Za ndaani na za chini chini nimesikia kuwa kumbe Shida ni Urais Mungu na Uenyekiti wa CCM ulivyo na unprecedented power, Wabunge wengi wa CCM na viongozi kutoka bara hawapendi suala la kutawaliwa na Rais kutoka Zanzibar, nchi yenye watu wasiofika milioni 2,.
Sasa inasemekana wanasubiri either litokee la kutokea Sasa hivi, au hata 2030 ambapo mzanzibari Samia atakuwa sio Rais Tena wa Tanzania ambapo ataingia Rais Mtanganyika basi bunge litabadili Sheria kuwa Tanzania isitawaliwe na Mtu Zanzibar , mana madhara ni makubwa na Chama kinapata wakati mgumu Kwa wananchi ambao wengi hawataki au hawapendi kutawaliwa na Rais kutoka Zanzibar.
Shida sio uongozi wa Samia labda ni Mbaya sana, ila Kitendo Cha Tanganyika kutawaliwa na Mzanzibari hiyo ndo shida, hata kama Samia angempa Kila mtanzania Bilioni moja bado watanganyika hawawezi mioyoni mwao kukubali mzanzibari.
Ni kama Labda tuseme itokee tu Nchimbi awe Rais wa Zanzibar ni kitu ambacho hakipo.
Kwa Hali ilivyo Samia ndo atakuwa Rais wa Mwisho kutawala kutoka Zanzibar. Na CCM ya Samia Haitaki Lissu agombee, mana akigombea uchaguzi hautakuwa CCM vs Wapinzani. Uchaguzi utakuwa ni Zanzibar VS Tanganyika, ambapo matokeo yatakuwa mabaya,
CCM hawawezi kufanya reform mgombea akiwa Samia Kwa sababu hatoweza kushinda, ila wakibadili Mgombea wanaweza kushinda. Nyingi Hamjui ilivyo tabu kumpenda mtoto wa Kambo kuliko mtoto uliemzaa wewe