Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,622
Reaction score
10,247
Miaka flani niko Bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nikaongea nae kuhusu kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nikatua Jackson Heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mimi kutafuta kazi, Marekani kazi zipo ila sasa kule ukisikia kazi ni kazini kweli full supervision unafanya kazi kwa muda wa saa 10 mpaka 12, hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyewe unalipwa kwa saa, kwa hiyo lazima ukomaee ila kazi tu zipo.

Baada ya muda kudunduliza hela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa Sandy Springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa kawaida, kila kitu ni hela yaani ukisikia capitalism kule ndo inakuwa practice

Suala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokuwa makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi TZ sababu za kifamilia.

Maisha ya Marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au una kipaji kitu ambacho kwa Watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao.

Kwenda Marekani hivihivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata hela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda Marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, uwe competent, hivihivi sikushauri hata kidogo.

California, New York, Illinois, Massachusetts na Washington hayo ni majimbo ya kuyaepuka, kodi na gharama za maisha ziko juu ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivyomiss Marekani ni exposure ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kuna kikampuni nitaenda kukifungua deleware kama domestic company, baadae Virginia na Texas kama foreign company.
 
Sawa ndugu umetufahamisha ulikuwa
M
Milion na ushee in perspective ya bongo,ila kwa huko US hiyo pesa ni ndogo sana.labda uwe mvivu tu wa kupiga kazi.
Marekani kazi sio ishu ziko nyingi tatizo ni gharama za maisha na kipato unachokipata haviendani ndo changamoto kubwa
 
Back
Top Bottom