Ukishafikisha miaka 20 na kuendelea na bado unawategemea wazazi kwa asilimia 100, umekwisha

Wazazi wanatakiwa kutoa elimu ya kujitambua mara kwa mara kwa vijana awe wa kike au wa kiume, mfano kijana wa miaka 20 awe wa kike au wa kiume unatakiwa kuamuka Asubuhi sana hata Kama huendi popote amka oga, vaa vizuri Anza kujishughulisha na kazi za nyumbani, osha choo na bafu, deki nyumba, fagia mazingira, lima hata bustani Kama Kuna eneo, futa madirisha, tandika kitanda, yaani iwe mwiko kukaa na kuangalia TV muda wa saa nne na mchana, kingine vijana msipende kwenda kuishi kwa shemeji ndo kumeharibu muelekeo wa wengi, imagine unaenda kwa shemeji Ili uonekane active unaamka unanyoosha nguo za shemeji yako na akienda kazini unashinda ungalia TV na shemeji Hana muda wa kukufundisha maadili sana sana utafanya kazi za kujenga familia ya dada yako ukija kushituka umri umeenda Bora ungekaa kwenu ukawa unatafuta mwelekeo wa maisha yako.
 
Back
Top Bottom