Ukisikia haya maneno ujue unaombwa rushwa

dtj

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
1,333
1,379
1. Sasa umejipangaje?
2. Umekuja na ela ya soda hapo?
3. Tatizo dogo sana hili, vipi unasemaje sasa?
4. Mlungura upo? tufanye kazi!


Kama na wewe umekutana na mengine tupia hapa watu wasanuke... Kimenuka kwa magu. Haki hainunuliwi!
 
hili tatizo limeshakwisha ndg yangu!
pole sana kwa usumbufu ndg yangu!
sisi ni ndugu!
ni muhimu kusaidiana ndugu yangu!

ktk huduma na hasa za serikali, ukiona umekirimiwa kupitiliza kwa kutumia msamiati 'ndugu', jiongeze, nyoosha mkono hapo! Kinyume chake, ukiona mtoa huduma anakupiga bit la kufa mtu, anatokwa na mapovu kwa ukali, mishipa ya shingo imemsimama, lkn hapayuki, sauti yake ipo chini, usiogope, wee jiongeze tu!
 
eh!.. hii kazi tunaifanyaje?
Tunaanzaje?
Nakusikiliza
Kazi ilishaisha hii, bado wewe tu
tatizo lako nishalifanyia kazi, niangalie basi
Kuliona faili lako hadi ninywe maziwa, kuna vumbi sana
Hili si jukumu langu mimi nakubeba tu, bebeka basi
daaah wee kama ulikuwepo siku naambiwa hayo maneno, afu alikuwa mdada, ilibaki kidogo tu ktk kujiongeza, nusu nipitilize, nilitaka kuomba mzigo, lkn sijui ilikuwaje sikuomba!
 
Back
Top Bottom