Ukitegemee kupata connection za Wanadamu

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Katika jamii Yetu ni kweli sio rahisi ukafanikiwa pasipo kupata MTU WA kukushika mkono, lakini ni kosa kubwa Sana la kuweka tumaini Kwa Mwanadamu

Ni kweli tunategemeana na tunapaswa kuishi Kwa kueshimiana na kumwona mwenzako ni Bora kama wewe na vitu kama hivyo

Lakini katika Mambo yote tusiweke tumaini katika watu, biblia imetukataza, amelaaniwa MTU Yule ambaye amemfanya mwandamamu kuwa kinga yake, kumtegemea mwanadamu ni kujiweka kitanzini

Neno kulaaniwa ni Kinyume cha baraka na neno baraka ni kuweka kitu, Mungu amewekeza ndani Yetu kitu cha kutusaidia tuweze kufika mahali alipotukusidia

Unaweza kuwalaumu watu kwamba awakusaidia, wala kujali mahali unapopitia na kila Aina ya neno

Kuna watu wengine wamekosana na ndugu zao Kwa sababu wanaamini wananafasi za kuwasaidia , ni kweli wanasehemu katika Maisha yako lakini kama hawajafanya ?

Kuna wakati unatafuta connection na watu ukitegemea watu kukufikisha mahali flani ambapo unatamani kufika , na wengine kupitia kutafufa connection wamefarakana Mungu

Usijekutafufa connection Kwa kupoteza mahusiano yako na Mungu , ni Bora upoteze connection lakini mahusiano yako na Mungu yako vizuri, mahusiano yako na Mungu ni muhimu Sana kuliko connection

Umewai kusoma habari za Yusufu , Yusufu akiwa Kwa potifa akakutana na connection ya mke wa potifa, Ila Yusufu aliona ni njia ya kuelekea upotevuni sio kila connection inakufikisha Kule Mungu alikukukusudia zingine zinakupelekea mautini

Yule mkuu WA wanywesha alipomsahau Yusufu ,Yusufu hakuangaika na mkuu WA gereza kuomba kuonana naye kwani alijua ambaye aliyempa connection ya kukutana na mkuu WA wanyweshaji ndiye atakaye mfikisha Kwa Farao.

Ile kwamba watu wako WA karibu wamekataa kukusaidia kufikia ndoto yako sio kwamba hautafikia ndoto yako, enedele a kutembea na Bwana , endelea kumwamini Bwana kwamba hiko siku atakukutanisha na watu ambao watakufanikisha kwenye ndoto yako

Hacha kuwalilia wanadamu , Millie Mungu ata kama wamekuacha Mungu hata kucha weka tumaini kwa Mungu anayekupa connection Kwa Jina la Yesu Mungu atakufungulie mlango WA ndoto yako , Amen
 
Back
Top Bottom