Ukishangaa ya Musa utaona ya filauni

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
334
Mkuu huyo wa Mkoa amemwambia Makamu huyo wa Rais kuwa Mara kuna utajiri mkubwa wa madini aina ya dhahabu katika vijiji 19 vya Wilaya ya Musoma Vijijini, vijiji 7 vya Wilaya ya Serengeti na pia katika vijiji 11 vilivyopo wilayani Tarime, huku Wilaya ya Rorya kunafanyika utafiti ambako kuna dalili za kuwapo dhahabu.

Machibya alieleza kuwa madini ya dhahabu yamepata wawekezaji katika migodi ya Norh Mara ambako kuna kampuni ya uchimbaji ya Barrick Tanzania ambayo kwa mwaka jana ilizalisha kilo 10,052,488, zenye thamani ya dola za Marekani 163,938,056 na kwamba Serikali ilipata mrahaba wa dola 4,956,753.28. Huku ikichangia huduma za jamii dola 353,000.
Source:Habari Leo,March 02, 2008http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=7381

Hayo maandishi niliyo yawekea rangi,yanaonyesha jinsi tulivyologwa(?)Kampuni ya madini inapata $163bn, serikali inaambulia $4ml na eti huduma za jamii za thamani ya $300elfu. Hapo mkuu wa mkoa anaona tumefaidi, kumbe ni zero kabisa. Jamani wana JF hii imekaakaaje lakini. Tuko makini na raslimali zetu!!!!
 
This is nonsense,madini yetu alafu hao jamaa wanachukua Lions share.
Something has to be done here
 
Source:Habari Leo,March 02, 2008http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=7381

Hayo maandishi niliyo yawekea rangi,yanaonyesha jinsi tulivyologwa(?)Kampuni ya madini inapata $163bn, serikali inaambulia $4ml na eti huduma za jamii za thamani ya $300elfu. Hapo mkuu wa mkoa anaona tumefaidi, kumbe ni zero kabisa. Jamani wana JF hii imekaakaaje lakini. Tuko makini na raslimali zetu!!!!

Hizo takwimu hazina ukweli wowote, hata HabariLeo la leo title ya habari hiyo kwenye gazeti hili inasema "Makamu wa Raisi Adanganywa" inawezekana wale walio-upload kwenye mtandao wamepitiwa.
 
Wamekosea ? Hili ni gazeti la Serikali kweli wanaweza kukosea namna hii ? Wakuu wa Mikoa nadhani hawa ni washikaji wa Kikwete so wanafanya yale wanayo imbishwa na serikali kuu ambayo ni Kikwete .Kikwete nawakumbatia watu wa aina hii unategemea sasa yeye aliyepewa kuangalia maslahi ya Chama na Kikwete afanyeje ?
 
BWM - LAMADA ILIYOPO ILALA
-MRADI WA KIWILA (TANESCO ITALIPA MILLIONI300 KILA SIKU
UKIWA TAYARI.
- HOTELI YA NYOTA 3 AFRIKA KUSINI.
-NYUMBA YA KIFAHARI LUSHOTO.
- MAMILIONI YA DOLA KATIKA MABENKI YA NJE.
- MALORY YA MIZIGO YASIOPUNGUA 20 (SCANIA 124 MODEL @
MILIONI 80)
NJIA ALIZOTUMIA KUPATA PESA , EPA,LOAN NBC
HAKULIPA MPAKA NBC IMEUZWA NA DENI LAKE. FURSA SAWA KWA
WOTE. NA NJIA ZINGINE AMBAZO AKIWA IKULU AMEFANIKISHA
KUPATA PESA KWA NJIA CHAFU.( NDIO SABABU BALALI MPAKA LEO
SERIKALI INASHINDWA KUMREJESHA.
KWA HIYO NAWAAMBIA WATANZANIA WENZANGU, TULIPOTOKA NI MBALI NA AWAMU YA TATU WAMETUMALIZA SI MMCHEZO KWA MIAKA 10,

