"Ukitoka tu nakumeza"

Mtanzanika

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
2,389
1,131
Jamaa alipokua akitoka nyumbani kwake asubuhi, alistushwa na sauti iliyokua inatoka nyuma ya nyumba yake..alisikia sauti nzito ikianza kwa kukoroma “Mhnnnnn……Ukitoka tu nakumeza…..Mhnnnnn….Ukitoka tu nakumeza” sauti ilikua ikijirudia rudia (nonstop).

Alipatwa na hofu na hivyo kabla hajafungua geti alipiga simu kwa majirani kuomba msaada. Si muda mrefu majirani kadhaa wenye silaha mbali mbali walifika kumnusuru jirani mwenzao. Ile sauti ilikua inaendelea kusikika. Kwa umakini huku wakinyata, walijigawa makundi mawili kuizunguka nyumba ili kuona kitu gani kinataka kummeza jirani yao.

Laa haulaaa!!!kumbe nyuma kulikua na Mwendawazimu akisema na mafua yaliyokua yakining’inia puani mwake kwa kuyatahadharisha……“Mhnnnnn……Ukitoka tu nakumeza”
 
uwii my apetite! jamani mambo gani haya lunch hour lol!
 
Back
Top Bottom