Ukisoma hapa hutaogopa kifo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukisoma hapa hutaogopa kifo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Aug 11, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,751
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Kama ukisoma mafundisho ya dini nyingi hata yale ya asili utabaini kwamba mbinguni ni mahali ambapo panatakiwa kuogopwa na kukwepwa. Tunaambiwa kuwa kuna pepo lakini pia kuna moto.

  Hakuna hata mmoja ambaye amewahi kufa na kurejea na kutuambia kilichotokea baada ya kifo. Tunahofia kwa sababu hatuna uhakika na kitachotokea baada ya kifo na ndio maana tumebaki kutishwa na maandiko ya dini.


  Maandiko mengi ya dini yamejaa vitisho vingi ambavyo ukisoma utaogopa sana kifo, tumetishwa kuhusu kuchomwa moto, kuumwa na majoka, na kuishi kwenye giza milele na mateso mengine ya ajabu ajabu, ikiwa unajihisi una dhambi hofu ndio inazidi kuongezeka maana unajua kuwa hutakuwa salama.

  Hivi ni nani kati yetu ana uhakika kuwa akifa ataenda peponi? Naamini hilo ni swali gumu kwa kuwa hakuna hata mmoja kati yetu aliyewahi kujiuliza swali hilo.

  Kuna masharti magumu sana yanayosimuliwa katika dini zetu hizi ambayo inabidi yatimizwe ili mtu aweze kufika peponi, na kwa kuwa wengi wetu tunajua kwamba ni vigumu kuyatimiza masharti hayo tumejikuta tukihofia kifo, kwa sababu tunajua kwamba tukifa hatutakuwa salama.

  Hivi kama mafundisho ya dini yangesema kuwa huko mbinguni kuna pepo tu, ni nani angehofia kifo?

  Watu hawataki kuyaacha maisha hata kama ni mabaya naya kutisha kwa sababu hawana uhakika na maisha yao baada ya kifo, wanajiuliza je huko mbinguni maisha yatakuwaje? Kwa nini mtu afe, halafu akateseke zaidi? Huko hakuna mjadala kama mtu ni wa motoni ni wa motoni tu.

  Kama ukimwambia mtu asijali hata kama akifa, kwa sababu kifo kina maana ya kuuacha mwili na sio yeye kupotea, anaweza kukuuliza, "kama nitauacha mwili ina maana gani mimi kuendelea kuwepo? Sitakula, sitafanya mapenzi, sitaendesha gari, sasa ya nini kufa?"
  Ni kweli yuko sahihi kwa sababu kipimo chake ni mahitaji ya mwili, kwa kuwa ndiyo anayoyafahamu zaidi.

  Kwa bahati mbaya Dini zetu zinawatisha wengi badala ya kuwafundisha kuhusu baada ya kifo.

  Ukweli ni kwamba maisha baada ya kifo yapo, lakini hayatakuwa kama haya tunayoishi tukiwa na miili hii inayoonekana. Ni vigumu mtu kuamni kwa sababu tumekuwa tukiishi na miili hii tunayoiona tangu kuzaliwa kwetu na hivyo kukubali nadharia hii ni ngumu kidogo.

  Hebu nikuulize wewe unaesoma hapa, Hivi hujasikia watu wakisema "Bora mungu amchukue akapumzike" pale ambapo kuna mgonjwa anayeumwa na ugonjwa unaomtesa na kumpa maumivu makali? Au hujawahi kusikia watu wakisema " Bora kafa akapumzike kwa amani, ameteseka sana"
  Hivi kumbe watu wakifa wanapumzika! Ajabu eeh! Sasa huu moto wa milele na majoka, na mateso mengine tunayoambiwa yanatoka wapi? Je huko kupumzika kunakosemwa kunaweza kuwa ni mahali kwenye nafuu zaidi ya mateso anayoyapata huyo mgonjwa kwa wakati huo? Sidhani kama hilo lina ukweli.

  Labda nihitimishe kwa kusema kuwa kufa ni hatua muhimu ya mwanaadamu kutoka katika hatua moja kwenda hata nyingine, ambayo itakuwa ni tofauti na mwili huu tunao uona, mwili ambao hauwezi kujibainisha na mwili huu tulionao, kwa hiyo unapofiwa huna haja ya kuhofu kwani huyo aliyekufa hajapotea bali amechukua mwili mwingine na kuanza maisha mapya.