IKIWA AWAMU YA NNE KWA MIAKA MIWILI TU VITU VYAO NDIO HIVI ITAKUWAJE NA HAWA WAKIFIKISHA MIAKA 10, MUNGU TUSAIDIE KUWAFICHUA NA WENGINE.
ONYO KWA MUHESHIMIWA JK KIMYA CHAKO UNACHOKAA KWA SABABU NA WEWE UNATA KA KUWA KAMA HAO MASWAHIBA WAKO KUPITI CHAMA CHAKO TUTAKUHAMA,KWANI KWA SASA MMEZIDI MPAKA TUNAWACHUKIA, ITAFIKA WAKATI TUTAAMUA MMOJA WACHACHE WAFE HAKI IPATIKANE,HAIWEZIKANI SISI WATANZANIA TUENDELEE KUCHAGUA MAFISADI WATUTAWALE WAKATI TUKIWAJUA KICHAKA CHENU NI C C M. SOMA ALAMA ZA NYAKATI JK KAMA ULISHAAZA KUINGIZA MKONO KWENYE KASIKI LA TAIFA, TOA MKONO WAKO MAPEMA WENZIO WATAKUKIMBIA USINYAMAZE KIMYA UKASEMA UNAWASTIRI WENZAKO HAWAKO NA WEWE KWASABABU WAMESHAGUNDULIKA,WANATAFUTA JALALA LA KUTUPIA UCHAFU WAO, NA WAMESHAPATA JALALA HILO NI WEWE WANATAFUTA SABABU TU YA KUKUSHIKA PABAYA WAANZE.
WATANZANIA WENGI TUNAJUA UCHAFU WENU, HAYA YALIYOJITOKEZA YA RICHMOND EPA IPPTL,KIWIRA NK NI KAMA TONE LA MAJI KATIKA BAHARI, KWA TAARIFA MALI ZA JAMAA YAKO EL NI NUSU YA BAJETI YA SERIKALI YAKOKWA MWAKA MMOJA , NDANI YA MIAKA MIWILI TU MLIOKAA. NI HATATRI SIJUI NI MASHINDANO GANI MNAYOSHINDANA KUDHULUMU WATANZANIA BILA HURUMA. KWA NINI HAMPENDI KUSIFIWA KUWA INCHI IMEKUWA KWA UCHUMI KWA SABABU YA UONGOZI WENU,BALI MNAWAACHA WANANCHI MAFUKARA HOHEHAHE,NA MKILAZIMISHA KUTUKUZWA BILA SABABU,RUDINI KWA MOLA WENU MUOGOPE MOTO WA KESHO ,MTAULIZWA JUU YA UONGOZI WENU,NDUGU JK BADILIKA USIOGOPE WACHACHE WALAFI,WANANCHI TUTAKULINDA UKIONYESHA DHAMIRA YA KWELI, KWA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WALIOHUSIKA KULAMBA KILA WALICHOKIONA MBELE YAO.USIFANANE NA WAO,USIKUBALI KUTUMIKA KUWAFICHA NA KUWAKINGIA KIFUA HAO, WATAKUGEUKA SIKU HIYO HAKI ITAKAPOSIMAMA,WATAUMIA WATOTO WAKO NA FAMILIA KWA JUMLA , WAJENGEE HESHIMA KUTOKANA NA UONGOZI WAKO, USITAKE KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KULINDANA, USITAKE DUNIA ,HII INAPITA ,ANGALIA MIFANO YA BURE ILI UPATE ELIMU YA TUTAKUENZI UKITUACHIA NCHI HII KATIKA MITO YA ILIYOJAA MAZIWA,JINA LAKO LITATUKUZWA KWA VIZAZI VYAKO. JK TUNAIMANI NCHI YETU NI TAJIRI SANA MARA ELFU 10, LAKINI MATATIZO NI NYINYI MNAOTAKA KUTANGULIZA MASLAHI YENU, MKIIACHA NCHI HAIFAI KILA MIAKA MNAYOENDELEA KUTAWALA,MKIWADANGANYA WANANCHI KAMA WATOTO. JK IKIFIKA MPAKA JESHI LA NCHI NYINGINE WANAPANDA MPAKA JUU YA PAA YA IKULU, INASIKITISHA KWA KWELI, KWANI NDIPO MLIPOTUFIKISHA KUWA DHALILI KIASI HIKI NADHANI HAMTARUDIA KOSA HILO, JK IBADILISHE NCHI HII KWANI INAWEZEKANA KWA ASIMILIA 100,KAMA UTAKUWA TOFAUTI NA WALIOKUTANGULIA,ONDOA KINGA YA KUZUIA MAFISADI KUSHITAKIWA ,TUNATAKA WEWE UKISTAAFU KUSIWEPO NA NAKINGA YOYOTE KWAKO NA KWA WENGINE ILI SHERIA ICHUKU NAFASI YAKE. TUNA HASIRA SANA JK KWANI TUNA HAKIKA NYINYI NDIO MNAOTUSABABISHIA HALII,KWA MASLAHI YENU,TUNAKUTEGEMEA JK TIMIZA AHADI ZAKO AMBAZO ULIWAAHIDI WADANGANYIKA WAKO,MPAKA SASA HAKUNA HATA MOJA ULILOFANIKIWA KWA KWASABABU YA KUKUMBATIA UOZO WA VIONGOZI.
KWA SHAURI JK UKIWA MWENYEKITI WA CHAMA CHAKO USIKUBALI CHAMA CHAKO NDIO KIMBILIO LA MAFISADI WALA RUSHWA KWA KUWAPIGIA KAMPENI CHAFU ILI WASHINDE UCHAGUZI,TUWACHIE SISI WANANCHI TUTACHAGUA WENYEWE,MSITUGHILIBU NA HELA ZENU CHAFU,NA MIZIKI YENU,JK UNAJUA KUWA USHINDI WENU KATIKA UCHAGUZI NI KWA MCHEZO MCHAFU NDIO MAANA WANAPATIKANA VIONGOZI WACHAFU NA HATIMAE UNAWAJAZA KATIKA MABARAZA YA MAWAZIRI,UNATEGEMEA KUVUNA NINI NA VIONGOZI WAAINA HIYO.
ILANI,KUANZIA LEO IWE MWISHO KUMWITA YEYOTE SHUJAA KWA SABABU YA UFISADI ALIOUFANYA, UTAPATA AIBU.NINI UNACHOTAKA KUTOKA KWAKE. MWACHE DUNIA NDIO ITAHUKUMU NA WALA SIO WEWE ETI KWA SABABU NI RAIS KAULI YAKO INAHESHIMIKA USITUMIE NAFASI HII ADIMU. NIKWELI NA KWAMBIA EL HAKUSINGIZIWA UFISADI HAKUANZIA KWAKO NI TOKEA ZAMANI,HUYO RAFIKI YAKO NI WA SIASA TU JIHADHARI NAYE, ANANYUMBA ZAIDI YA 30 ARUSHA ZIPO KWA MAJINA YA WATU NA HAO WATU UKIWAFUATILIA NA TRA HAWAWEZI KUSEMA WAMEPATA WAPI PESA HIZO, JK FANYA KWELI NADHANI UNAJUA YALIYOTOKEA KATIKA VIWANDA VYA SUKARI KILOMBERO NA WEWE UKANUSURU, USIFIKIRI HATUJUI, TUNAJUA YOTE KUHUSU BWM ALIVYOTUIBIA. TUNAKUSHUKURU

