Ukishangaa ya Mussa!

Ukishangaa ya Mussa!

Mkandara

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,813
Reaction score
9,063
Wahenga walisema UKISTAAJABU ya Mussa UTAYAONA ya FIrauni. KUMBE Huko Kuona ni zaidi ya kustaajabu maana ni sawa UPUMBAVU wa kuabudu Wachungaji. Sijui kama naeleweka?

Nikumbushe miaka ile ya uongozi wa JK, Chama cha Mapunduzi kilikuwa hatarini yaani kimekwisha kabisa katika ushawishi. Chama hakina sera wala mvuto ilikuwa swala la muda tu. Yaani ilikuwa aibu mtu kujinasibu na Chama na kila mtu alitegemea kuwa huo ndio mwisho wa Utawala wake. Hilo lilikuwa wazi kabisa isipokuwa kwa mbinu za dola.

Wapinzani nao wakaunda nguvu moja ya UKAWA kupambana na dola lakini kama wahenga wasemavyo. Katika Msafara wa Mamba, Kenge nao wamo! Dola ni zaidi ya Chama kimoja ni mtandao mkubwa unaohusu vyombo vyote vya serikali wao hawakuliona hilo.

Nilisema hapa kabla ya Uchaguzi mkuu kuwa Chadema wamefanya kosa kubwa sana kuchanganya nguvu na mahasimu wao, hoja hiyo ilipingwa kwa nguvu kubwa sana na wale wasojua tofauti ya Mamba na Kenge! Kwa sababu kwao hoja kubwa ilikuwa kufika penye maji mengi wakinadi - Mpaka kieleweke!

Nukuu zipo humu humu. Matokeo ya uchaguzi yalipitoka - Upinzani chali, ilikuwaje, Tukaanza kujiuliza funguo za gari kapewa nani?

Chuma akamamata nchi kinyume cha mategemeo ya wengi, hasira zote zikamgeukia Magufuli nsiye hasomu wao, wakati CCM jua linawawakia chama kikarudi kupata nuru! Leo hii imebakia hadithi hadithi..

Nasema hivi kama sio Magufuli kujitoa mhanga kwa chama hiki kuchukua Uongozi kuogmbea Urais mwaka 2015, hiki chama kilikuwa kimekufa kabisa! Ati leo hii kuna watu wanadiriki kabisa kujivunia Chama ilihali wakimnanga Mwendazake! Hawa ndio wale waitwao mitume wa uongo!

Kuna jamii sasa hivi wanaabudu Wachungaji kwa ilani za Utajiri. Hawa watu ni Wapumbavu kwa Marefu na Mapana na katu hutaweza waongoa katika imani zao hata kama wanapotea. Tatizo lake moja tu, Sii rahisi kujua tofauti yetu sisi sote..
 
Nasema hivi kama sio Magufuli kujitoa mhanga kwa chama hiki kuchukua Uongozi kuogmbea Urais mwaka 2015, hiki chama kilikuwa kimekufa kabisa! Ati leo hii kuna watu wanadiriki kabisa kujivunia Chama ilihali wakimnanga Mwendazake! Hawa ndio wale waitwao mitume wa uongo!
Kingekufa mara ngapi, kifo huwa ni kimoja tu
 
Hii nchi inachekesha sana. Kweli leo hii kuna watu wanaupigia upatu na mfano utawala wa Magufuli??
Ungejua maana ya aupatu wala usingeweza jenga hoja. Kifupi, kulaani utawala wa Magufuli ni sawa na walolaani utawala wa Ghadaff huko Libya. Miafrika kama Punda bila bakora haiendi..
 
Kingekufa mara ngapi, kifo huwa ni kimoja tu
Kinge ina maana ponapona, chupuchupu, mtoto alookolewa toka shimo la choo! Kiswahili lugha nyepesi sana..
 
Ungejua maana ya aupatu wala usingeweza jenga hoja. Kifupi, kulaani utawala wa Magufuli ni sawa na walolaani utawala wa Ghadaff huko Libya. Miafrika kama Punda bila bakora haiendi..
Unamiliki na ufahamu wa watu wengine? Kama sijui maana ya "kupigia upatu" unadhani ningeandika. Ghadaff ana maajabu gani ya kusifiwa. Ama kule kuponda kwake maraha Ulaya na wale wasichana ndiyo jambo ya kusisimua?

Mifano ya viongozi bora kwa Afrika haipaswi kuwa Magufuli na Ghadafi.
 
Unamiliki na ufahamu wa watu wengine? Kama sijui maana na "kupigia upatu" unadhani ningeandika. Ghadaff ana maajabu gani ya kusifiwa. Ama kule kupnda kwake maraha Ulaya na wale wasichana ndiyo jambo ya kusisimua?

Mifano ya viongozi bora kwa Afrika haipaswi kuwa Magufuli na Ghadafi.
Kamsifie Zamaradi basi, nyie waumini wa Wachungaji na maji ya upako tutawaeleza nini?
 