   
 2. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,854
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  ni dini gani za asili zinazofundisha vitisho ,by the way unamaanisha nini unaposema dini za asili?
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Niseme tu, hujabadilisha mtazamo wangu kuhusu kifo.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,057
  Likes Received: 3,805
  Trophy Points: 280
  Natafakari...
   
 5. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yohana wa ufunuo aliona watu wakienda motoni idadi yao kama mchanga wa bahari. Hawa ni wengi kutisha. Hivyo usiwe na wasi kama utaenda motoni utakuwa umetimiza neno la Mungu vilevile.
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 10,995
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Hana jipya hata kidogo! Karibu A town leo! Kwn utakutana na makamanda wakiendeleza harakati ya Ukombozi leo.
   
 7. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,849
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  AminI Mungu yupo na utalipwa kulingana na matendo yako hapo siku ya mwisho.
   
 8. sixgates

  sixgates JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 3,972
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  umetoa maoni yako,haikosi ni hisia zako. .si tunafata kile ambacho Mungu ametuambia kupitia vinywa vy manabii,haikutosha miaka elfu mbili iliyopita Yesu alikuja mwenyewe. . .wewe unachofanya ni kutuambia dini ina vitisho,siwez kukataa,ila neno la Mungu lina fact!. .n way nimependa jin mtazamo wako japo hauna logic.
   
 9. d

  davestro Senior Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama nlivyokuwa sijijui kabla ya kuzaliwa ndivyo ntakavyokuwa nikifa.Thats what I Believe
   
 10. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 921
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kama huamini basi jibu maswali haya mawili 1.Kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi? 2. Ulalapo huoti ndoto nzuri na mbaya? 3. Kama no2 ni ndiyo je,uliyoyaota ulikuwa na uwezo wa akili na mwili? Hitimisho: Maandiko yanasema tutafufuliwa,hivyo tutarudi na miili yetu kama awali. Tafadhali epuka nadharia za Darwin.
   
 11. olele

  olele JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 80
  Cheza kamari, ukiamini Mungu yupo na utende mema hautapoteza chochote kuliko usipomuamini halafu ukamkute, utafanyaje?
   
 12. K

  Karry JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hakuna dini inayotoa vitisho
   
 13. A

  Aine JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,615
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndg, ni afadhali uamini ukifika huko usimkute huyo Mungu, haitakucost chochote, KULIKO kutoamini halafu ukifika huko umkute amejaa tele utalia na kusaga meno na hayo uliyoyaandika hapo yatakufuata. Mungu yupo, kufa kupo, jehanam, ipo na MBINGU ipo, afadhali uamini leo kabla hasira ya Mungu haijawaka juu yako
   
 14. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  unapinga nadharia kwa kutumia nadharia.
  Umejitahidi kuandika habari ndefu lakini haina hoja ya msingi.

  Kukusaidia ni kwamba swala la kuogopa kufa sio la imani ya kidini, by nature every living organism struggle for existance, ndomana sio wewe tu mwanadamu unayeogopa kufa hata kuku, bata, njiwa n.K isipokuwa ni kweli kuwa psychology can just modify, na hapo ndio habari za vitisho hivyo ulivyo visema vinachukua nafasi.
   
 15. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Habari yako ndeeefu na haina hoja ya maana
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,483
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri kabla ya kutafuta kama kuna maisha baada ya kifo tafuta kwanza mambo yote yaliyopo duniani ukiwemo wewe mwenyewe yamefanywa na nani? Halafu kama ni mkristo soma Bibilia vizuri. Soma Mathayo 17: 1 - 13 halafu utupe tafakari yako ndugu na link ya Bible naweka kabisa hapa The New American Bible - IntraText
   
 17. m

  mankind Senior Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 185
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  umeeleza vizuri sana mkuu UNA JIPYA.
   
 18. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,796
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Ina-cost Bana, manake itabidi uache dhambi zote kwa maana ya kukaa mbali na Starehe zote,, halafu ndiyo uende usimkute? Dah, nitachoka sana aisee......
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,236
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye Bold huo ufunuo umeutoa wapi?, in short umejuaje kwamba mtu akifa anachukua mwili mwingine na kuanza maisha mapya
   
Loading...