AHSANTE
SEFF
 
Hizo takwimu hazina ukweli wowote, hata HabariLeo la leo title ya habari hiyo kwenye gazeti hili inasema "Makamu wa Raisi Adanganywa" inawezekana wale walio-upload kwenye mtandao wamepitiwa.

Hii habari ninaisoma kwenye habari leo kwenye habari za kitaifa chini ya kichwa "Wachimbaji wadogo Mara kutengewa maeneo". Na katika habari hiyo, inaonyesha mkuu wa mkoa anatoa taarifa kwa makamu wa rais kama ilivyonukuliwa. Yawezekana takwimu alizotoa mkuu wa mkoa si sahihi?

Hiyo ya Dr. Shein adanganywa ni kitu kingine kinachohusiana na ziara aliyofanya kwenye kiwanda cha kusindika minofu ya samaki. Kwa hiyo kuna habari mbili tofauti zenye heading tofauti.
 
BWM - LAMADA ILIYOPO ILALA
-MRADI WA KIWILA (TANESCO ITALIPA MILLIONI300 KILA SIKU
UKIWA TAYARI.
- HOTELI YA NYOTA 3 AFRIKA KUSINI.
.....
AHSANTE
SEFF
Ingependeza iwapo ingekuwa katika maandishi madogo...
 
Back
Top Bottom