..Tatizo la Magufuli lilikuwa ni ukatili tena usiojificha.

..Magufuli alikuwa hajisumbui kuficha uovu wake, na ndio maana ni Raisi anaryeshambuliwa kuliko watangulizi wake.

..Kwa mfano, unampiga Mbunge Risasi ktk makazi ya viongozi wa bunge la serikali halafu unategemea watu wasichukizwe.
 
Kamsifie Zamaradi basi, nyie waumini wa Wachungaji na maji ya upako tutawaeleza nini?
Bado unarudia kosa lile lile. Wewe humiliki hisia na fahamu za watu wengine. Mimi nimsifie Zumaridi kwa lipi la maana alilonalo?

Huoni kwamba Zumaridi na hao watu wako wanafanana? Wote ni watu waliofanikiwa kuwavunga (Brain washing) mbongo zao watu wachache wajinga!!

Watawala bora ni wale wanaopingana kwa hoja na watu wanaowapinga na siyo kwa mabavu ama ghiliba!!
 
Bado unarudia kosa lile lile. Wewe humiliki hisia na fahamu za watu wengine. Mimi nimsifie Zumaridi kwa lipi la maana alilonalo...
Hahahaha sasa CCM imewafanyia nini Wananchi? Kama shule za kata tumezisikia toka Lowassa akiwa makamu wa rais, miradi ya umeme na maji kufika vijijini yote ya Magu! Ufisadi umerudi kama zamani kina Symbion IPTL wote wanavuta hela, miradi haikamiliki bado waumini wa Wachungaji mnaenda kanisani...kwikwikwi!
 
Hahahaha sasa CCM imewafanyia nini Wananchi? Kama shule za kata tumezikoa toka Lowassa akiwa makamu wa rais, miradi ya umeme na maji kufika vijijini yote ya Magu! Ufisadi umerudi kama zamani kina Symbion IPTL wote wanavuta hela, miradi haikamiliki bado waumini wa Wachungaji mnaenda kanisani...kwikwikwi!

..usiseme ufisadi umerudi kana kwamba kulikuwa hakuna mafisadi wakati wa Magufuli.

..sema mafisadi wa wakati wa Magufuli wanabadilishana nafasi na mafisadi wa utawala wa Samia.
 
..usiseme ufisadi umerudi kana kwamba kulikuwa hakuna mafisadi wakati wa Magufuli.

..sema mafisadi wa wakati wa Magufuli wanabadilishana nafasi na mafisadi wa utawala wa Samia.
Ebu nipe mifano kwa ushahidi, maana kusema rahisi sana! Mama Samia kabadilisha viongozi wateule 200 na bado watu wanapiga hela! Uwajibikaji unazidi kupungua, vilio vyenu mnavileta hapa JF..
 
Mkandara andika basi ueleweke.

Miradi gani haijakamilika?

Enzi za Magufuli kulikuwa hakuna rushwa?

REA imeanzishwa mwaka 2007 hata kabla huyo mtu wako hajawa Rais, kwa nini sifa zote ziende kwake??

Maji toka ziwa Victoria na Program kubwa za maji zilianza enzi Lowassa akiwa Waziri wa maji, kwa nini yeye Magufuli ndiyo mnamvika kila sifa hata asizozistahili??

Halafu kama watu wanakwenda Kanisani wewe kinakukera nini? Mbona hujaandika watu wanaokwenda Bar, Mpirani, kwa makahaba, au kwenye matamasha ya muziki??
 
Ebu nipe mifano kwa ushahidi, maana kusema rahisi sana! Mama Samia kabadilisha viongozi wateule 200 na bado watu wanapiga hela! Uwajibikaji unazidi kupungua, vilio vyenu mnavileta hapa JF..
Unakumbuka Magufuli alibadilsha wakurugenzi wa Halmashauri 120 kwa wakati mmoja na bado ripoti ya CAG ikaonesha kuwa huko kwenye Halmashauri hela zinaliwa kama mchwa wanavyokula fito zilizojengea nyumba ya udongo??
 
Ebu nipe mifano kwa ushahidi, maana kusema rahisi sana! Mama Samia kabadilisha viongozi wateule 200 na bado watu wanapiga hela! Uwajibikaji unazidi kupungua, vilio vyenu mnavileta hapa JF..

..Na wapinzani kutekwa, kuteswa, na kuuwawa, nako unatetea?

..Magufuli alipokufa aliacha wafuasi wa Chadema zaidi ya 400 ktk magereza mbalimbali kwa tuhuma za uongo za kisiasa.

..sasa hebu mlinganishe Magufuli na wakoloni wa Kiingereza. Je, Muingereza aliwafunga au kuwaweka korokoni wafuasi wangapi wa Tanu? Wakati tunapata Uhuru wafuasi wangapi wa Tanu walikuwa magerezani ili tuweze kusema Magufuli ana afadhali kuliko Wakoloni?
 
Ni mbinu zipi zilitumika kuhakikisha ccm haipotezi dola
 
Back
Top Bottom