharage....hahaha natania).

Hii itakupa muda wa kujiridhisha kujua harufu inatokea wapi,Kama utapaona na ukajua sababu ya moto sio umeme,unaweza kuwasha umeme wako,ila Kama ukijua sababu Ni umeme,hakikisha unamuita mtaalamu wako wa umeme Mara moja aje atatue tatizo.

Pia zima umeme pale utakapo ona moshi au moto ukiwaka katika eneo lisilotakiwa kuwaka Moto au kutoa Moshi.

2.Kama moto umetokea katika kifaa cha umeme au waya hakikisha unaondoa Chanzo cha hewa ya oxygen,kwa kukifunika Chanzo Cha moto kwa kutumia mchanga.

Hivyo hakikisha una ndoo ya mchanga ndani mwako,hakikisha unahifadhi ndoo hiyo hasa katika corridor,au mahali ambapo kila mtu anafikia,ili wakati wa Moto wa umeme iwe rahisi kuifikia.

3.Kama una fire extinguisher ambayo inazima Moto "daraja C" itumie kuzima moto huo,hakikisha inazima daraja Hilo la moto Soma katika maelezo yake,vinginevyo unaweza leta balaa zaidi,kwako mwenyewe au ukasababisha moto kuongezeka.

4.Pia unaweza kuuzima kwa kutumia sodium bicarbonate changanya na baking soda Kama Moto bado ni mdogo.

VITU AMBAVYO HUTAKIWI KUFANYA WAKATI WA MOTO WA SHOTI YA UMEME.

1.Usizime Moto huo kwa kutumia maji,kwenye Moto wa umeme maji hayauzimi,bali yatauongeza Moto kwasababu maji Ni kipitisho kizuri Cha umeme hivyo yanaweza kuongeza shoti ya umeme kwa waya kugusana zaidi.

Lakini pia maji yanaweza yakatiririka yakakutana na mitungi ya gesi,na maji hayo yakiwa yemegusana na waya za umeme kitakacho tokea ni milipuko.

Pia maji hayafai kwasababu unavyozima Moto wa umeme maji yanagusana na waya na yanaweza kugusana na mwili wako,kwa hatua hiyo umeme utakuua Mara moja.

2.Usichomoe au kugusa waya uliokatika,au kutoa cheche wakati wa shoti ya umeme,Ni hatari zaidi kaa mbali kabisa.

HATUA ZA MUHIMU KUJIOKOA.

1.Kama umeona Moto Ni mkubwa au unazidi kua mkubwa,haraka jiokoe wewe na familia yako kwanza.

Usihangaike kuokoa Mali,au vitu vya thamani,sababu Moto huondoa hewa ya oxygen,hivyo kuendelea kukaa eneo Hilo Ni hatari kwa maisha yako.

2. Epuka kutaka kuwa shujaa katika kupambana na Moto,ambao tayari unaona umekuzidi nguvu,toka nje Mara moja na usiingie Hadi zimamoto watakapo fika.

3.Wasiliana na zimamoto haraka.

TAHADHARI ZA KUCHUKUA KUEPUKA SHOTI YA UMEME.

1.Mwite mtaalamu wa umeme akague nyumba yako Mara kwa Mara.

2.Epuka kuzidisha mzigo wa vifaa vya umeme nje ya uwezo wa waya.

3.Hakikisha vilinda saketi vinafanya kazi vizuri wakati wote.Hapa mtaalamu wa umeme atakuja kukagua Kama vilinda saketi vyako viko salama kwa kuvipima na kutengeneza shoti bandia kuona kama vifaa hivyo vinajizima.

Na Kama havipo Sawa vibadilishe.

4.Kuwa makini na ufungaji wa vifaa feki.

5.Kila ukisikia harufu ya kitu kuungua,mfano plastiki,nguo au waya,zima umeme maramoja na umuite mtaalamu wa umeme kufatilia.

5.Jitahidi kuwa na fire extinguisher inayozima Moto Aina zote yaani A,B na C

6.Jitahidi uwe na ndoo ya mchanga ndani mwako,iweke sehemu ambayo ni rahisi kuifikia.

Asanteni kwa muda wenu (karibuni kwa huduma za kisasa za wirering za umeme)

(Nasikia nyumba nyingi mara nyingi zinaungua kwa moto siku ya jumanne haaa..haa...Sina uhakika lakini nimesikia tu)

Eng.Transistor).
 
Ahsante sana kwa elimu yako ya umeme

Uendelee kubarikiwa kwa kusambaza maarifa ya taaluma yako kwa sisi wakina mitomingi
 
Asante sana.
Naomba ushauri na ufafanuzi wa aina za vizima moto.
Yaani hizo A, B na C.
 
Asante sana.
Naomba ushauri na ufafanuzi wa aina za vizima moto.
Yaani hizo A, B na C.
Class A - Moto wa mbao, karatasi au nguo.
Class B - mafuta ya petrol, diesel au oils.
Class C - Moto wa gesi,au material yatoayo gesi ya kulipuka,Moto unaoweza jiongeza
Class D - vyuma vya moto.
Class E - Moto wa vifaa vya umeme,simu,tv,radio etc.
 
Back
Top Bottom