Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni: Nchini Uganda mtoto wa miaka 9 amuoa mtoto mwenzie wa miaka 6

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,848
20,697
Picha


UKISTAAJABU ya Musa utayashuhudia ya Firauni, utamaduni wa watu wa magharibi mwa Uganda ni wa ajabu sana.

Wakazi wa kijiji cha Nakapyata, wilayani Buyende nchini Uganda wamefanya sherehe ambapo watoto wawili wenye umri wa miaka tisa na sita waliozwa.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Uganda, mvulana mwenye umri wa miaka tisa ambaye anasoma darasa la nne katika shule ya msingi ya Buyende na msichana mwenye miaka sita ambao wote waliripotiwa kuzaliwa wakiwa na meno mawili waliozwa siku ya Jumatatu na kupatiwa nyumba ya kitamaduni ili waishi pamoja.

Chini ya Sheria za Uganda, ni makosa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 kufunga ndoa ama hata kushiriki katika tendo la ngono. Serikali inaendelea kuchunguza utamaduni huo ambao unakiuka sheria za mtoto.

Inadaiwa watoto hao wawili walianza kuchumbiana wakati mvulana alipokuwa na umri wa miaka mitatu na msichana akiwa na umri wa miezi mitatu pekee. Hatua hiyo baadaye iliimarisha uhusiano kati ya familia zote mbili, huku Delifazi Mulame baba wa mvulana akimuita msichana huyo kama ‘mke wa mwanangu’. “Mwanangu alizaliwa na meno mawili na mkewe akazaliwa na meno mawili.

Kuzaliwa kwake kulileta baraka nyingi na jina lake linapaswa kuwaunganisha watu wa makabila ya Baganda na Basoga,” alisema Mulame.
 
Kwa hiyo meno hayo ndio sababu ya kuoana kwao au kuna kingine kama kubalehe au kuvunja ungo?
Nakumbuka miaka ya nyuma kuna mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 3 aliota matiti na Dr walithibitisha kuwa anaweza kupata ujauzito FACT

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kwa hiyo meno hayo ndio sababu ya kuoana kwao au kuna kingine kama kubalehe au kuvunja ungo?
Nakumbuka miaka ya nyuma kuna mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 3 aliota matiti na Dr walithibitisha kuwa anaweza kupata ujauzito FACT

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Mtoto wangu pia alikutwa na hill janga akiwa na miaka 2 na ma Dr walithibitisha hill pia. No changamoto kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshukuru Mungu yupo vizuri kwa sasa amesharudi kwenye hali yake ya utoto. Pata picha mtt wa miaka 2 anaota maziwa na nywele sehemu za siri, ni mtihani kwakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Haki ya Mungu ni mshtuko sana
Pole sana kwa hayo na Mungu amuangalie
Ni muujiza tunaonyeahwa kwamba kila kitu kinawezekana
Umepitia magumu sana na umevumilia
Sina haja.ya kukuuliza mengi najipa majibu mwenyewe
Pole sana

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Hao madoctor fake. Huo uongozi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Fake kivipi wakati ushuhuda unauona na mwenye mtoto anakuambia alikuwa na maziwa na nywele za chini kuota kwa miaka 2
Hili nakumbuka kuna mtoto SA alikuwa hivyo na alikuwa na miaka 3 tu chuchu kubwa tu na alikuwa anapata hedhi
Sasa kama anapata hedhi mimba itakosekanaje?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Hiyo siyo mara ya kwanza kutokea kisichana cha miaka 6 kuolewa. Kuna "mtume" alimuoa binti mwenye umri wa miaka 6 wakati muoaji akiwa na umri wa miaka zaidi ya 50.
 
Back
Top Bottom