Ukistaafu ondoka ofisini benki ya posta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukistaafu ondoka ofisini benki ya posta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Kibiongo, Jan 5, 2010.

 1. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna huyu mkuu wa benki ya Posta amestaafu tangu 26/11/2009 lakini hadi leo hii bado tunamuona anaingia ofisini kama kawaida na anadunda mzigo kama zamani. Nimejuzwa kuwa hana barua ya kumwongezea mkataba wala barua ya ajira, lakini eti anasubiri barua toka serekalini kwa maana aliahidiwa na bodi yao kuwa atapewa barua ya mkataba mwingine. Huyu alistaafu rasmi mwaka 1997 baadaye akapewa mkataba wa miaka mitatu na ameendelea hivyo hivyo na mikataba hadi hiyo 26/11/2009 mkataba wake wa nne ulipomalizika. Sasa fikiria ana umri gani.

  Mshahara wa desemba kakunja bila mkataba, benki ina wakuu wa vitengo vya fedha, sheria, ukaguzi wa ndani, rasilimali-watu nk. lakini wako kimya. Je, tuelewe kuwa wanatafuna naye jasho la wafanyakazi wanyonge au anatumia nguvu za giza. Vyombo husika, wizara ya fedha, benki kuu, bodi ya wakurugenzi wote kimyaa !!!!!!!!!!!! Jamaa kaoa mke toka Mlingotini sijui ndiyo maana wote hao hawaoni ndani wamezibwa macho na akili na ujasiri. Maamuzi yake hayana difference na yule mkuu wa ile nyumba kubwa ya kule Zimbambwe, yaani ni ubabe juu ya ubabe ukifanya fyoko kazi huna. Lo!! poleni sana wana benki ya posta maana hamna pa kulilia, mzazi wenu bodi naye kapigwa kipapai haoni ndani ila kadata tu kama panya aliye banwa na mlango.

  Wanajamvi nimewatonya haya machache ili tusaidiane kuyafanyia utafiti wa kina kuona uhalali wa kikongwe kuendelea kukaa ofisini na kutafuna mihela ya wavuja jasho bila barua yoyote na kufanya maamuzi ambayo mimi nayaite kuwa ni BATILI. Tumwambie waziwazi kuwa ONDOKA OFISINI BWANA. Umestaafu, BASI INATOSHA.

  Jamani tusichoke kupiga kelele hadi kieleweke.

  Nasubiri michango yenu.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,388
  Trophy Points: 280
  tupatie details na majina tumvae kwani nani kasema amerasimishwa ofisi?
   
 3. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahasante Mzee Mwanakijiji, huyo mkuu wa benki ya Posta anaitwa Alphonce Kihwele, Mkuu wa Fedha anaitwa Mhule, Mwenyekiti wa bodi anaitwa Mama Rutashobya (Prof) toka Chuo kikuu pale Mlimani. ENDELEA.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu mama Mwenyekiti wa Bodi si ndiye yule mama alikuwa kwenye bodi ya BOT wakati Ballali na Mafisadi wanaiba hela za EPA? Sasa ana sifa gani zaidi za kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya benki wakati tenure yake BOT ilikuwa na madudu mazito?Serikali ya muungwana kweli haina hadhi!!
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Majungu kwa kwenda mbele...
   
 6. M

  Myamba Senior Member

  #6
  Jan 6, 2010
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yes, Mama Rutashobya was with the BOT. Actually this is the case of BOT, TPB Board and Ministry of Finance to deal with.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,106
  Trophy Points: 280
  Kweli kuna watu wabishi jamani.
   
 8. O

  Omumura JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wapo wengi wa aina hiyo wamejaa kila kona ya ofisi za umma.
   
 9. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Tuwe makini na watu wa aina hii,waweza kuwa kati ya wale waishio kwa nguvu za GIZA huku wakiendelea kutuulia maalbino wetu,Kama mkataba umekwisha aende nyumbani akae na familia yake ikitokea akaongezwa arudi apokelewe,Inakuwaje mtu mkataba umekwisha bado yuko ofcn anafanya kazi na kusaini mikataba kana kwamba bado ni mtendaji mkuu.Ngoja nitafiti kidogo kuhusu huyu mtu nitarejea kwenu
   
 10. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Mkuu Masatu,cjakuelewa unaposema majungu kwa kwenda mbele unamaanishi hoja isizungumziwe kwa kuwa ni majungu au una maana nyingine.Nafikiri ni vema mjadala uendelee ili ukweli uje peupe,Ni vigumu kuamini kwamba mtu aweza kaa ofcn huku hana mkataba na aone sawa kabisa,Lakini kwa Tanzania yetu yote yanawezekana kwani wengi wako juu ya sheria nji hii...
   
Loading...