Ukitoa kauli hii usitegemee msaada kutoka kwangu

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,707
71,003
Habari wakuu,

Nina ndugu yangu mmoja alipatwa na tatizo la mtoto wake kupata ajali na ikabidi alazwe na kufanyiwa upasuaji. Kwa bahati mbaya alikuwa hana hela, hivyo akaamua kunipigia simu ili nimsaidie; nikwambia hapa nipo njiani naenda kulipa ada ya watoto wa sekondari wamefukuzwa shule sababu ya ada ya shule, nikitoka shuleni kulipa ada nitajaribu kukopa kwa marafiki zangu, akasema nitumie hiyo hela halafu ada ndiyo ukakope, nilichukia nikafuta na mpango wa kumsaidia.

Naombeni mawazo yenu kuhusu uamuzi niliochukua.
 
Ilitosha kumwambia huna kwa muda huo ila baadae utaangalia na kukopa kwa marafiki zako Kama ukipata utamsaidia rahisi sana hukukuwa na haja ya kumwambia kuwa unaenda kulipa ada
Kwa hiyo mimi ndiyo nilikosea kusema ukweli
 
Ningejiuliza:
Ajali ya mtoto ilikua kubwa kwa kiwango kipi?

Inatishia uhai? Hapana, kama ni hapana basi huyu ni mbinafsi. Nitamkopea ila robo ya kiwango alichotaka.

Inatishia uhai? Ndiyo, basi alichoongea ni upendo wa mzazi kwa mtoto hivyo ana haki ya alichotamka. Ningejibu kistaarabu kua 'Nakuhakikishia tutafanikisha, usijali' kisha ningeendelea na mchakato.

NB: Ila kama inatishia uhai, na unajua na ukamkatia simu chief wewe ndiye mbinafsi kwa hapo. Sijajua shule ya mwanao ni ipi as shule zinafungwa Ijumaa hii so kuwafukuza kisa ada ingekua ni kumpiga chura teke kwa kuwaanzishia likizo mapema.
 
Habari wakuu,

Nina ndugu yangu mmoja alipatwa na tatizo la mtoto wake kupata ajali na ikabidi alazwe na kufanyiwa upasuaji, kwa bahati mbaya alikuwa hana hela hivyo akaamua kunipigia simu ili nimsaidie, nikwambia hapa nipo njiani naenda kulipa ada ya watoto wa secondary wamefukuzwa shule sababu ya ada ya shule, nikitoka shuleni kulipa ada nitajaribu kukopa kwa marafiki zangu, akasema nitumie hiyo hela halafu ada ndiyo ukakope, nilichukia nikafuta na mpango wa kumsaidia.

Naombeni mawazo yenu kuhusu uamuzi niliochukua.
Hao watoto wako huko shuleni huwa wanafaulu?!

Jifunze kumpenda jirani yako kama nafsi yako!
 
Habari wakuu,

Nina ndugu yangu mmoja alipatwa na tatizo la mtoto wake kupata ajali na ikabidi alazwe na kufanyiwa upasuaji, kwa bahati mbaya alikuwa hana hela hivyo akaamua kunipigia simu ili nimsaidie, nikwambia hapa nipo njiani naenda kulipa ada ya watoto wa secondary wamefukuzwa shule sababu ya ada ya shule, nikitoka shuleni kulipa ada nitajaribu kukopa kwa marafiki zangu, akasema nitumie hiyo hela halafu ada ndiyo ukakope, nilichukia nikafuta na mpango wa kumsaidia.

Naombeni mawazo yenu kuhusu uamuzi niliochukua.
Mtu anafanyiwa upasuaji na yuko hali mbaya na yule aliye stopishwa shule hapo ninani mwenye umuhimu mwanzo kua na hekima na busara mm ningalimsaidia yule kule hospital kwanza
 
Na wewe jifunze kumwambia mtu straight sina pesa labda nikipata nitakupa ,badala ya kupindapinda kona nyingi ..unajua ukweli unahuma lakini unapoa haraka maana unakubaliana na hali yoyote
 
Mtu anafanyiwa upasuaji na yuko hali mbaya na yule aliye stopishwa shule hapo ninani mwenye umuhimu mwanzo kua na hekima na busara mm ningalimsaidia yule kule hospital kwanza
Mwenye umuhimu ni watoto wangu, anatakiwa kuwa na hela ya dharula au angekopa kwa marafiki zake
 
Mwenye mtoto kukuambia umpatie ada nawewe ukakope Basi jua mtoto wake alishikwa Sana..ungemsaidia tu mengine yangefuata baadae..
Ningemsaidia halafu watoto wangu warudi nyumbani
 
Kweli ada ya watoto ni muhimu hasa kwakuwa ni jukumu lako lakini kwa wakati huo ungejaribu kuvaa viatu vyake je uhai au shule ipi muhimu? ,uhai ukipotea ndo basi tena lakin shule ipo chini ya uwezo wetu, akifa huyo mtoto leo hata kama kukosekana kwa hela siyo sababu kiukweli utabeba lawama na ingekuwa mtu kama mm hata udungu unaisha kabisa
 
Hujanielewa, wewe badala ya kutoa maoni ungefanya nini unaanza kuni define mimi, ungekuwa wewe ungerudi na watoto nyumbani au ungelipa ada

1. Haukuwa sahihi kulingana na maamuzi yako endapo tu:-

A) mgonjwa akiwa kwenye hatari ya kupoteza uhai.

Endapo angekuwa kwenye hatari hiyo, ulipaswa kumsaidia ilikuokoa maisha baada ya hapo unakopa kulipia watoto. Uhai haupatikani popote akifa mkopo/msaada hautakuwa na maana itakuwa umechelewa.

Kwa upande wa watoto wako
- shule ipo
- watoto wapo
- utalipa ndani ya siku 1 au 2 haitawaathili sana

B. Endapo mgonjwa hayupo kwenye habari yoyote kupoteza uhai, ungeweza kulipia watoto wako kisha ukanipa
- hospital ipo
- mgonjwa yupo
- uhai utakuwepo

2. Ulipaniki. Mimi iliwahikunitokea nilifanya maamuzi ya haraka kwa mtu alienililia kwenye simu akihitaji msaada kwavile nilikuwa na pressure za ofisini....meetings na mambo kibao nikampuuza alipolazimisha nikazima simu.

Kesho asubuhi nikaletewa taarifa mgonjwa amefariki kwa kucheleweshwa hospital
Mpaka leo naumia sana nikikumbuka maana ningeweza kabisa kumsaidia. Bora angefariki nikiwa nimesaidia kufika hospital kwa muda

Hitimisho
Tujitahidi sana kusikiliza wenzentu kunawakati wanachanganyikiwa kwa kuzidiwa na mzigo wa tatizo, anakuwa haambiliki, hatuliziki na haelewi maana kazidiwa kichwani sio yeye Bali akili zimeparaganyika.
- sikiliza kwa makini
- usijibu ukiwa umepaniki
- Jipe muda japo saa moja, tulia tafakali
- toa jibu sahihi baada yakufikilia nakutafakali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom