Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kama ukisoma mafundisho ya dini nyingi hata yale ya asili utabaini kwamba mbinguni ni mahali ambapo panatakiwa kuogopwa na kukwepwa. Tunaambiwa kuwa kuna pepo lakini pia kuna moto.
Hakuna hata mmoja ambaye amewahi kufa na kurejea na kutuambia kilichotokea baada ya kifo. Tunahofia kwa sababu hatuna uhakika na kitachotokea baada ya kifo na ndio maana tumebaki kutishwa na maandiko ya dini.
Maandiko mengi ya dini yamejaa vitisho vingi ambavyo ukisoma utaogopa sana kifo, tumetishwa kuhusu kuchomwa moto, kuumwa na majoka, na kuishi kwenye giza milele na mateso mengine ya ajabu ajabu, ikiwa unajihisi una dhambi hofu ndio inazidi kuongezeka maana unajua kuwa hutakuwa salama.
Hivi ni nani kati yetu ana uhakika kuwa akifa ataenda peponi? Naamini hilo ni swali gumu kwa kuwa hakuna hata mmoja kati yetu aliyewahi kujiuliza swali hilo.
Kuna masharti magumu sana yanayosimuliwa katika dini zetu hizi ambayo inabidi yatimizwe ili mtu aweze kufika peponi, na kwa kuwa wengi wetu tunajua kwamba ni vigumu kuyatimiza masharti hayo tumejikuta tukihofia kifo, kwa sababu tunajua kwamba tukifa hatutakuwa salama.
Hivi kama mafundisho ya dini yangesema kuwa huko mbinguni kuna pepo tu, ni nani angehofia kifo?
Watu hawataki kuyaacha maisha hata kama ni mabaya naya kutisha kwa sababu hawana uhakika na maisha yao baada ya kifo, wanajiuliza je huko mbinguni maisha yatakuwaje? Kwa nini mtu afe, halafu akateseke zaidi? Huko hakuna mjadala kama mtu ni wa motoni ni wa motoni tu.
Kama ukimwambia mtu asijali hata kama akifa, kwa sababu kifo kina maana ya kuuacha mwili na sio yeye kupotea, anaweza kukuuliza, "kama nitauacha mwili ina maana gani mimi kuendelea kuwepo? Sitakula, sitafanya mapenzi, sitaendesha gari, sasa ya nini kufa?"
Ni kweli yuko sahihi kwa sababu kipimo chake ni mahitaji ya mwili, kwa kuwa ndiyo anayoyafahamu zaidi.
Kwa bahati mbaya Dini zetu zinawatisha wengi badala ya kuwafundisha kuhusu baada ya kifo.
Ukweli ni kwamba maisha baada ya kifo yapo, lakini hayatakuwa kama haya tunayoishi tukiwa na miili hii inayoonekana. Ni vigumu mtu kuamni kwa sababu tumekuwa tukiishi na miili hii tunayoiona tangu kuzaliwa kwetu na hivyo kukubali nadharia hii ni ngumu kidogo.
Hebu nikuulize wewe unaesoma hapa, Hivi hujasikia watu wakisema "Bora mungu amchukue akapumzike" pale ambapo kuna mgonjwa anayeumwa na ugonjwa unaomtesa na kumpa maumivu makali? Au hujawahi kusikia watu wakisema " Bora kafa akapumzike kwa amani, ameteseka sana"
Hivi kumbe watu wakifa wanapumzika! Ajabu eeh! Sasa huu moto wa milele na majoka, na mateso mengine tunayoambiwa yanatoka wapi? Je huko kupumzika kunakosemwa kunaweza kuwa ni mahali kwenye nafuu zaidi ya mateso anayoyapata huyo mgonjwa kwa wakati huo? Sidhani kama hilo lina ukweli.
Labda nihitimishe kwa kusema kuwa kufa ni hatua muhimu ya mwanaadamu kutoka katika hatua moja kwenda hata nyingine, ambayo itakuwa ni tofauti na mwili huu tunao uona, mwili ambao hauwezi kujibainisha na mwili huu tulionao, kwa hiyo unapofiwa huna haja ya kuhofu kwani huyo aliyekufa hajapotea bali amechukua mwili mwingine na kuanza maisha mapya.