Ukitaka ukosane na rafiki omba akukopeshe fedha...

Ukitaka ukosane na rafiki omba akukopeshe fedha...

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,346
Reaction score
56,072
Ukitaka ukosane na rafiki omba akukopeshe fedha.

Siku mbili tatu zilizopita nilipata changamoto kidogo za kiuchumi kutokana na mambo ya ujenzi, wajuzi wanasema zege halilali.

Nikajishauri nikaona ngoja niombe fedha ya dharura kwa marafiki zangu. Majadiliano yakawa hivi:-

Mimi: Mambo vipi mkuu? Naomba unisaidie kiasi fulani cha dharura by Alhamisi nitakurudishia hata kwa riba.
Rafiki 1: Sawa haina shida kaka nitakucheki baadaye
Baada ya hapo kimya, ukimpigia simu hapokei.

Rafiki 2: Ok nitakupatia kesho
Kesho inafika kimya, ukimpigia simu hapokei

Rafiki 3: Siko vizuri kiuchumi, biashara zimesimama kaka
Bora huyu alikuwa muwazi na nilimuelewa

Rafiki 4 : Siko vizuri kaka, nitakupatia nusu yake
Mimi: Nashukuru nilikuwa naitaji full

Kutokana na hali hiyo, nilichoweza kujifunza ili usikosane na rafiki yako inabidi mahusiano yenu yasihusu mambo ya fedha.
 
Equation x, Usimkope rafiki yako mwambie naomba kiasi fulani sio kwa mkopo.

Na wala usimkopeshe rafiki yako inabidi umpe tu usimdai na kama huna sema huna.

Na hata Ndugu akikuomba umkopeshe muambie sina hela labda nikupe kiasi kidogo ufabye na mipango mingine upate kujazilia.

Na hata wewe ndugu Muombe hela usimkope.
Mimi kama unanikopa unaniambia utanirudishia kesho si bora usubiri hiyo kesho tu utumie pesa yako.omba bwana.

Sasa mfano wewe mtoa mada sijui kwa nini hukusubiri hiyo alhamisi tu ukatumia pesa yako.

Mkopo wa uhakika uende kwa watu ambao wapo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Saikolojia zetu sisi watu hatupendi kuombwa Mungu ndo hupenda watu wakimuomba.kwa hyo hakuna mtu atafurahi ukienda kumuomba kitu.

Fuata hii principle kisha rudi hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
safuher,
Kweli mkuu,ilikuwa ni lazima niombe anikopeshe sababu ilikuwa kiasi kikubwa kidogo.Na ilikuwa ni dharura tu kwa sababu nilishatumia 15m tayari kwa ajili ya kumwaga jamvi
 
Back
Top Bottom