Ukishangaa ya Simbachawene na Bashe utayaona ya Mwigulu

Mbochong'a

JF-Expert Member
May 2, 2011
759
1,293
Simbachawene: Kuna siku bungeni alikuwa anatoa mchango wake lakini kwa dakika zote za mchango alikuwa anamsifia mkuu. Ilikuwa kuhusu kununua ndege na kujenga SGR na stiglers. Nakumbuka alitoa mpaka mifano ya marais na nchi ambazo wananchi waliteseka kwanza kipindi miradi ya maendeleo inatengenezwa na baadae kuneemeka.

Basi bwana, baada ya kuangalia na kusikiliza ule mchango wake bungeni, kimoyo moyo nikasema mmmmh huyu anaweza kurudishwa kwenye baraza si kwa kumsifia huku mkuu. Kweli, baada kama ya siku tatu hivi akateuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Bashe: Huyu kwanza alikuwa team Lowasa, kwahiyo hakuwahi kuwa kwenye list hata ya reserve ya mkuu wetu. But alitokea kipindi kile makatibu wakuu wastaafu walivyoandika barua kwenda kwa chama kuripoti matendo machafu anayofanya Musiba kuwapaka matope watu mbalimbali walioko kwenye chama na wastaafu.

Basi bwana, baada ya barua ile, Bashe akaichambua na kuitolewa ufafanuzi na katika ufafanuzi wake alikuwa anamkingia kifua mkuu wetu. Alifikia point ya kusema kuwa mpaka sasa hivi wao kama chama wanatambua candidate wa uchaguzi 2020 ni mkuu na si mwingine.
Kupitia ile press na waandishi na kumsifia vile mkuu, nikajisemea tena kimoyo moyo mmmh!! Huyu namuona mahala flani kwenye system. Kweli bwana akateuliwa wizara ya kilimo.

Mwigulu: Kwanza naomba kusema kitu, kwa upinzani! Ni bora huyu jamaa akawa waziri kuliko mbunge wa kawaida. Huyu jamaa ni mwiba kwa upinzani.
Ok, jambo la kwanza lililomsaidia kurudi kwenye baraza ukiachana na mchango wake wa juzi bungeni, ni kuwa humble baada ya uteuzi wake kutenguliwa. Hakuonekana mtu wa kulalamika au kaonewa. So akaendelea kukitetea chama kupitia mitandao n.k.

But, kilichomrudisha barazani ni mchango wake wa juzi bungeni. Alimtetea sana mkuu kuhusu kauli mbalimbali za wapinzani kuhusu kutoonekana mstari wa mbele kwa mkuu wa nchi. Ilifikia point akasema mnataka mumuone mkuu mbele kwani amekuwa nesi!!
Kweli bwana, baada ya masaa machache kuzikwa kwa aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, mkuu akamteua Mwigulu kukava ile nafasi.

Conclusion: Nadhani sasa njia ya kurudi kwenye system imeshaeleweka hasahasa kwa wale mawaziri waliotenguliwa. Juzi kati nilimuona Nape akianza mdogo mdogo. Namshauri asilegeze kamba amshtue na January amwambie kurudi kwenye system ni simple. Ni kujitoa akili tu na kutoa support kwa mzee baba hata kama unaona hapa hakujakaa vizuri.

Ni hayo tu ladies and gentlemen. Tuendelee kujikinga na corona. Hawa virus wapo aisee
 
Ethics za mabaniani (dharma) ukiwa kwenye ajira wewe kaa kwenye mstari wa boss awe sahihi au la loyalty ni muhimu; malipo yake kama kuna promotion wanaanza kufikiriwa wale viherehere wazuri au hata zikitokea nafasi ya kazi zinaanza kufikiriwa familia za viherehere kama wa ndugu wanatafuta ajira kabla ya wengine (that sums up CCM).
 
Ethics za mabaniani (dharma) ukiwa kwenye ajira wewe kaa kwenye mstari wa boss awe sahihi au la loyalty ni muhimu; malipo yake kama kuna promotion wanaanza kufikiriwa wale viherehere wazuri au hata zikitokea nafasi ya kazi zinaanza kufikiriwa familia za viherehere kama wa ndugu wanatafuta ajira kabla ya wengine (that sums up CCM).
Ni kweli kabisa. Viherehere wanakula mashavu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom