Ukisoma ilani ya uchaguzi ya CHADEMA unashindwa kuelewa kwanini walimpinga Magufuli

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2015 pamoja na mambo mengine, ilikuwa na mambo yafuatayo;

1. Kujenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa viwango vya kisasa kwa kuzingatia maslahi ya nchi.

2. Kuboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa nchi jirani.

3. Kujenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora

4. Kujenga shirika la ndege la taifa

5. Kujenga miundombinu ya kisasa kwa lengo la kuondoa misongamano ya magari katika majiji, kuimarisha usafiri wa majini kwa kuboresha na kuweka miundombinu mipya.
 
Tatizo sio kati ya haya uliyoainisha... Bali ni kuwafanya CDM kama upinzani ni adui no 1 nchini, kuua kutesa, kuteka!! Haya ndio moja ya sababu kubwa ya chuki!!
 
Wanamchukia amesababisha wakose sera. Uwezo wao wa kufikiri uliishia pale.
 
Uharamu upi, kujipigia debe ni uharamu? Utasemaje kuhusu William Ruto wa Kenya ambaye alifanya kampeni kwa miaka yote mitano, tena akiwa serikalini?
Utakuwa mtoto mdogo usiyejua kilichokuwa kinaendelea. Kuna mzee mmoja hapo Arusha anaitwa Kasori. Huyu alikuwa personal assistant wa Mwl Nyerere hadi 1999 Nyerere alipofariki, wakiwa na mmoja wa walinzi wa mwalimu aliyeitwa Tendewa. Baada ya Lowasa kuupata uwaziri mkuu, Tendewa ndiye alikuwa mkuu wa ulinzi kwa Lowasa.

Come 2015, mzee Kasori alipinga bila kificho ugombea wa Lowasa, akaandika makala nyingi magazetini kuelezea uchafu wa Lowasa.

Kilichofuata ni Kasori kuikimbia nyumba yake baada ya kutishiwa kuuwawa na Tendewa.

Not fair, huh? RIP Mtikila.
 
CDM Kwa sasa ni UNPREDICTABLE.

Baada ya KATIBA mpya kupatikana,

Ni kheri kikazaliwa chama kipya, CHOTARA, kisichofungamana na CCM Wala CDM.

Kisichokuwa Cha kijamaa Wala kibepari. Non alignment.

Tusubiri.
 
Kumbe Magu alikuwa anafiata sera za CHADEMA ndio maana CCM wenzake walikuwa wanamchukia a k.a walamba asali
Aliamua kutekeleza ilani ya CDM, akachukiwa na CCM wenzie, akajua ataungwa mkono na CDM , walipomkana ndo akaanza kujaribu kuwanunua aje kufanya nao KAZI Serikalini,

Mnyikaaah ilibaki kiduchu asalimu AMRI bt mwisho aligoma.

Magu alikosea support Kutoka pande zote, bt wananchi tulimpenda sana.

Mungu ni mwema, naamini atatuletea MZALENDO mwingine aina ya Magu.

Ameen
 
Umeshindwa kabisaa kuwaelewa hawa chadema wao hawakumchikia kwa sababu ya ilani walimchukia sababu ya kupora uchaguzi
 
Tatizo sio kati ya haya uliyoainisha... Bali ni kuwafanya CDM kama upinzani ni adui no 1 nchini, kuua kutesa, kuteka!! Haya ndio moja ya sababu kubwa ya chuki!!
Hayo ni 9 la 10 ni kuwa tundulissu alisema ndani siku 100 angemnyonga Magufuli, angewaachia wafungwa wote, na kupandisha mishahara ya Polisi na watumishi wote. Akawa amesahau kabisa kuwa Katiba ya CHADEMA haimpi Rais madaraka hayo kila Jimbo (=kabila) litakuwa na Rais wake na IGP wake na Hazina yake.
 
Hayo ni 9 la 10 ni kuwa tundulissu alisema ndani siku 100 angemnyonga Magufuli, angewaachia wafungwa wote, na kupandisha mishahara ya Polisi na watumishi wote. Akawa amesahau kabisa kuwa Katiba ya CHADEMA haimpi Rais madaraka hayo kila Jimbo (=kabila) litakuwa na Rais wake na IGP wake na Hazina yake.
Unayo clip mkuu
 
Back
Top Bottom