Ukitaka kuwa mbaya, dai chako!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Mie jamani huyu shoga yangu wala simwelewi. Mwanzoni mwa mwezi ulopita, alikuja kunazima vidani vyangu vya dhahabu ili kuhudhuria pamvu ya dada yake. Siku kadhaa baadae akaja kunambia kwamba, vidani vyangu vimepotea, lakini akaahidi kunilipa. Sasa naona karibu mwezi wesha, mwenzangu kimya! Juzi nimemkumbusha, imekuwa nongwa. Anapita kila mtaa kuntangaza ubaya.

Jamani wenzangu hebu nambieni, ubaya wangu uwapi? Yaani kudai changu ndiyo niwe mbaya! Vidani vyangu, mwenyewe nimepewa na bibi yangu Al Marhum Bi Kijakazi, leo hii huyu hayawani asiye na haya anletea za kuleta! Mwenyewe nilikuwa na mtoko weekend hii na nilitaka nikaoshee huko kwenye mtoko, lakini huyu majununi ananipa majibu ya kifedhuli. Ama kweli, wafadhilaka wapundaka, heri kumfadhili mbuzi, kuliko binadamu mwenye maudhi!

Eti wana JF wenzangu, nimfanye nini huyu baradhuli?
 
baada ya matusi yote hayo, basi nakushauri umsamehe tu...
 
Zinduna, hilo liwe ni fundisho tosha kwako, usimuazime mtu kitu chako chochote "personal" iwe dhahabu, fedha, shaba, nguo, plastiki, mume. Kwa kifupi chochote kile. Ukitaka uwe na furaha ya maisha kama unaweza mpe kuliko kumuazima.

Na wala wewe usiazime cha mtu chochote kile, kama huna kaa utulie utafute chako.
 
kwani na wanaume pia huwa mnatuazimisha?
wewe ulishapata watu wakataka kukuazima gozi lako?
 
Zinduna, hilo liwe ni fundisho tosha kwako, usimuazime mtu kitu chako chochote "personal" iwe dhahabu, fedha, shaba, nguo, plastiki, mume. Kwa kifupi chochote kile. Ukitaka uwe na furaha ya maisha kama unaweza mpe kuliko kumuazima.

Na wala wewe usiazime cha mtu chochote kile, kama huna kaa utulie utafute chako.

Huh?? Mume?? Nae aazimishwa.... Umenshangaza Twin... kwa misingi ipi?? aaise, the imagination yenyewe imenitia hasira.....

@Zinduna.... Pole Dear, twajifunza tokana na Makosa....
 
komaa nae mpaka akupe chako hata siku moja don't give up kwenye mambo ya hela
mwambie ASILETE UPIMBI KWENYE SWALA LA SHILINGI
 
ama kweli fadhila,mfadhili mbuzi,unaweza ukapata mchuzi,lakini binadamu malipo yake ni maudhi. Source Jagwa Muzik vol 3. Nalog off
 
Zinduna, hilo liwe ni fundisho tosha kwako, usimuazime mtu kitu chako chochote "personal" iwe dhahabu, fedha, shaba, nguo, plastiki, mume. Kwa kifupi chochote kile. Ukitaka uwe na furaha ya maisha kama unaweza mpe kuliko kumuazima.

Na wala wewe usiazime cha mtu chochote kile, kama huna kaa utulie utafute chako.

Swaddakta, hapo umenena dada yangu, keshanifundisha huyo, wallahi hata leso simwazimi tena hata akinambia nina ndweo!
 
Huh?? Mume?? Nae aazimishwa.... Umenshangaza Twin... kwa misingi ipi?? aaise, the imagination yenyewe imenitia hasira.....

@Zinduna.... Pole Dear, twajifunza tokana na Makosa....

Da, AshaDii, ahsante mwaya, wajua vidani vyenyewe vya urithi ndo maana roho yaniuma mwenzio
 
Da Zinduna nina uhakika hapa watu wengi hawataelewa uliposema "leso" =Khanga lakini "ndweo" hata mimi umeniacha na kukaa kwangu kote Unguja miaka 3
 
Nimekuelewa kabisa dear... Kuna vitu ambavo kwa mwingine huweza onekana kidogo saana but mhusika pekee ndio akaelewa hasa uthamani wa hicho kitu. Hivo nimekupata kabisa.... Hata hivo Zinduna, shoga daima sio mtu ambae yatakiwa ujibwage mpaka wajisahau, for mara nyingi mie nimeona wadada wenzangu walalamika mambo ya mashoga... It is beta uwe na rafiki ndio BUT Kue na mipaka fulani ambayo haitakiwi kuvukwa, for ikivukwa hio mipaka hufanya wee ushindwe control Certain things zikitokea kama hii.... Narudia; Pole saana.
 
ndo hivyo mashoga walivyo.....ila komaa nae....mwizi tu huyo.....hajapoteza wala nini....vipo anavyo....ila Zindu....pamvu na ndweo maana yake ni nini.....?
 
Da Zinduna nina uhakika hapa watu wengi hawataelewa uliposema "leso" =Khanga lakini "ndweo" hata mimi umeniacha na kukaa kwangu kote Unguja miaka 3

Ndweo maana yake ni Kiburi au Majivuno kwa Kingazija.
Mnisamehe, na kama lugha yangu ni ngumu naomba muwe mnaomba ufafanuzi kama alivyofanya mwenzenu.
 
Back
Top Bottom